Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Faida za matunda ya Zeituni kwa afya

Mafuta ya mzeituni ni mafuta ambayo yamepata umaarufu kutokana na umuhimu wake kwa afya ya binadamu.
Ni mafuta ambayo haya-gandi kwenye joto la kawaida na ni mafuta ambayo yana virutubisho vingi muhimu kwa afya.
Mafuta ya mzeituni ni mafuta yanayo-kamuliwa kutoka kwenye matunda ya mzeituni.

Tuzifahamu faida za kiafya ambazo mtu anaweza kuzipata kwa kula matunda ya mzeituni.

Haya ni matunda madogo kutoka kwenye mti wa mzeituni, kama yalivyo mafuta yake pia yana virutubisho vingi muhimu kwa afya.
Japo upatikanaji wake nchini ni mchache ila kuna baadhi ya watu wanalima mizeituni na pia unaweza kuyapata kwenye supermarket.

Matunda ya mzeituni yana wingi wa viondoa sumu mwilini pamoja na vitamin E ambavyo husaidia kusafisha mwili na kuzi-kinga seli za mwili zisiharibiwe kirahisi.
Hivyo matunda ya mzaituni ni kinga ya saratani na ni kinga ya matatizo ya uzeeni kama vile kupoteza kumbukumbu yanayosababishwa na kufa kwa seli za ubongo.

Matunda ya mzaituni yana wingi wa madini chuma ambayo yanasaidia katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu hivyo ni muhimu kwa wenye matatizo ya upungufu wa damu (Anemia).

Yana madini ya shaba ambayo husaidia kuimarisha afya ya moyo.

Yana madini ya calcium ambayo husaidia kuimarisha mifupa, misuli na mishipa ya fahamu mwilini.

Ulaji wa mara kwa mara wa matunda ya mzaituni:

Matunda ya mzaituni yana wingi wa nyuzi lishe ambazo zinasaidia kuimarisha mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kusaidia kutibu matatizo mbalimbali ya tumbo na kulainisha choo.
Pia nyuzi lishe ni kinga ya magonjwa ya moyo.

Kama upo kwenye diet ya kupunguza uzito nyuzi lishe na mafuta kwenye zaituni zita-kusaidia kuhisi tumbo limejaa kwa muda mrefu bila kula.

Vitamin E kwenye zaituni inaweza kusaidia kuondoa maumivu na uvimbe mwilini kama kwa mtu mwenye bawasili.

Baadhi ya virutubisho kwenye matunda ya mzaituni tafiti zimeonesha vina uwezo wa kuzuia ukuaji wa seli za saratani kwenye matiti, utumbo mpana na kwenye tumbo la chakula.
Kuhusiana na hilo bado tafiti nyingine zaidi zinahitajika kuthibitisha uwezo huo wa virutubisho vya zaituni kuthibiti seli za saratani kwa binadamu.

0
0