Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Nguvu ya mchanganyiko wa asali na limao kwa afya

Limao na asali ni vitu viwili tofauti na kila kimoja kina faida zake kwa afya ya binadamu.
Ila unapovichanganya vyote asali na limao kwenye maji ya moto au chai inaongeza nguvu zaidi na kukupa faida zaidi za kiafya.
Asali ina wingi wa viondoa sumu mbalimbali mwilini, madini na vitamin mbalimbali muhimmu kwa afya.
Pia limao lina wingi wa vitamin C na virutubisho vingine muhimu kwa kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa sumu mwilini na kuimarisha afya ya mfumo wa chakula.
Katika makala hii tuziangalie faida za pamoja za kuchanganya limao na asali kwa afya.

Husaidia kuondoa sumu mwilini:
Mchanganyiko wa asali na limao unasaidia kusafisha mwili kwa kuondua sumu mwilini. Ili kupata matokeo mazuri inashauriwa kunywa mchanganyiko huo tumbo likiwa halina kitu ukiwa haujala kitu chochote.

Husaidia kuupa mwili nguvu:
Kinywaji mchanganyiko wa asali na limao ni chanzo cha haraka cha nguvu mwilini, ni kinywaji kizuri wakati au baada ya kazi au mazoezi.

Husaidia kuimarisha kinga ya mwili:
Kinga ya mwili kutokuwa imara ni chanzo cha magongwa ya mara kwa mara. Kinywaji mchanganyiko wa asali na limao ni chanzo kikubwa cha vitamin C mwilini na virutubisho vingine ambavyo vinasaidia kuimarisha kinga ya mwili.

Husaidia kuimarisha mfumo wa chakula:
Asali na limao kwenye maji ya moto husaidia kukukinga na matatizo kwenye mfumo wa chakula kama vile kupata choo kigumu kwasababu inasaidia kusafisha utumbo na kuondoa mabaki ya chakula kisichomeng’enywa.

Husaidia kuimarisha afya ya ngozi: Kinywaji cha asali na limao kinasaidia kuimarisha afya ya ngozi kwa kuifanya ngozi kuwa laini na yenye mng’ao kwasababu inasaidia kusafisha damu na kuongeza uzalishaji wa collagen kwenye ngozi.

Kinga ya mawe kwenye figo:
Uwezo wa asali wa kuua bacteria jumlisha na uwezo wa limao kutoa mkojo kwenye figo kwa pamoja inasaidia kusafisha figo na kukukinga na tatizo la mawe kwenye figo.

Huimarisha afya ya moyo:
Wingi wa vitamin C kwenye kinywaji cha asali na limao unasaidia kuimarisha afya ya moyo na kukukinga na matatizo mengine kama vile kiharusi.
Hii ni kwasababu vitamin C husaidia kuondoa mafuta mabaya ya cholesterol mwilini ambayo huhatarisha afya ya moyo.

Tiba ya kuvimba miguu:
Kuvimba miguu ni matokeo ya kuongezeka kwa maji mwilini kwasababu mbalimmbali za kiafya.
Kwasababu ya uwezo wa kinywaji cha asali na limao kuchochea figo kutoa mkojo inasaidia kupunguza maji hayo mwilini.
Ila sio kila kuvimba miguu husababishwa na kujaa maji kuna sababu zingine ambazo zinaweza kusababisha tatizo hilo.

0
0