Muonekano wa Giza:

Msaada

Faida za kunazi kiafya

Kunazi ni tunda dogo la mviringo lenye mbegu katikati na linapokuwa limeiva rangi yake inabadilika kutoka kijani kuwa na rangi ya damu ya mzee.
Tunda la kunazi toka miaka mingi iliyopita limekuwa likitumiwa kama tiba ya tatizo la kukosa usingizi na tatizo la wasiwasi.
Katika makala hii tuzifahamu faida mbalimbali za kunazi kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi.
Kwanza fahamu kuwa kula tunda la kunazi kunaupa wili wako nyuzi lishe, vitamin na madini chumvi muhimu kwa afya ya mwili.

Ina wingi wa viondoa sumu mwilini:
Kunazi ina wingi wa viondoa sumu ambayo husaidia kuondoa kemikali hatari mwilini ambazo zinaweza kusababisha madhara kwenye seli za mwili na kusababisha magonjwa ya muda mrefu kama vile kisukari, magonjwa ya moyo na saratani.

Husaidia kuimarisha afya ya ubongo na usingizi:
Moja kati ya tiba zilizokuwa zikitumia kunazi miaka ya nyuma kwa sehemu mbalimbali duniani ni kutibu tatizo la kukosa usingi.
Hata hivyo tafiti mbalimbali kwa wanyama zimethibitisha uwezo wa kunazi kusaidia kupunguza tatizo la kukosa usingizi na kumfanya mtu kulala kwa muda mrefu.
Pia husaidia kuondoa wasiwasi na kusaidia kuimarisha afya ya ubongo kwa kuondoa kemikali zinaweza kuua neva za fahamu kwenye ubongo.

Inaweza kusaidia kuimarisha kinga ya mwili na kinga dhidi ya saratani:
Kutokana na uwepo wa viondoa sumu mbalimbali kwenye kunazi husaidia kuukinga mwili dhidi ya magonjwa kwa kuondoa kemikali hatari mwilini.
Pia tafiti kwa wanyama ziligundua kuwa virutubisho vya kunazi husaidia kuimarisha seli za kinga ya mwili ambazo hupambana na magonjwa mbalibali.
Vilevile tafiti kwa wanyama ziligundua kuwa virutubisho vya kunazi vina uwezo wa kuua seli mbalimbali za saratani kama vile saratani ya ovari, shingo ya kizazi, matiti, ini, utumbo mpana na saratani ya ngozi.

Kuimarisha mfomo wa umeng’enyaji wa chakula:
Kwasababu ya uwepo wa nyuzi lishe kwenye kunazi ni lishe muhimu kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa chakula mwilini.
Husaidia kupitisha chakula na kinyesi kwa haraka kwenye mfumo wa chakula kuepusha mgandamano wa chakula au kinyesi kwenye utumbo.
Pia virutubisho vya kunazi vinasaidia kuimarisha kuta za kwenye mfumo wa chakula na kuzikinga zisipate vidonda na zisidhuliwe na bacteria hatari kwenye mfumo wa chakula.

Tunda la kunazi unaweza kulila lenyewe kama matunda mengine kawaida ladha yake ni tamu na muundo wake ni kama tunda la apple.
Pia unaweza kusaga juisi ya matunda ya kunazi na kuitumia kama vinywaji vingine.

Hitimisho
Tunda la kunazi lina wingi wa viondoa sumu mwilini. Tafiti mbalimbali zilizofanywa maabara na kwa wanyama ziligundua kuwa virutubosho vya tunda la kunazi husaidia kuimarisha afya ya ubongo, kuimarisha kinga ya mwili na mfumo wa umeng’enyaji wa chakula.
Hata hivyo tafiti nyingi za kisayansi kwa binadamu zinahitajika kuthibitisha zaidi faida hizo kwa binadamu.

0
0
1