Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Karafuu tiba asili ya kisukari.

Karafuu ni vipande vya maua kutoka kwenye mti wa mkarafuu.
Mara nyingi karafuu hutumika kama kiungo, kuongeza ladha ya chakula, pia hutumiwa kama manukato kwenye bidhaa mbalimbali kama vile dawa za meno, sabuni na vipodozi.
Karafuu ina virutubisho vingi mbalimbali muhimu kwa afya ya binadamu.
Ulaji wa karafuu unasaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile mafua, kikohozi, maumivu ya kicha n.k

Tafiti zimeonesha pia virutubisho vya karafuu vinasaidia kudhibiti kiwango cha sukari mwilini. Kiasi cha kijiko kimoja tu cha chai kinatosha kumpa mtu faida hizo za karafuu. Tafiti zimeonesha kuwa virutubisho vya karafuu vina uwezo wa kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu mara tu baada ya kumaliza kula chakula kisha ukala karafuu. Katika virutubisho vya karafuu kuna asilimia 30 ya mjumuisho wa virutubisho aina ya polyphenol.

Tafiti zimeonesha kuwa virutubisho hivyo vina faida mbalimbali za kiafya ndani ya mwili. Vina faida kwenye ini na sehemu nyingine mwilini muhimu kwa utendaji kazi wa homoni ya insulin. Homoni ya insulin ni homoni muhimu inayodhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Homoni ya insulin kushindwa kufanya kazi vizuri mwilini inasababisha kiwango cha sukari kuongezeka mwilini. Pia virutubisho vya karafuu vimeonekana kusaidia kushusha kiwango cha sukari kwenye damu kwa kufanya mambo yafuatayo mwilini:

Inachochea ufyonzaji wa sukari kwenye misuli sehemu mbalimbali mwilini na kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu. Inazuia uzalishaji wa sukari ya ziada kutoka kwenye ini kuingia kwenye damu. Pia virutubisho hivyo vinazuia vimeng’enywa vya chakula kumeng’enya vyakula vyenye sukari ili visiongeze sukari kwenye damu.

Katika utafiti uliochapishwa mwaka 2019, watu wenye kisukari baada ya kupewa virutubisho vya karafuu muda mchache baada ya kula kiwango chao cha sukari kwenye damu kilionekana kushuka kulinganisha na watu ambao hawakutumia karafuu. Pia virutubisho hivyo vya karafuu vimeonekana kuwa na uwezo wa kuzibiti kiwango cha sukari mwilini kwa siku nzima.

Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa watu ambao wanatumia dawa za hospitali kudhibiti kisukari. Kama tayari unatumia dawa za hospitali haushariwi kutumia karafuu, ni muhimu kwanza kumuona daktari kwa ushauri zaidi.

0
0