Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Karafuu kinga dhidi ya Saratani

Saratani ni tatizo la kukosekana kwa mpangilio wa ukuaji wa seli mbalimbali ndani ya mwili.
Kukosekana kwa udhibiti wa ukuaji wa seli hizo mwilini husababisha kuwa na uvimbe na wakati mwingine huingiliana na shughuli mbalimbali mwilini.
Ukuaji wa seli hizo mwilini unaweza kuingiliana na shughuli za mwili na kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Karafuu ni vipande vya maua kutoka kwenye mti wa mkarafuu.
Mara nyingi karafuu hutumika kama kiungo, kuongeza ladha ya chakula, pia hutumiwa kama manukato kwenye bidhaa mbalimbali kama vile dawa za meno, sabuni na vipodozi.
Karafuu ina virutubisho vingi mbalimbali muhimu kwa afya ya binadamu.
Ulaji wa karafuu unasaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile mafua, kikohozi, maumivu ya kicha n.k

Pia tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa karafuu ina virutubisho muhimu kwa mwili vinayosaidia kuukinga mwili dhidi ya saratani.
Utafiti mmoja maabala uligundua kuwa virutubisho kwenye karafuu vinasaidia kuzuia ukuaji wa seli za saratani na kuziua seli za saratani mwilini.
Pia utafiti mwingine uligundua kuwa mafuta halisi ya karafuu yana uwezo wa kuziua takribani asilimia 80 ya seli za saratani ya kwenye koo la chakula.
Utafiti mwingine ukafanikiwa kugundua kuwa kuna kirutubisho cha Eugenol kwenye karafuu ambacho kimeonekana kuwa na uwezo wa kuua seli za saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
Virutubisho kama eugenol kwenye karafuu ni hatari vikitumiwa kwa wingi na mafuta ya karafuu vikitumiwa kwa wingi vinaweza kuleta madhara kwenye ini hasa kwa watoto wadogo.
Kwasababu hiyo unashauriwa kutumia karafuu kwa kiasi kidogo tu na muhimu kwa kuchanganya na vyakula au vinywaji vingine kuliko kula sana karafuu yenyewe.

0
0