Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Formula - Episode 02

Mama Sitti aliendelea kulalamika.
“Lakini mama, hizi kozi nyingine mimi sijazielewa vizuri halafu ukizingatia ukiwa mwalimu wa sayansi mambo mbona ni rahisi tu ajira zao ziko njenje.”
“Hebu acha ujinga wewe ajira njenje wakikulipa hela nyingi sana wanakulipa laki saba aya laki saba hapo hawajakata hela bado mimi hujanitumia hela ya matumizi inabaki shi ngapi? Unataka kuwa masikini, yani mimi sikusomesha mtoto wangu uwe masikini nilikusomesha uje uwe tajiri lakini nashangaa bado una mawazo ya kimasikinimasikini mwanangu hebu chagua kozi nyingine achana na ualimu.”
Mama yake Sitti aliendelea kumuambia.
Hata baba yake aliporudi alizidi kumshauri kuwa asichague kozi ya ualimu kwasababu ualimu haukuwa na soko tena.
“Ualimu bwana hii kozi ni ya ajabu sana kwanza ina watu wengi wanaosoma usizani kwamba huko chuoni utakuwa peke yako kiasi upate ajira kirahisirahisi tu yani siku hizi mambo ni magumu chagua kozi nzuri ualimu achana nao.”
“Lakini baba mimi nilikuwa napendakuwa mwalimu.”
“Hebu acha ujinga wako chagua kozi nyingine.”
Alisema baba yake.

Sitti alienda mtandaoni aliangalia vile vyuo ambavyo alikuwa akivipenda na kuchagua kozi nyingine kabisa.
Na matokeo ya chuo yalipotoka alikuwa amechaguliwa chuo kikuu cha SUA.
Kwa kozi ya sayansi ya Aquaculture.
Mama yake alimsisitiza sana kujitunza.

Hatimaye muda wa kwenda kujiunga na chuo ulifika aliwekwa chini na mama yake.
“Mwanangu sasa hivi vikwanzo vyote ulivyokuwa unakutana navyo vilikuwa sio kitu chuoni ndiyo baba lao, kule utakutana na wakaka mahandsome utakutana na wakaka wanaendesha magari watakudanganya na kila kitu lakini utakapomaliza chuo hautawaona tena, hawatakuoa watatafuta wasichana mabikira wawaoe.
Mwanangu soma.
Kama nilivyokuambia yani siku ya kwanza ya wewe kuanza kuhangaika na vijana iwe ni baada ya kukabidhiwa degree yako, ukishapewa degree yako uko free lakini kama uko chuoni hakikisha hudanganyiki na mkaka yoyote.
Watakuharibia tu maisha yako utadisco utarudi nyumbani na mimi nakuambia ukifanya ujinga wako wowote huko chuoni usije ukarudi hapa nyumbani kwangu. Sijui unanielewa?”

“Ndiyo Mama.”
“Kwahiyo mwanangu mtu yoyote akija chuoni akakuambia oooh Sitti wewe ni mzuri sana sijui nini mwambie najua, najua kuwa mimi ni mzuri kwahiyo wewe fanya mambo yako yani wasije wakakusumbua mwanangu kuwa na msimamo siku hizi bila kuwa na usichana wako hautaolewa unabaki kubung’aa tu hapa nyumbani kututia aibu, nataka usome uwe mfano kwa wengine usijekutuaibisha soma kama unakufa kesho. Sawa mama?.”
Aliongea Mama Sitti.
“Ndiyo Mama.”
Alijibu Sitti.

Safari ya kwenda chuoni iliwadia.
Alifika chuoni na masomo yalianza kama kawaida.
Yale yote ambayo mama yake alikuwa akimhusia aliyaona huko chuoni.
Wakaka mbalimbali walianza kumfukuzia kwaajili ya kuanzisha mahusiano nae.
Kila mara maneno ya mama yake yalimuijia akilini.
“Ukizingua tu huko usije ukarudi hapa nyumbani.”
Na yeye hakutaka kitu kama hicho kitokee.
Wale wote waliojaribu kumsifia aliwajibu kama mama yake alivyomuambia, najua kuwa mimi ni mzuri.
Vijana wengi pale chuoni walikuwa wakijadili na kusema huyu Sitti anajisikia sana.
Hata hivyo hakujali.
Hakutamani hata kuwa na mahusiano.
Wale wote ambao aliokuwa akiwaona wakiwa na mahusiano yao chuoni aliwaona kama watu ambao wamesaliti wazazi wao.
“Hivi wewe Joy wazazi wako wanajua kama huku una mwanaume unamlilia.”
Alikuwa akimuambia mdada ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu sana.
“Achana na mambo ya wazazi wewe.”
“Yani huo ndiyo ujinga ambao siwezi kuufanya maishani mwangu kabisaa, unamlilia mwanaume hata kwenu hawajui.”
Aliendelea kuwaza.
“Unajua nini Sitti, kila kitu huwa kinaenda kwa hatua itafika kipindi mimi nitampeleka Denis nyumbani, sasa unafikiri tunaanza tu mahusiano nampeleka kwetu.”
“Hehehe hongera sana yani hata kama, mimi siwezi kumlilia mwanaume ambaye sijampeleka nyumbani.
Unamlilia for what, hata akiamua kukuacha anakuacha.
Wewe endelea kurukaruka tu.”

“Hivi wewe umeshawahi kuwa na boyfriend?”
“Wa kazi gani?”
“Eeenh unataka kuwa sister.”
“Nataka kuwa brother.”
“Ila Sitti wakaka wengi chuoni wanasema unadharau.”
“Yes hiko ndiyo kitu ambacho nilikuwa nakitaka yani hakuna mtu atakaye niharibia maisha yangu.”
“Sitti mbona ni mtu mzima nani wa kukuharibia maisha yako sahivi.Yani wewe usome umalize upate degree yako nani wa kukuharibia maisha.
Kukuharibia maisha anakuchania madaftari au anafanyaje au anapunguza coursework yako ama anakuchania assignment eeenh? Acha ujinga Sitti.”

“Siyo kwamba tuna date kwasababu sisi sijui hatuna akili sijui nini kila kitu kinaenda kwa process, ukitaka kuja kuolewa baadae lazima uanze kudate halafu mnaenda stage by stage.”
Aliendelea Joy.
“Na hiyo stage ya kumlilia mwanaume ni ya ngapi?”
Sitti alijibu.
Joy aliamua kumpuuzia.
“Yani mnafanya mambo ya ajabu sana mimi sitahangaika na mkaka yoyote nitamaliza zangu chuo nipate degree yangu ndiyo nitapata mwanaume wa kuja kunioa sasa.”
“Aya bikra Maria.”
Joy alimjibu.
“Hahahaa… Ita vyovyote unavyojisikia mwaya.”

Maisha ya chuo yaliendelea.
Sitti hakutaka hata kujiingiza kwenye mahusiano, alikuwa na marafiki zake wachache wa kike tena wala hakutaka urafiki na boys kuhofia kuingizwa majaribuni.
Miaka mitatu si mingi hatimaye alimaliza chuo.
Wazazi wake walifurahi sana.
Alifaulu vizuri mno.
Alipata degree yake na kisha kurudi nyumbani.
Mama Sitti asivyokuwa na dogo mtaa mzima ulijua kuwa mwanae amemaliza chuo.
Miaka ilizidi kusogea hatimaye Sitti alifikisha miaka ishirini na sita.
Tangu amalize chuo alikuwa ni mtu wa kuhangaika huku na huko kutafuta kazi.
Hata hivyo kazi zilimuia vigumu kupata.
“Sitti…”
Siku moja mama yake alimuita.
“Hebu wakati basi unahangaika kupata ajira tuletee basi hata mchumba wako.”
“Mchumba gani?”
Sitti alimuuliza.
“Inamaanisha wewe una miaka ishirini na sita huna mchumba kabisaa.” “Sina.”
“Kwahiyo huko chuoni ulikuwa umeandaa kufanya nini, wenzako wametoka chuoni wameolewa wewe bado upoupo tu.”
Sitti alikunja sura kana kwamba alikuwa amuelewi mama yake alichokuwa anakiongea.
“Mama wewe si ulikuwa unasema nikienda chuoni nisome nisirukeruke.”
“Mtoto mjinga huyu yani wewe.
Heheheeeee…
Eee mungu wangu bora ningejifungua maandazi nikagawana na manesi pale hospitali tukala tukashiba.
Kwahiyo umeenda huko umekaaa…
Jamani naomba tu niishie hapa nisiseme sana nikaonekana nataka kusema.
Eeenh yani limtu limezubaa aya sasa utafute mume uolewe.”

Mama yake alikuwa akiongea huku akipiga makofi.
Sitti alinyanyuka na kuelekea chumbani.
“Huyu Mama ni anakuwaje jamani?! Eeenh! Heee hii shughuli yakumtafuta mume hiiii…”

Mara alimkumbuka Baraka ni mmoja kati ya wakaka ambao walikuwa wanamtaka tangu wakati wako chuoni.
Lakini ni mkaka pekee ambaye mpaka wakati huo alikuwa bado akimsumbua.
“Huyu tangu first year alikuwa yuko na mimi tangu first year alikuwa ananitaka na mpaka leo bado ananiambiaga kuwa ananitaka.
Itakuwa ananipenda kweli. Ngoja nimkubali.”

Alimpigia simu.
“Hello.” “Hello Sitti.”
Alijibu Baraka.
“Uko wapi?”
“Niko tu nyumbani.”
“Za siku?”
“Nzuri.”
“Nilikumisi sana.”
“Hata mimi nimekumis pia Sitti.”
“Ok nilikuwa nataka nikusalimie tu.”
“Mmmh ni muda mrefu sana hujanichek leo imetokea kama bahati vile.”
“Aaanh nimekukumbuka.”
Aliongea Sitti huku akichekacheka ovyoovyo.
“Nashukuru kunikumbuka.”
Aliongea na kukata simu.
Alipokata simu alimtext.
“Nimefurahi kusikia sauti yako.”
“Leo umekula nini vile Sitti maana siyo kwa kunifurahia huko wakati nakumbukaga zamani ulikuwa ukinifokea kweli.”
“Hivi Baraka kwanini siku zote wakati nilikuwa nikikufokea ulikuwa haukati tamaa kila siku ulikuwa ukinikumbusha.
Hata nikiacha kukutext wewe huwa unanitext kama kawaida.
Kwanini?”

“Kwasababu nakupenda Sitti. Yani siyo siri mimi nakupenda sana lakini sijui kwanini hautaki kunielewa.”
“Mimi nakuelewa.”
“Kivipi?”
“Aaanh sema tu nilikuwa nataka nijue kama unanipenda kweli au vipi.” “Mimi nakupenda.” Baraka alijibu.
“Lets date....Nimekubali.”
Alisema Sitti.
“Are you serious au unatania”
Baraka alijibu.
“Am serious.”
“Woow siamini macho yangu.”
“Amini Baraka hata mimi nilikuwa nakupenda lakini nilikuwa tu nataka nijue kama kweli unanipenda.”
“Wooow so kati ya wale wote waliokuwa wakikufukuzia chuoni mimi ndiyo nimepata bahati.”
“Yes kwasababu ni muaminifu sana.” “Ahsante sana Sitti. Nakupenda pia.” Na mahusiano kati ya Sitti na Baraka yalianzia hapo.
Mapenzi yao yalikuwa moto moto.
Hadi kufikia wakati Sitti akamuambia Mama yake.

“Mama sio muda mrefu nitamleta mchumba wangu nyumbani.” “Hayo ndiyo maneno sasa.” Mama yake alifurahia.
“Lini utakuja kunitembelea.” Baraka alimuuliza Sitti.
“Mmmh anyday utakaposema.”
“Sawa, hamna shida.” “Halafu pia nilimuambia mama kuhusu swala la wewe kuja nyumbani amefurahi sana.”
“Woow na mimi nitafurahi sana kumuona.”
Sitti alijipanga vilivyo kwenda kumtembelea Baraka ambaye alikuwa akiishi mkoa mwingine.
“Mama mi nataka kusafiri.”
“Unaenda wapi?”
“Naenda kumuona mchumba wangu.”
Alisema Sitti.
“Eeenhe wapi huko anapokaa?”
Anaishi Dodoma.
“Oooh aya msalimie sana mkwe lini sasa mtakuja.”
“Nikitoka uko nikirudi nitamleta nyumbani.”
“Sawa msalimie sana ila uwe makini sana.”
Mama yake na Sitti aliongea.
Sitti alijipara vilivyo, alijikoki, akajiandaa na kisha kuelekea Dodoma kwaajili ya kumuona mpenzi wake Baraka alipokelewa vizuri na kisha kupelekwa hotelini.
“Why hotel?!”
“Aaanh unajua nyumbani bado sijajiandaa vizuri umenishitukiza.”
“Lakini mbona tulishapanga kuhusu hii safari muda mrefu sana.”
“Aanh usijali tutaenda. As for now kaa hapo hotelini tufurahie maisha.”

Hiyo siku ilikuwa ni siku ya kwanza kwa Sitti kukutana kimwili na mwanaume.
Alisikia maumivu makali sana.
“Kumbe inauma hivi.”
Alimuambia Baraka.
“Ooh siamini kama nimekukuta na usichana wako.”
Sitti alitabasamu.
“Kwakweli ulikuwa na haki ya kuringa, sasa nimeelewa kwanini ulikuwa unaringa ukiwa chuoni.”
“Thank you.”
Alijibu Sitti.
“I promise to love you siyo siri ni heshima sana ambayo umenipa. Aaah but kwanini umeamua kunipa mimi leo.”
Baraka aliuliza.
Sitti alijichekesha ovyoovyo huku akizungusha macho yake.
“Kwasababu i trust you and kwasabau pia wewe ni mwanaume ambaye nategemea kuanzisha nae familia.”
Alisema Sitti.
“Woow… that is awesome.”
Alisema.
Alikaa Dodoma wiki nzima akiwa hapohapo hotelini.
Walifanya mapenzi kadri ya uwezo wao tena bila kinga.
“Condom hazina utamu, mi binafsi sifeel chochote yaani.” Tangu kusikia maumivu mpka kuanza kusikia vizuri.
Sitti alifurahia, alimfurahia sana Baraka.
Hata wiki moja ilipoisha alitamani asirudi nyumbani kwao.
Lakini hakuwa na namna ilibidi arudi.
Alimfungashia mama yake zawadi nyingi.
Mama yake alifurahi sana kupokea zawadi zote zile kutoka kwa mwanae.
“Nimefurahi sana jamani.”
“Aya mwenzako anasema atakuja lini?”
“Atakuja muda wowote hivi karibuni kwahiyo tujiandae.”

Siku zilizidi kwenda huku mahusiano kati ya Sitti na baraka yakizidi kuimarika.
Kila mara mama yake na Sitti alikuwa akimsisitiza kuhusu kumleta Baraka nyumbani.
Mara zote ambazo alikuwa akimuambia Baraka kuhusu kwenda nyumbani alikuwa akimuambia subiri naweka mipango sawa.
Lakini Sitti aliendelea kumkumbusha Baraka kila siku kiasi kwamba ilionekana kama ni kumkera.
“Lakini Sitti kwani shida ni nini si nitakuja wakati ukifika mbona kama unanifosi.”
Alijibu.

Sehemu 1 Sehemu 3
0
0