Kabla ya kutumia Mlonge zingatia mambo haya
Mti wa mlonge ni moja kati ya miti maarufu sana kwenye maswala ya tiba asili.
Tafiti mbalimbali zimegundua virutubisho zaidi ya 90 vyenye msaada kwa afya kwenye mti wa mlonge.
Virutubisho hivyo vimeonekana kusaidia kuondoa sumu mwilini, kudhibiti vimelea vya magonjwa kama vile fangasi na kinga dhidi ya saratani.
Kwenye mti wa mlonge, magome, mbegu na majani vinaweza kutumika kupata virutubisho vyake.
Kuna baadhi ya jamii zinautumia mlonge kama mboga.
Licha ya kuwa na faida zake nyingi kwa afya kuna baadhi ya mambo ni muhimu kuyazingatia unapotaka kutumia mti huu wa mlonge.
Kwa kutumia kula majani na mbegu za mlonge ni salama kwa kula.
Mizizi na magome ya mizizi ya mti wa mlonge yameonekana kuwa si salama kwa kula kwasababu ya uwepo wa sumu kwenye mizizi.
Kwa mjamzito, ni salama kutumia mlonge kuanzia miezi minne ya ujauzito na kuendelea.
Sio salama kwa mjamzito kutumia mizizi, magome na maua ya mlonge.
Baadhi ya kemikali kwenye mizizi, magome, na maua ya mlonge yanaweza kusababisha mfuko wa kizazi kujiminya hali inayoweza kusababisha
mimba kutoka au kuharibika.
Kuna ushahidi wa baadhi ya jamii zilitumia mizizi na magome ya mti wa mlonge kutoa mimba.
Kwa mama anayenyonyesha, imeonekana kuwa majani ya mlonge pekee ni salama kutumia kwa kipindi cha miezi mnne pekee.
Hakuna tarifa za kutosha kuhusu sehemu zingine za mti wa mlonge kwa mama anayenyonyesha hivyo ni vizuri kuepuka matumizi ya sehemu nyingine
za mlonge kama una nyonyesha.
Kwa watoto, majani ya mlonge yameonekana kuwa na usalama kuliwa kwa kipindi cha miezi miwili tu kwa watoto.
Kwa wenye tatizo la upungufu wa homoni ya thyroid mwilini, tafiti zimeonesha kuwa matumizi ya mlonge yanaweza kufanya tatizo
hili kuwa baya zaidi.
Kama una tatizo hili ni vizuri kuepuka matumizi ya mlonge.
Kwa wenye tatizo la kisukari, kama unatumia dawa za kisukari haishauriwi kutumia mlonge kwasababu mlonge unasaidia
kushusha sukari kwenye damu.
Kwasababu hiyo kama unatumia dawa za kisukari mlonge unaweza kusababisha sukari ikashuka zaidi kwenye damu kuliko kawaida.
Unaweza pia kusoma: