
Kitunguu saumu tiba asili ya presha ya kupanda
Kitunguu saumu ni jamii ya vitunguu ambavyo hutumika kama kiungo cha chakula, pia kutokana na wingi wa virutubisho vyake muhimu kwa afya ya binadamu kimekuwa kikitumiwa kama tiba ya matatizo kadhaa ya kiafya.
Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa kitunguu saumu ni msaada hasa kwa watu wenye matatizo ya moyo na mfumo wa damu kwa ujumla.
Kula punje 2 za kitunguu saumu kila siku muda wa wiki 8 mpaka 12 tafiti mbalimbali zimeonesha kunasaidia kushusha shinikizo la damu.
Ripoti mbalimbali za utafiti zimethibitisha uwezo wa kitunguu saumu kina uwezo wa kushusha presha kwa mm 6.7 namba ya juu na kwa mm 4.8 namba ya chini.
Allicin ni moja kati ya virutubisho vingi muhimu vinavyopatikana kwenye kitunguu saumu.
Kirutubisho hiki tafiti zimeonesha kuwa kina msaada mkubwa katika kushusha shinikizo la damu kwasababu kiritubisho
cha Allicin kindhibiti uzalisha wa homoni ya angiontensin II.
Angiotensin II ni moja kati ya homoni zinazotumiwa na mwili kudhibiti kiwango cha shinikizo la damu mwilini.
Uzalishwaji wa homoni hiyo husababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu inapotokea presha ya damu imeshuka.
Inapotokea hitilafu mwilini homoni hiyo huzalishwa bila udhibiti na kusababisha shinikizo la damu kupanda kuliko kawaida.
Kirutubisho cha allicin kwenye kitunguu saumu kimeonekana kuwa na uwezo wa kuzibiti uzalishaji wa homoni ya angiotensin II na kusababisha kushusha presha ya damu.
Pia kirutubisho cha allicin kimeonekana kuchochea uzalishaji wa kampaundi za nitric oxide na hydrogen sulfide mwilini ambazo nazo huchangia kwenye udhibiti wa shinikizo la damu mwilini.
Pia uwepo wa virutubisho kama vile viondoa sumu na vidhibiti vichocheo vya magonjwa vina msaada mkubwa wa kudhibiti shinikizo la damu mwilini na kumkinga mtu kupata matatizo ya moyo.
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa watu ambao wapo kwenye matumizi ya dawa za kushusha presha.
Kama unatumia dawa za kushusha presha na ukatumia kitunguu saumu kuna uwezekano presha yako ikashuka sana kuliko kawaida na kuhatarisha afya yako.
Kama upo kwenye matumizi ya dawa au uangalizi wa daktari, na kama una matatizo mengine ya kiafya yanayo ambatana na shinikizo la damu ni muhimu kumuona daktari kwanza kabla ya kuamua kutumia kitunguu saumu.
Tafuna punje 2 za Kitunguu saumu na punje 4 za Karafuu Upate faida hizi kwa afya yako
Mchanganyiko wa kitunguu saumu na asali uliovundikwa una faida gani kwa afya?
Unaweza pia kusoma: