Hyung Nim - Episode 02 
Nilichaguliwa chuo kikuu cha Dar es salaam katika kozi ile ile ambayo niliitaka Accounting.
Mama yangu alifurahi sana na familia yetu nzima kwa ujumla.
“Hatimaye ndoto zako zinatimia mwanangu.”
Mama aliniambia.
“Lakini utaendaje Dar na siyo mwenyeji wa kule itabidi nikupeleke.”
Mama aliniambia.
“Aahah hapana mama kwa bahati nzuri tumechaguliwa na marafiki zangu chuo kimoja Maria, Angel na Lily wote tunaenda
chuo kimoja kwahiyo tutaondoka wote.”
“Aaah, mkiwa nyie wanne wala hata sipatwi na hofu.”
Mama alisema.
“Mtafikia wapi mwanangu.”
“Lily amesema tutafikia kwa mama yake mkubwa wote ametuombea.”
Kwa kuwa familia zetu zilikuwa marafiki haikutia shaka.
Mama akanikabidhi kwa rafiki yangu kipenzi Lily na kisha tukaondoka kuelekea chuoni.
Gibson alikuwa ubungo akitusubiria nilifurahi sana kumuona Gibson.
Tofauti na alivyokuwa akionekana kwenye picha alikuwa ni mzuri zaidi ya picha zake, hakika Gibson alikuwa ni Handsome.
Alikuwa ni mrefu hakuwa mnene wala mwembamba alikuwa na sura nzuri ya kuvutia.
Ngozi yake laini macho mazuri na zaidi ya yote alikuwa na vishimo katika mashavu, alikuwa na dimples.
Nilifurahi sana kumuona nilimkumbatia kwa nguvu.
“Karibu sana Dar.”
Aliongea kwa sauti yake tamu.
Nilihisi kusisimkwa kwa mwili kuwa karibu naye.
Alinipeleka chuoni pamoja na marafiki zangu akatuonesha baadhi ya maeneo ya chuo huku akitusaidia kufanya mambo mbalimbali
yaliyokuwa yakihusiana na usajili nilifurahi sana kuwa karibu yake.
Siwezi kuielezea furaha niliyokuwa nikihisi.
“Gibson you are going to be my man.”
Nilisema.
Nilipangiwa kukaa hostel za chuoni katika ukumbi namba tatu jengo B chumba namba 718.
Kwa Gibson alikuwa mwaka wa pili yeye hakupangiwa chumba hivyo alifanikiwa kununua katika ukumbi namba 3 jengo D chumba namba 1115.
Rafiki yake Jose alikuwa akiishi ukumbi namba 1, Wilson na Albert walikuwa wakikaa ukumbi namba tatu Block A chumba namba 115.
Nilifurahi sana aliponitambulisha kwa marafiki zake niliweza kukutana nao walionesha upendo mkubwa kwangu.
Nilikuwa ni kana kwamba wananisubiria kwa hamu na walikuwa wamefurahi sana kukutana na mimi.
Nilijihisi wa upekee na wa tofauti sana alinionesha mazingira ya chuo alinifundisha vitu vingi.
Moyo wangu ulikuwa na uhakika kwamba nilikuwa nikimpenda Gibson kila mara nilihisi moyo ukienda mbio na mapigo ya moyo
yakiongezeka nilipokuwa karibu naye.
Kila nilipomtazama nilihisi akili ikipaa.
Nilijiona kama malkia kuwa karibu naye.
“Your mine.”
Kila mara nilikuwa nikiwaza.
Siku moja Jose aliniuliza.
“Jenny, Gibson ana wivu sana juu yako.”
Nilicheka.
“Hasa anionee wivu mimi kama nani?”
“Si mpenzi wake.”
Alisema.
“Hamna mimi siyo mpenzi wake mimi ni rafiki yake.”
Nilisema.
Ni kitu ambacho nakijutia siku zote za maisha yangu.
“Acha utani kila mtu anajua wewe ni mpenzi wake, hasa huo urafiki umetoka wapi?”
“hahaha…”
Nilicheka.
“Kama mimi ni mpenzi wake muite muambie aje anitambulishe.”
Niliongea kwa pozi.
“Aaah kwahiyo unataka kuniambia kwamba hamko katika mahusiano si ndio.”
“Yaah.”
Nilijibu.
“Sawa kama umeamua kunidanganya.”
“Hamna siwezi kukudanganya sina sababu ya kukudanganya Jose.”
Nilimuambia.
“Poa basi kama vipi.”
“Sawa.”
Wilson na Albert waliniuliza pia.
“Wanataka nini hawa.”
Niliwaza.
“Potelea mbali.”
Nikawapotezea.
Mara zote nilipokutana faragha na Gib nilimpenda na kumpenda.
Alikuwa so romantic alinipa wakati mzuri sana wa kuwa pamoja naye.
Sikumtamani tena wala kuwa na mpenzi wangu Tonny niliazimia kumuacha Tonny ili kuendelea kuwa na Gibson ingawa
iliniwia vigumu sana kumuambia Tonny.
Mara nyingi Gibson alikuwa akiniuliza huyu ni nani kila alipoona picha ya Tonny.
“Ni rafiki yangu nilimuambia.”
Alicheka tu.
“Hasa kucheka kwake inamaanisha kanielewa au kanidharau.”
Niliwaza.
“Aaah shauri yake.”
Nilijuwa Gibson amevutiwa na mimi kwa kila hali na nilijua Gibson ananipenda sana ingawa sikutaka kuonesha watu kuwa
nampenda sana Gibson ukizingatia tayari walikuwa wanamfahamu Tonny hata wao pia walimpenda Tonny isingekuwa rahisi kwao
kukubaliana na mahusiano yangu mapya niliyotaka kuyaanzisha kati yangu na Gibson.
Lily aliniita.
“Jenny.”
Siku moja.
“Unajua kuwa Gibson anakupenda sana.”
Nilicheka.
“Muache anipende.”
Niliongea.
“Anakupenda sana.”
“Shauri yake.”
“Sawa.”
Aliamua kuishia hapo.
Ni kama kuna vitu alitaka kuniambia lakini aliamua kusitisha kutokana na jinsi nilivyomjibu.
Gibson alianza kunibadilikia.
Hanipigii tena simu kama ilivyokuwa mwanzo, hanitumii meseji hadi nimuanze, wakati mwingine nikimpigia simu ananifokea.
“Gibson kwanini umekuwa hivi?”
“Nimekuwaje?”
“Nimebadilika nimekuwa wa kijani? Eee?.”
“Mbona umekuwa too harsh to me jamani.”
Niliongea kwa sauti ya kubembeleza.
“Aaah, niko kawaida halafu nina mambo mengi usiniletee drama zako za ajabu ajabu.”
“Gibson kwanini umekuwa hivi.”
Niliwaza.
“Whats wrong?”
Nilijiuliza maswali bila majibu.
Kadri siku zilivyozidi kuendelea ndivyo Gibson alivyozidi kubadilika nilikosa amani kabisa nilihisi kupungua uzito.
“Gibson mimi nakupenda kwa nini unanifanyia hivi?”
Niliwaza kwa nafsi yangu.
Hakika Gibson alikuwa amenichanganya kabisa.
Nilishindwa kujiongoza mimi mwenyewe.
Lily aliniita.
“Jenny una nini?”
“Lily nampenda sana Gibson lakini nashangaa kwanini siku hizi anakuwa hivi kwanini ananifokea haoneshi tena kunipenda.”
“Jenny, Gibson anakupenda.”
Lily aliniambia.
“Hapana siyo kweli Gibson hanipendi kama angekuwa ananipenda asingekuwa ananifanyia hivi.”
“Jenny Gibson alishawahi kukwambia kwamba anakupenda.”
Aliniuliza.
Lilikuwa ni swali la ghafla sikutengemea.
“Ndiyo alishawahi kuniambia.”
“Ulimuambiaje?”
“Nilimwambia tu tuwe marafiki.”
“Hamna mtu ambaye anayeweza kuvumilia hivyo, Jenny yani anakupenda halafu umwambie kwamba mtakuwa marafiki,
hapana hamna mtu anayeweza kuvumilia.
Na hiki ndiko kilichotokea kwa Gibson amejitahidi sana kufanya urafiki na wewe lakini yeye anaumia moyoni kwa sababu
anakupenda anachokifanya ni kuwa mkali kwa sababu anajua hawezi tena kuwa na wewe kwahiyo anataka kuwa mbali na wewe.”
“Jamani!!”
Nilishituka sana kwa taarifa hiyo.
“Mungu wangu nifanye nini sasa?”
Nilijiuliza.
“Mimi naenda kumuambia.”
Nilimuita ingawa mara kwa mara alikuwa kila nikimuita alikataa kuja siku hiyo alikuja.
Tulikaa sehemu tulivu tukiongea.
“Eeeh niambie.”
Aliongea.
Mara nyingi tunapokuwa sehemu kama hizo huwa hawi mkali kwangu ananionesha mapenzi yote.
“Nakusikia bibie.”
“Gibson nakupenda.”
Nilimuambia.
“Nakupenda pia.”
Alijibu.
Nilifurahi sana moyoni mwangu kusikia hivyo nilijua hayo yote yameisha.
“Nakupenda sana Jenny.”
Aliniambia huku akinivutia kwake alinikumbatia na kisha ndimi zetu zikakutana.
Ilikuwa ni busu zito na refu ambalo liliniacha na faraja kubwa ndani ya moyo wangu.
“Sasa wewe ni wangu.”
Tuliendelea kubaki hivyo kwa muda mrefu hadi usiku mwingi ulipoingia.
“Ni muda wa kurudi sasa.”
Aliniambia.
“Sawa.”
Nilikuwa na furaha sana wala sikutaka kumficha.
Alinisindikiza hadi karibu na kwangu.
Akanivuta akanikumbatia na kisha akanibusu kwenye paji la uso.
“Uwe na usiku mwema.”
Aliniambia.
Hakika nilifurahi sana.
Niliondoka na kurudi chumbani kwangu nikiwa na furaha, Lily aligundua kwamba nina furaha sana.
“Jenny mbona umefurahi hivyo.”
“Hamna kawaida tu.”
Nilimjibu huku nikichekacheka kwa aibu.
“Sawa bwana kama siku hizi tunafichana.”
Ni kweli hatukuwa na tabia ya kufichana lakini sikuona umuhimu wa kumuambia.
Mara nyingi Lily hakuonesha kuvutiwa na Gibson ni kitu ambacho nilikuwa sikipendi sana.
“Kwanini anamchukia Gibson wangu? Hata afanyeje hawezi kunifanya niache kumpenda Gibson nampenda sana.”
Niliwaza.
Asubuhi ya siku iliyofuata niliamka mapema sana na kumpigia simu Gibson ili kumtakia siku njema, nilipiga simu haikupokelewa.
“Au hajaamka.”
Niliwaza.
“Au ameenda kuoga?”
Nilijiuliza maswali yasiyo na majibu.
“Ngoja nijaribu tena asipopokea nitampigia baadaye.”
“Haloo.”
Ilikuwa ni sauti kavu na ya ukali.
Nilitetemeka.
“Mambo.”
Niliongea kwa sauti ya upole.
“Poa ongea shida yako.”
“Enhee! Gibson una nini?”
“Sina kitu ongea haraka.”
Nilibaki kimya nilishindwa kujua nini cha kuongea.
“Ana nini huyu?! Inamaanisha yale yote tuliyofanya jana hayana maana yoyote, kwanini tena awe hivyo.”
“Kama huongei nakata simu.”
“Noo Gibson subiri.”
Nilikuwa nimeshachelewa simu ilikuwa imeshakatwa.
Nilibaki tu na maumivu moyoni mwangu.
Nilishindwa kuingia darasani siku hiyo.
Lily aliniuliza.
“Una nini?”
“Naumwa.”
Nilimuambia.
“Twende hospitali.”
“Hapana siendi.”
Nilinyong’onyea sana.
Ilipofika jioni hali yangu haikuwa nzuri mara nyingi nilikuwa nikisumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Nilipelekwa hospitali nikalazwa.
“Jenny una nini wewe?”
Lily aliniuliza.
“Sina kitu kuumwa ni kawaida tu.”
Nilimwambia.
“Daktari aliniambia kwamba kutokana na kwamba una vidonda vya tumbo hupaswi kuwa na mawazo.”
“Kwanini una mawazo?”
“Jenny hujui tuko shuleni hapa eee?”
“Hapana Lily ni hali ya kawaida tu shukuru Mungu naendelea vizuri.”
“Aaah.”
Nilivuta pumzi.
“Gibson hajaja kuniona?”
Niliuliza.
“Hajaja.”
“Ulimpa taarifa kwamba naumwa.”
“Ndiyo nilimpa taarifa kabla hutujakufikisha hapa.”
“Alijibu?”
“Alisema tu mpe pole.”
Niliangalia chini kwa huzuni.
“Saa hizi hajapiga simu kuulizia hali yangu.”
“Hajapiga.”
“Ok sawa.”
Moyoni mwangu niliumia sana.
“Kwanini Gibson unanitreat hivi? Nimekufanyia nini lakini au kwa sababu umejua nakupenda.”
Nilikaa hospitalini takribani wiki nzima na kisha nikaruhusiwa kurudi hostel.
Gibson hakuja kuniona hata baada ya kupewa taarifa kuwa nimerudi niliamua kunyamaza kimya na mimi,
siku ya tatu yake nilishindwa nilimtumia ujumbe.
“Mambo.”
“Poa unaendeleaje?”
“Vizuri.”
Alinijibu.
“Naumwa hata kuja kuniona Gibson kwanini unakuwa hivyo?”
“Nilikuwa sijui kuwa umeruhusiwa, halafu nina mambo mengi sana yamenibana.”
Wala hakuhisi kuwa amefanya kosa aliona ni kitu cha kawaida tu.
Niliamua kuyaacha yapite.
“Sawa tu.”
“Kuna siku utajua thamani yangu.”
Nilimuambia.
Mara kwa mara nilikuwa nikimsisitizia nakupenda alijibu tu nakupenda pia.
Rafiki zake walikuwa wakinipenda sana hasa Jose.
Siku moja Jose aliniita chumbani kwake nilienda nilipofika nilimkuta Gib.
Nilikaa kitandani.
Jose aliniambia.
“Jenny natoka mara moja narudi sasa hivi.”
Nilijua alitaka kutupa muda wa kuwa pamoja na kuongea mawili matatu.
Gibson akasema.
“Tunaondoka wote.”
Jose akamuambia.
“Si ubaki na Jenny.”
“Twende bwana si atabaki mwenyewe.”
Wakaondoka.
Nikabaki tu mwenyewe nimekaa.
Pembeni yangu ilikuwepo simu ya Gibson kwa sababu alinifundisha jinsi ya kuifungua niliichukua na
kuifungua nikaanza kuangalia picha sikuamini nilipokuta picha yake na msichana fulani hivi mzuri sana.
Niliumia sana kugundua kwamba Gibson ana msichana mwingine.
Nikaamua kufuatilia ili nijue huyo msichana ni nani, nilikuja kujua kwamba anaitwa Elizabeth na walianza mahusiano yao muda mrefu.
Kumbe wakati wote ulikuwa ukinilaghai tu.
“Potelea mbali.”
Nilirudi chumbani kwangu nikiwa mnyonge sana.
“Gibson kwanini umeniumiza?”
Nilifika chumbani kwangu Lily aligundua kwamba nimebadilika.
“Una nini Jenny?”
“Nothing, naomba tu nilale.”
Alinipisha nikalala.
Ni kweli nilikuwa natembea na maumivu makubwa sana sikuwahi kuhisi kama kuna siku ningekuja kugundua ukweli
wenye kuumiza kama huo.
“Gibson ana msichana mwingine! Na ndiyo maana siku hizi amekuwa mkali kwangu.”
Nilitamani sana kuwa na mahusiano na Gibson lakini nilikuwa nimechelewa.
Marafiki zake hawakuacha kunisumbua, hasa Jose.
“Utamng’ang’aniaje Gibson wakati unajua kuwa ana mpenzi wake?”
“Niache nampenda hivyohivyo.”
Niliwambia.
Jose, Wilson na Albert wote walikuwa wakinitaka lakini kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana Gibson sikutaka kuwa nao.
“Aaah sina jinsi wacha nikubali tu, nitamwomba niwe mwanamke wake wa pembeni.”
Ilikuwa tofauti na matarajio yangu Gibson hakuwa na hisia tena juu yangu.
Niliumia sana katika ukweli huo.
“Sawa kama ameamua kufanya hivi mimi siwezi kumlazimisha acha afanye anachokitaka.”
Nilisema.
Katika urafiki wetu nilikuwa karibu sana na Angel wakati Lily alikuwa karibu sana na Maria tulikuwa tunapenda sana kuchati
kwenye kikundi cha whatsapp na zaidi ya hapo kila mtu alikuwa anachati na mtu yoyote binafsi, nilikuja kugundua jumbe
zisizofaa kati ya Lily na Maria.
Moyo uliniuma siwezi kuelezea.
“Maria ana mahusiano na Gibson!! Lily anajua. Na wakati wote walikuwa wakinitia moyo na amekuwa akinishauri
kwamba Gibson siyo mtu mzuri.”
Najua kuwa Lily anampenda sana Maria kuliko mimi lakini sikutengemea angeruhusu kitendo cha kinyama kama hichi
kifanyike kwangu.
Nililia sana.
Lakini yote nimeyataka mwenyewe.
Najuta sana kitu ambacho nimekifanya kwasababu ni kweli nilimpenda sana Gibson lakini nilijiona kwamba mimi ni wa thamani sana
kuliko hisia zilizokuwa ndani ya moyo wangu, najua nimempoteza Gibson milele hawezi kuwa wangu tena.
Ni mtu ambaye nilikuwa nampenda sana.
Lakini kwa sababu ya dharau nilizokuwa nazo, kwasababu ya jinsi ambavyo nilikuwa nikijichukulia.
Nilijiona mimi ni wa thamani sana.
Lakini sasa hivi nalia na maumivu yangu.
HYUNG NIM (nimekupa jina hili kwa kuwa wewe ni nyota yangu kipenzi kwa kuwa siwezi kukushika ila naweza kukuona tokea
mbali popote niwapo sitaacha kukutazama).
Mwanaume niliyekupenda uende kwa amani.
***** MWISHO *****
Unaweza pia kusoma: