Tumia vyakula hivi kusafisha Figo zako
Figo ni moja kati ya viungo muhimu sana kwenye mwili wako.
Kwa kawaida binadamu ana figo mbili mwilini.
Figo hufanya kazi kubwa ya kusafisha damu mwilini baada ya ulaji na unywaji wa vitu mbalimbali.
Unywaji wa maji kwa wingi, kuzingatia ulaji wa baadhi ya vyakula na mtindo mzuri wa maisha unazisaidia figo zako kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Ili kuweka Figo zako katika usalama jambo la kwanza la kuzingatia ni kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha.
Kwa mwanamke wastani wa lita 2.7, sawa na glasi 11 na nusu za maji kwa siku.
Kwa mwanaume wastani wa lita 3.7, sawa na glasi 15 na nusu za maji kwa siku.
Kunywa maji ya kutosha kunazisaidia figo zako kuchuja taka mwili kirahisi mwilini.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi ili kuimarisha afya ya Figo zako unashauriwa kutumia vyakula ambavyo
havina na vinavyosaidia kuondoa mafuta mabaya yanayoweza kuganda kwenye mishipa ya damu, kama vile mafuta mabaya ya cholesterol.
Kula vyakula vyenye protini kwa wingi,
Mboga za majani na matunda kwa wingi.
Kuna baadhi ya vyakula pia vinaweza kusaidia kuimarisha afya ya figo zako kama vile:
Mwani:
Baadhi ya tafiti zilizofanywa haswa kwenye mwani wa kahawia(Brown) zilionesha kuna msaada wa virutubisho vyake
kwenye kongosho, figo na ini.
Utafiti huo uliofanywa kwa panya waliokuwa wanakula mwani kwa siku 22 mfululizo walionekana kupunguza kwa kiasi kikubwa
magonjwa ya figo na ini.
Zabibu:
Utafiti uliofanywa kwa wanyama kwenye zabibu nyekundu uligundua kuwa juisi ya zabibu nyekundu na zabibu zilizokaushwa
zinauwezo wa kudhibiti vichocheo vya magonjwa na kuondoa sumu, hali inayosaidia kuzilinda figo, mafuta mabaya yasigande kwenye Figo
na kuimarisha afya ya figo.
Njia nyingine muhimu ya kuzilinda figo zako ni ulaji wa vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi ili kuzuia mawe kwenye figo.
Madini ya calcium yanasaidia kuyeyusha mawe kwenye figo.
Ili kuhakikisha mwili wako unapata madini ya calcium kwa wingi zingatia,
Unywaji wa maziwa na bidhaa zingine za maziwa zilizopunguzwa mafuta kama vile Yogurt,
Ulaji wa nyama isiyo na mafuta,
Na ulaji wa kunde.
Unaweza pia kusoma: