Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Faida za Asali kwa afya

Asali ni kimiminika cha asili kinachotengenezwa na nyuki kwa mkusanyiko wa nectar kutoka kwenye mimea.
Asilimia kubwa ya asali ni sukari ya asili, ina kiwango kidogo sana ya virutubisho vingine, nyuzi lishe, mafuta na protini.
Licha ya kuwa na sukari nyingi na uchache wa mafuta, protini na nyuzi lishe, asali pia ina wingi wa virutubisho vingine muhimu kwa afya kutoka kwenye mimea tofautitofauti.
Asali imekuwa ikitajwa sana kuwa ni moja kati ya vinywaji vya asili vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu na kutumiwa kama tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya.

Tuzifahamu faida mbalimbali za kiafya za kunywa asali kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi.

Husaidia kusafisha mwili.
Asali ambayo bado haijapitia kwenye michakato mingi ya uandaaji wake ina viondoa sumu mwilini, na asali nyeusi ina wingi wa viondoa sumu hivyo kuliko asali nyeupe.
Viondoa sumu hiyo husaidia kusafisha kemikali hatari mwilini ambazo zinaweza kuharibu seli za mwili kama zikijikusanya nyingi ndani ya mwili.
Kusafisha mwili kunasaidia kukukinga na magonjwa ya muda mrefu kama vile magonjwa ya moyo na kisukari.
Pia inasaidia kuchelewesha dalili za uzee.

Inadhibiti wingi wa sukari kwenye damu kulinganisha na sukari ya kawaida.
Ni muhimu kwa wenye tatizo la kisukari kutumia asali kama mbadala wa sukari ya kawaida kwasababu asali inasaidia kudhibiti madhara ya sukari kwenye damu.
Asali kama sukari zingine inaongeza sukari kwenye damu ila kwasababu ya virutubisho vyake vingine vinasaidia kudhibiti madhara ya sukari hiyo mwilini.
Licha ya kuwa asali imeonekana kuwa ni nzuri kwa matumizi kuliko sukari ya kawaida sio sababu ya kuitumia kwa fujo, tumia kwa kiasi kiafya.

Husaidia kuimarisha afya ya moyo. Unaweza kutumia asali kama kinga dhidi ya matatizo ya moyo, kwa mujibu wa tafiti mbalimbali asali imeonekana kusaidia kushusha shinikizo la damu, kudhibiti kiwango cha mafuta kwenye damu, kurekebisha mapigo ya moyo na kuzuia seli hai za mwili kufa.
Yote hayo yana mchango mkubwa wa kuimarisha afya ya moyo na mfumo wa damu mwilini.

Husaidia kuponesha vidonda na majeraha ya moto.
Matumizi ya asali kama tiba mbadala wa vidonda na majeraha ya moto yana historia ndefu sana na mpaka sasa bado watu wanaamini katika uwezo huo wa asali.
Pia baadhi ya tafiti zimethibitisha uwezo huo wa asali, ila kwa majeraha ya moto ambayo hayajachimba ndani sana kwenye ngozi.
Kwa majeraha ya moto yalichimba zaidi ndani ya ngozi haishauriwi kutumia asali kabla ya kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

Husaidia kutuliza kikohozi kwa watoto.
Tafiti mbalimbali kwa asali na kikohozi kwa watoto zimeonesha uwezo mkubwa wa asali kusaidia kutuliza kikohozi kwa watoto na kusaidia kikohozi kupona haraka.

Jambo la muhimu la kuzingatia, usimpe mtoto mwenye chini ya mwaka 1 asali kuna athari za kiafya anaweza kuzipata.
Haishauriwi kumpa kabisa mtoto chini ya mwaka 1 hata kiasi kidogo tu cha asali.

Pia kuna baadhi ya watu wana allergy na asali, kama utatumia asali na kuona dalili zozote za mzio kama vile dalili za asthma, kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na mwili kuishiwa nguvu acha kutumia asali.

0
0