Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Tafuna punje 2 za Kitunguu saumu na punje 4 za Karafuu Upate faida hizi kwa afya yako

Ni kwa wastani wa punje 4 tu za karafuu na punje 2 za kitunguu saumu, ukiweka utaratibu wa kuzitafuna kwa pamoja angalau mara moja kila siku kuna faida nyingi unazoweza kuzipata kutoka kwenye virutubisho vyake.
Punje hizo za karafuu na kitunguu saumu zinatosha kuupatia mwili wako madini, vitamin na virutubisho vingine vingi muhimu kwa afya yako.

Inasaidia kuongeza kinga ya mwili.
Tafiti zimeonesha kuwa baadhi ya virutubisho kwenye kitunguu saumu vinasaidia kuongeza kinga ya mwili na kukukinga na magonjwa mbalimbali.
Pia virutubisho vingine kwenye kitunguu saumu vimeonekana kudhibiti baadhi ya virusi mwilini hasa virusi vya mafua.

Inasaidia kuimarisha afya ya ubongo.
Kutokana na uwepo wa madini ya manganese kwa wingi kwenye kitunguu saumu na karafuu inasaidia kuimarisha afya ya ubongo.
Inasaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiri na kutunza kumbukumbu.

Inasaidia kuimarisha mifupa.
Madini ya manganese kwenye kitunguu saumu na karafuu yanasaidia kuongeza ujazo kwenye mifupa na kuifanya iwe imara.

Inasaidia kusafisha mwili na kuzilinda seli za mwili zisiharibiwe kirahisi.
Virutubisho kwenye karafuu na kitunguu saumu vinasaidia kusafisha mwili, itakusaidia kukukinga na magonjwa ya muda mrefu na yasiyo ya kuambukiza kwa kuzilinda seli za mwili zisiharibiwe kirahisi na kemikali mbaya mwilini.
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa baadhi ya virutubisho kwenye karafuu vinasaidia kuimarisha afya ya ini, na kulilinda ini lisiharibiwe na baadhi ya sumu mwilini.

Ni kinga dhidi ya saratani.
Baadhi ya tafiti za maabara zimeonesha kuwa virutubisho kwenye karafuu vina msaada wa kudhibiti ukuaji wa baadhi ya seli za saratani mwilini.

Ni tiba na kinga ya matatizo ya meno na kinywa.
Baadhi ya virutubisho kwenye karafuu vimeonekana kuwa na uwezo wa kudhibiti bakteria hatari hasa wanaosababisha matatizo ya meno na matatizo mengine ya kinywa kama vile harufu mbaya mdomoni, kuvimba fizi na kutoka damu kwenye fizi.

Tiba ya vidonda vya tumbo vya tumbo.
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa virutubisho kwenye karafuu na kitunguu saumu vina uwezo wa kudhibiti bakteria wa H.Pylori, bakteria ambao kwa asilimia kuwa husababisha vidonda vya tumbo.

Inasaidia kuimarisha afya ya moyo.
Virutubisho kwenye kitunguu saumu vimeonekana kuwa na msaada wa kuimarisha afya ya moyo kwa kusaidia kudhibiti mafuta mabaya cholesterol kwenye damu na kusaidia kushusha shinikizo la damu kwa wenye tatizo la presha kupanda.

Inasaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
Baadhi ya tafiti za maabara na kwa wanyama virutubisho vya karafuu vimeonekana kuwa na uwezo wa kudhibi kiwango cha sukari kwenye damu kwa kuchochea uzalishaji wa homoni ya insulin na kuchochea ufyonzaji wa sukari kutoka kwenye damu kuingia kwenye seli za mwili kwa matumizi yake ya kawaida.

Inasaidia kuongeza umri wa kuishi.
Katika ripoti ya utafiti kwa watu wa china, mwaka 2019 ilionesha kuwa wazee waliokuwa wakila kitunguu saumu angalau kila wiki waliishi kwa muda mrefu zaidi kuliko wazee ambao walikuwa hawatumii kitunguu saumu kila wiki.
Sababu kubwa ikizaniwa kuwa ni uwezo wa kitunguu saumu kuimarisha kinga ya mwili kupambana na magonjwa ya kuambukiza ambayo ni magonjwa yanayowasumbua wazee kwa asilimia kubwa.

0
0