Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Karafuu tiba asili ya meno na fidhi

Karafuu ni vipande vya maua kutoka kwenye mti wa mkarafuu.
Mara nyingi karafuu hutumika kama kiungo, kuongeza ladha ya chakula, pia hutumiwa kama manukato kwenye bidhaa mbalimbali kama vile dawa za meno, sabuni na vipodozi.

Karafuu ina virutubisho vingi mbalimbali muhimu kwa afya ya binadamu.

Ulaji wa karafuu unasaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile mafua, kikohozi, maumivu ya kichwa n.k

Karafuu imeonekana kuwa na virutubisho vyenye uwezo wa kuua bacteria mbalimbali.
Pia tafiti zikaonesha kuwa baadhi ya virutubisho kwenye karafuu vina uwezo wa kuzuia ukuaji wa bacteria kinywani wanaosababisha uharibifu wa fizi na meno.

Mafuta ya karafuu ni mafuta yanayokamuliwa kutoka kwenye karafuu yakiwa pamoja na wingi wa virutubisho kutoka kwenye karafuu.
Inashauriwa kutumia mafuta ya karafuu kusukutulia mdomoni kwasababu ya wingi wa virutubisho vya karafuu ambavyo vinasaidia kusafisha kinywa na kuua bacteria hatari mdomoni.

Kwa kusukutulia mafuta ya karafuu mdomoni :

Kwa kusugulia meno na unga wa karafuu au kwa kutumia mafuta ya karafuu:
Inasaidia kuondoa ukungu kwenye meno na vijidudu vingine viliyogandamana kwenye meno na kuyafanya meno kuwa meupe.
Kwasababu inasaidia kuondoa ukungu na kuua vijidudu kwenye meno pia karafuu inasaidia kuyakinga meno yasitoboke.

0
0