Faida ya Mafuta ya Karafuu kwa Afya
Mafuta ya karafuu ni mafuta kutoka kwenye karafuu ambavyo ni vipande vya maua ya mti wa mkarafuu.
Karafuu imeanza kutumiwa kwa matumizi mbalimbali na binadamu toka karne nyingi zilizopita kabla ya kristo.
Mafuta ya karafuu Yamekuwa yakitumiwa pia kwa tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kwa binadamu.
Hii ni kutokana na wingi wa virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu vinavyopatikana kwenye karafuu.
Mafuta ya karafuu unaweza kuyatumia kwa kuchanganya na vyakula vingine ili kupata virutubisho vyake.
Pia unaweza kuyatumia kwa kupaka au kwa kufanyia masaji mwilini.
Baada ya tafiti mbalimbali za kisayansi kwenye mafuta ya karafuu yamethibitika kuwa na faida hizi kwa afya ya binadamu.
Ni Tiba ya maumivu ya jino, unatakiwa kutumia pamba kidogo unayoweza kuiweka kwenye jino lililotoboka,
ichovye kwenye mafuta yoyote ya kupikia, unaweza kutumia mafuta ya nazi au mafuta ya zaituni kama yapo.
Dondoshea tone moja au mawili ya mafuta ya karafuu kwenye pamba hiyo na kisha uiweke kwenye jino linalouma.
Pia ni tiba ya maumivu ya misuli, unaweza kutumia mafuta ya karafuu kufanyia masaji au kujikanda sehemu inayouma.
Ukitumia mafuta ya karafuu kwa kupaka kwenye ngozi inasaidia kuondoa miwasho kwenye ngozi na kutibu michubuko kwenye ngozi kwa haraka zaidi.
Pia tafiti mbalimbali za maabara zimeonesha uwezo wa mafuta ya karafuu kudhibiti ukuaji wa seli za saratani mwilini hasa saratani ya matiti, shingo ya kizazi na utumbo mpana.
Tafiti hizo zilizofanywa maabara bado zinahitaji tafiti nyingine zaidi kuthibitisha uwezo huo kwa binadamu.
Mafuta ya karafuu tafiti zimeonesha kuwa na uwezo wa kutibu fangasi aina mbalimbali pia yameonekana kuwa na uwezo wa kutibu fangasi aina ya candida, fangasi ambao mara nyingi huwasumbu wanawake sehemu za siri.
Pia mafuta ya karafuu tafiti zimeonesha kuwa yana uwezo kuua baadhi ya bakteria wanaosababisha magonjwa kwa binadamu.
Hasa bakteria wanaosababisha magonjwa kwenye mfumo wa upumuaji kama vile homa ya mapafu na mafua.
Unaweza pia kusoma: