Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Changanya Karafuu, Tangawizi na Asali upate faida hizi kwa afya

Tengeneza chai iliyo changanywa karafuu na Tangawizi ichemke angalau kwa dakika 5 mpaka 10 na kisha utumie asali kama sukari yako kwenye chai hiyo.

Kutumia chai hiyo mara kwa mara inaweza kukupa faida hizi zifuatazo kwa afya yako.

Inasaidia kusafisha mwili.
Virutubisho vya Karafuu, Tangawizi na Asali vinasaidia kuondoa kemikali hatari mwilini na kuzilinda seli za mwili zisiharibiwe na kemikali hizo.
Kusafisha mwili itakusaidia kukukinga na magonjwa ya muda mrefu na yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari na magonjwa ya moyo.
Pia itakusaidia kuimarisha afya ya ngozi yako na kuzuia dalili za uzee kuonekana mapema kama vile makunyanzi.

Ni kinga dhidi ya saratani.
Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa virutubisho kwenye Karafuu na Tangawizi vinasaidia kuondoa vihatarishi vya kupata saratani.
Tangawizi imeonekana kupunguza hatari ya kupata saratani ya utumbo mpana, kongosho na ini.
Pia Karafuu imeonekana kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.

Inasaidia kuimarisha afya ya ubongo.
Wingi wa madini ya manganese kwenye karafuu unasaidia kuimarisha afya ya ubongo pamoja na virutubisho vingine kwenye Tangawizi vimeonekana kusaidia kuimarisha utendaji kazi wa ubongo.
Vinasaidia kuimarisha uwezo wako kufikiri na kutunza kumbukumbu.
Pia ni kinga ya tatizo la kupoteza kumbukumbu linalosababishwa na kufa kwa seli za ubongo hasa kwa wazee.

Inasaidia kuimarisha mifupa na kuondoa maumivu ya joints.
Karafuu ina wingi wa madini ya manganese ambayo yanasaidia kuongeza ujazo kwenye mifupa na kuifanya iwe imara.
Na kama unasumbuliwa na maumivu kwenye viungo vya mwili Virutubisho kwenye Karafuu na Tangawizi pia vinasaidia kupunguza maumivu hayo.

Tiba ya kuvimbiwa.
Karafuu na tangawizi zinasaidia kuchochea umeng’enywaji wa chakula kwenye mfumo wa chakula.
Kasi ya chakula kupita kwenye utumbo itaongezeka na kukuondolea dalili za kuvimbiwa kwa haraka.

Inasaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
Chai ya Karafuu, Tangawizi na Asali ni muhimu kwa wenye kisukari kwasababu inasaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu hasa inapotumiwa baada ya kula.
Inasaidia kuchochea uzalishaji wa homoni ya insulin mwilini na kuchochea ufyonzaji wa sukari kutoka kwenye damu kwenda kwenye seli za mwili kwa matumizi yake ya kawaida.

Inasaidia kuua baadhi ya bakteria hatari mwilini.
Karafuu, Tangawizi na Asali virutubisho vyake vimeonekana kuwa na uwezo wa kuua baadhi ya bakteria hatari mwilini hasa bakteria wanaosababisha matatizo ya meno na kinywa, wanaosababisha magonjwa ya tumbo na magonjwa ya ngozi.
Pia virutubisho kwenye Karafuu na Tanagawizi vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu fangasi hasa aina ya candida wanaosababisha fangasi mdomoni na ukeni.

0
0