Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Kwenye picha imeonesha mwanaume akiwa ameshikilia kikombe pia akiwa ameshikilia koo lake, pia imeonesha Karafuu
			zikiwa zimemwagwa chini katikati kukiwa na bakuli la asali.

Karafuu na asali tiba asili ya kikohozi na mafua

Karafuu hivi ni vipande vidogo kutoka kwenye maua ya mti wa karafuu.

Kwa wanasayansi unaitwa Syzygium aromaticum.

Licha ya kuwa ni vipande vya maua ndani yake kuna utajiri wa virutubisho vingi muhimu kwa afya ya binadamu.
Na Karafuu inatumika na imekuwa ikitumika toka zamani kama tiba ya magonjwa mbalimbali ya binadamu.

Kwa Sukari ya asili, hii hutengenezwa na nyuki kwa kukusanya necta kutoka kwenye mimea tofauti tofauti.
Asali licha ya kuwa ni sukari ya asili ila ina wingi wa virutubisho vingine muhimu kwa afya ya binadamu.

Karafuu peke yake unaweza kuitumia kama tiba ya kifua na mafua, pia asali nayo unaweza kuitumia kama tiba ya kifua.

Ila Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa mchanganyiko wa asali na karafuu una nguvu zaidi ya kutibu kifua na mafua kuliko kutumia karafuu au asali peke yake.
Ikiwa unahisi koo lako linawasha washa, unakohoa au pua inaloa na kamasi msaada wako wa haraka ni karafuu changanya na asali.

Chukua vipande 5 vya karafuu vitwange upate unga unga, changanya na kijiko cha chakula kimoja cha asali kisha koroga uchanganye.
Mchanganyiko huo wote unaweza kuutumia mara 2 mpaka 3 kwa siku.

Mchanganyiko wa asali na karafuu una nguvu ya kupambana na virusi pamoja na bakteria kwenye mfumo wa upumuaji.

Kama una mambukizi kwenye mfumo wa upumuaji unaokusababishia kifua au mafua, mchanganyiko wa asali na karafuu ni tiba nzuri unayoweza kuitumia.

Msaada mkuu wa karafuu ni kupunguza muitikio wa magonjwa na kusafisha mwili.

Karafuu inasaidia kupunguza muitikio wa maambukizi kwenye njia ya hewa ambayo yanasabisha kikohozi au mafua.

Asali pia inasaidia kusafisha mwili na kusaidia virutubisho vingine kufyonzwa vizuri mwilini ili kupata matokeo mazuri ya virutubisho hivyo.

Karafuu tiba asili ya kisukari.

Karafuu tiba asili ya meno na fidhi

Karafuu tiba asili ya vidonda vya tumbo

Karafuu kinga dhidi ya Saratani

Nguvu ya mchanganyiko wa asali na limao kwa afya

0
0