Muonekano wa Giza:

Msaada

Pichani kuna kielelezo cha mtu kinachoonesha viungo vya ndani ya kifua hasa moyo na mishipa yake ya damu na pembeni kuna picha ndogo ya mviringo ya vipande vya karafuu.

Karafuu ni Muhimu kuimarisha Afya ya Moyo

Karafuu ni kiungo cha chakula, mara nyingi hutumiwa kuongeza ladha ya chakula.
Kibaolojia Karafuu ni Maua.
Maua yanayopatikana kwenye mti wa mkarafuu.
Maua hayo hukaushwa ili kupata vipande hivyo vya Karafuu.

Vipande hivi vya Karafuu hutumiwa vizima au vikiwa vimesagwa na kutumia unga wake.
Karafuu pia inaweza kutumiwa ikiwa imechanganywa kwenye chakula, chai au juisi ya matunda.

Licha ya uwezo wake wa kuongeza ladha kwenye vyakula pia Karafuu imegundulika kuwa na virutubisho muhimu kwa afya ya binadamu.

Virutubisho vya Karafuu muhimu kwa afya:

Karafuu ni Muhimu kwa Afya ya Moyo kwasababu zifuatazo:

Inasaidia kupunguza vichochezi vya magonjwa.

Kirutubisho cha Eugenol kwenye Karafuu ni moja ya kirutubisho muhimu mwilini kinachosaidia kupunguza vichochezi vya magonjwa.
Kupunguza vichochezi vya magonjwa kunasaidia kulinda viungo mbalimbali mwilini pamoja na Moyo dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Inasaidia kuondoa sumu mwilini.

Moja kati ya sababu zinazoweza kusababisha magonjwa ya moyo ni mlundikano wa sumu mwilini.
Sumu hizo ni matokeo ya ulaji mbaya wa vyakula na unywaji holela wa vinywaji na kuchochewa na mtindo mbovu wa maisha.
Virutubisho vya karafuu vinasaidia kupunguza sumu hizo mwilini na kuviweza viungo vya mwili katika hali salama.

Inasaidia kuimarisha kinga ya mwili.

Baadhi ya magonjwa ya kuambukiza yanaweza kuathiri afya ya moyo.
Magonjwa mengi ya kuambukiza ni matokea ya kudhoofika kwa kinga ya mwili.
Virutubisho vya Karafuu vinasaidia kuimarisha kinga ya mwili na kudhibiti magonjwa haya ya kuambukiza.

Inasaidia kuongeza madini ya Potassium mwilini.

Madini ya Potassium mwilini ni muhimu kwa afya ya Moyo kwasababu ni muhimu katika utendaji kazi wa misuli ya Moyo pamoja na mishipa ya fahamu mwilini.
Madini ya Potassium tafiti zimeonesha yanaweza kusaidia kupunguza hatari ya mtu kupata Kiharusi, Shinikizo la Damu na matatizo mengine kwenye mfumo wa damu mwilini.

Vyanzo vingine vizuri vya madini haya ya Potassium ni Ndizi, Machungwa, Spinachi, Viazi na Maparachichi.

Hitimisho:

Karafuu vipande vya maua kutoka kwenye mti wa Mkarafuu.
Licha ya matumizi yake kama kiungo cha chakula, Karafuu ina virutubisho vingi muhimu kwa afya ya binadamu.
Moja ya umuhimu huo ni kuimarisha Afya ya Moyo kwasababu Karafuu:

0
0
1