Kuchudi - Sehemu ya Pili (02)
Kuchudi alishituka alijaribu kufinya macho yake ili aweze kuzuia kuona kwenye mwanga ule mkali na hapo ndipo
alipojua kwamba alikuwa akijibizana na maaskari.
Hakufikiria mara mbili aligeuka na kutimua mbio.
Maaskari nao walimfungia tela.
“Huwezi kutujibu sisi hivyo.”
Ikawa ni patashika la kukimbizana.
Kuchudi alikimbia tu alikuwa hajui wapi anaelekea hakujua kama anarudi nyumbani au anaelekea mbali na nyumbani.
Lakini alichokuwa anakijali kwa muda huo ni kukimbia tu kwa maana kama angeshikwa na maaskari
wale basi wasingemuacha salama wangempa kipigo cha mbwa mwizi.
Alikimbia alipofika mbali alionekana kuishiwa pumzi na alianza kuchoka.
Ghafla aliona kibanda kikuukuu aliamini hapo ndipo ambapo angeweza kusalimisha roho yake kwa maana kuendelea kukimbia
kwake ilikuwa ni shida.
Alishachoka na pia wale maaskari hawakuacha kumfukuza.
Aliingia ndani ya kibanda kile.
Alifunika mlango wa kibanda kile na kisha kuchungulia aliona askari wakipita moja kwa moja.
Alianza kuwacheka kwa sauti.
“Wajinga kweli hawa.”
“We ni nani?”
Ghafla alisikia sauti iliyomshitua.
Aligeuka nyuma na kutazama.
Kilikuwa ni kikundi cha vijana wasiopungua sita ambao bila kuambiwa wala kuhitaji maelezo ilionesha
kwamba vijana hao walikuwa ni wavuta bangi.
Kuchudi alishituka sana.
“Wewe ni nani?”
Aliuliza.
“Mimi ni Kuchudi.”
“Wewe ni polisi?”
“Hapana mimi siyo polisi.”
“Unataka nini? Au umejileta mwenyewe?”
“Hapana nilikuwa nawakimbia polisi.”
“Kwahiyo wewe ni nani?”
Wale vijana walinyanyuka wote kwa pamoja na kisha kumuelekea Kuchudi pale alipokuwa amekaa.
Alikuwa anatetemeka.
“Naombeni mnisamehe, bahati mbaya.”
“Kama bati mbaya basi ezekea makuti.”
Kwenye sura ya vijana wale hakukuonekana hata chembe ya msamaha wala chembe ya huruma.
Alichelewa kujua kwamba kama angeendelea kuwaomba wale vijana wamsamehe basi angejikuta katika wakati mgumu.
Alijiona ameokoka kutoka kwenye mikono ya maaskari lakini ameingia kwenye mikono mibaya zaidi.
Hao vijana wasingemuacha salama, wangempora, wangempiga na kumfanyia vitu vingine vyovyote vile viovu.
Alikurupuka na kisha kutoka mbio huku akiendelea na ile ile njia yake aliyokuwa akikimbia mara ya kwanza.
Na hao vijana hawakubaki nyuma.
“Hawa ndiyo mashushu tunaowatafuta tukimshika huyu atakuwa halali yetu.”
Waliongea kwa lafudhi yao inayoonesha utopevu katika madawa ya kulevya.
Kuchudi alikimbia ili asalimishe roho yake.
Alikimbia sana hadi alihisi mapafu yanawaka moto.
Hakujua namna ya kujiokoa tena.
Alipita karibu na makaburi aliona hiyo ni sehemu ambayo angeweza kujificha asionekane.
Aliingia haraka katikati ya makaburi ambapo kulikuwa kuna vichaka vingi na kwenda kujificha.
Alikurupuka na kuingia ndani ya vichaka hivyo.
Hata hivyo alijikuta ameingia katikati ya kundi la watu.
Alibaki ameshangaa watu hao ambao usoni walikuwa wamejipakapaka unga wa rangi nyeupe na nyeusi.
Huku wengine wamejifunga nguo nyeupe hali baadhi yao wamejifunga nguo nyeusi.
Watu hao walikuwa takribani tisa kwa hesabu za haraka haraka.
Walikuwa wamefanya mduara mdogo ambao katikati yao kulikuwa kuna sinia lililojaa mapande ya nyama.
Hakika kuchudi hakuweza kujua watu hawa wanafanya nini usiku huo mnene.
Usiku uliokaribia saa sita.
Alibaki akiwashangaa huku na wale watu wakiwa wamemshangaa.
Mmoja kati ya watu wale ambaye alionekana kuwa ni mwanaume alisimama.
“Oooh nyama imejileta yenyewe tutaitoa kafara.”
Aliongea yule mtu.
Hapo hapo kuchudi alijua kwamba ameingia mikononi mwa wachawi tena wachawi wanaokula nyama za watu.
“Mungu wangu nimeisha.
Mimi mnisamehe.”
Wale watu ni kana kwamba walikuwa hawamsikii.
Walianza kuimba nyimbo ambazo yeye hakuzielewa huku wakimzunguka.
Aliona huu upenyo pekee ni kukimbia tu maana hakuwa na namna.
Unaweza pia kusoma: