
Karafuu tiba asili ya vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo ni vidonda kwenye kuta za mfumo wa chakula ambavyo mara nyingi hutokea kwenye koo la chakula, kwenye mfuko wa chakula au kwenye utumbo mwembamba.
Mara nyingi vidonda husababishwa na kukosekana kwa ulinzi kwenye kuta za mfumo wa chakula.
Ulinzi kwenye kuta za mfumo wa chakula unaimarishwa na uteute ambao unazuia vimeng’enywa vya chakula visifike kirahisi kwenye kuta hizo.
Inapotokea vimeng’enywa vya chakula kufika kwenye kuta vinaweza kuchubua kuta na kusababisha vidonda.
Moja kati ya vimeng’enya hatari ni tindikali inayozalishwa kwenye mfuko wa chakula.
Ni rahisi kwa tindikali kusababisha vidonda kwenye mfumo wa chakula kama itakutana moja kwa moja na kuta za mfumo wa chakula.
Sababu za mara kwa mara zinazoweza kupunguza ulinzi kwenye kuta ni kama vile msongo wa mawazo, maambukizi kwenye mfumo wa chakula na matatizo mengine ya kuzaliwa nayo.
Karafuu ni vipande vya maua kutoka kwenye mti wa mkarafuu.
Mara nyingi karafuu hutumika kama kiungo, kuongeza ladha ya chakula, pia hutumiwa kama manukato kwenye
bidhaa mbalimbali kama vile dawa za meno, sabuni na vipodozi.
Karafuu ina virutubisho vingi mbalimbali muhimu kwa afya ya binadamu.
Ulaji wa karafuu unasaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile mafua, kikohozi, maumivu ya kicha n.k
Tafiti zimeonesha kuwa karafuu ina kirutubisho kinachoitwa eugenol moja kati ya virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu.
Kirutubisho cha eugenol kinaongeza uzalishaji wa uteute kwenye kuta za mfumo wa chakula.
Uteute huo kwenye kuta za mfumo wa chakula unasaidia kuzuia kuta hizo zisiharibiwe na vimeng’enywa vya chakula na kusababisha vidonda.
Licha ya kuzuia kuta zisichubuliwe na vimeng’enywa pia kwa watu ambao wana vidonda tayari inasaidia kuzuia vidonda visiendelee kuchubuka.
Uteute huo pia unaziba kidonda na kukifanya kipone kwa haraka.
Tafiti zimeonesha kuwa kula angalau kijiko kimoja cha chai cha karafuu kila siku kwa angalau siku 28 mfululizo inasaidia kupata matokeo mazuri zaidi.
Unaweza kula karafuu kwa kutafuna punje zake zenyewe bila kuchanganya na kitu chochote pia unaweza kusaga karafuu na unga wake ukautumia
kuchanganya na vyakula au vinywaji vingine.
Unaweza pia kusoma: