Formula - Episode 03 
“Hapana siyo hivyo ila mama yangu ndiyo anasema uje nyumbani.”
“Kwani namuoa nani wewe au mama yako.”
“Noo that’s no it, lakini sasa ni vizuri kama tumeanza mahusiano uje nyumbani.”
“Nimesema nitakuja shida ni nini? Yani mnanifosi utasema nimekula hela zenu eeenh…”
Aliongea maneno mengi ambayo yalionekana kumkwaza Sitti.
Sitti alikasirika.
“OK kama unaona hiko ni sawa, sawa. Kama unaona kama mimi nakufosi kuja nyumbani kwetu ok acha sitakukumbusha tena.”
Alisema Sitti.
“Aisee itakuwa afadhali kila nikipokea simu yako lini unakuja nyumbani, meseji zako lini unakuja nyumbani, aanh nimechoka bwana.”
Alisema Baraka.
“Sawa hutakaa unione nakukumbusha tena.”
Alisema Sitti na kukata simu.
Alibaki ametulia tu.
“Yani huyu nitamnunia wiki nzima mpaka atanimisi mwenyewe atanitafuta.”
Alisema Sitti.
Aliendelea kukaa na kusubiri.
Mama Sitti tayari alikuwa ameshawaambia marafiki zake wote kuwa mchumba wa mwanae atakuja nyumbani hivi karibuni kwaajili ya kutoa mahari na
kujitambulisha kwaajili ya ndoa.
Aliwaambia kuwa tayari tumeshapanga tarehe ya harusi kwahiyo aliwaambia wakina mama wakatafute sare ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameshaipendekeza.
Wiki ilipita.
“Wewe hivi hiyo nitakuja, nitakuja mpaka lini, ujue mimi nimeshawambia watu kuwa atakuja.”
“Mama usijali amesema atakuja.”
Alisema Sitti huku akichekacheka.
“Jamani mimi nimechoka kusubiri jamani, naomba sana mfanye mapema mje.”
Alisema mama yake na Sitti.
“Tena nataka nipange bajeti ya mahitaji ya kinachohitajika tuandae mapema sio siku imefika wageni wamekuja hapa tunabaki tunahaibika.”
Sitti alinyanyuka tu huku akitabasamu na kumuacha Mama yake.
Sitti alinyanyuka na kisha kuelekea chumbani.
Hata hivyo alikumbuka kwamba kesho yake ana interview kwahiyo aliamua kumtafuta Baraka mara baada ya interview ile.
Asubuh na mapema aliamka.
Alijiandaa vizuri na kisha kumuaga Mama yake.
“Nakuombea kila lakheri mwanangu.”
Sitti alinyanyuka na kisha kuelekea kwenye interview.
Alifanya interview yake vizuri sana hata waliokuwepo pale walimsifia.
“Tutawapigia simu baadae wale wote ambao mmechaguliwa."
Sitti aliondoka wala hakufika mbali simu yake ikaita.
“Hello natumai bado hujaondoka kabla hujaondoka naomba tuonane.”
Simu ilisikika.
Sitti alipewa maelezo ya ofisi ya kukutania akaenda.
Alipofika alikutana na mmoja wa waliokuwa wakimhoji.
“Sikia Sitti Mara nyingi kampuni zinapofanya interview tayari zinakuwaga na watu wao yani interview ni kama geresha tu.
Ila Mimi nimeona unaweza na unahitaji sana hii kazi nataka kukusaidia sijui kama na wewe upo tayari kunisaidia.”
“Nitakupa chochote kile naomba nisaidie.”
Aliongea Sitti kwa mashaka.
“Good girl.”
Alisema yule mwanaume na kisha kusogea mlangoni na kuufunga Sitti hakuwa ametambua bado lengo la yule mbaba.
Hata hivyo alikuwa amechoshwa na kukaa nyumbani muda wote aliamua liwalo na liwe.
Mwanaume yule alimsogelea na kuanza kumshika shika mwili wake.
Sitti alionekana kuogopa.
Alitamani kupiga kelele na kujinasua lakini alipewa vitisho vilivyomfanya akae kimya na kuruhusu kuingiliwa hadi mwanaume yule aliporidhia.
“Asante nenda nyumbani we will surely call you later.”
Aliaga na kisha kurudi nyumbani kwao akiwa na furaha kwa ajili ya kuahidiwa kupata kazi hata mama yake alimuona.
“Eeenhe nini tena mbona una furahi.”
“Nimemaliza interview yangu salama namshukuru Mungu kila kitu kimeenda vizuri yani nina uhakika kupata hii kazi kwasababu nimeweza kujibu maswali
vizuri yani nimejibu vizuri mpaka interviewer wamenipenda.”
Mama yake alicheka.
“Eeenh Mungu anipe nini mimi jamani.”
“Yani mwanangu huyo anapata kazi mmmh, aya mchumba wake anakuja kumtolea posa anaolewa eeenh aisee Mungu amenibariki sana.”
Jioni ya siku hiyo ilimkuta siti akiwa kwao akifanya shughuli mbalimbali za nyumbani ingawa alikua akihisi kizunguzungu.
“Mmmh…”
Simu yake haikubanduka pembeni yake.
“Mbona sipigiwi simu mpaka saa hizi. Halafu sina hata bando ngoja nikaweke bando.”
Alitoka na kisha kuelekea dukani.
Alipofika dukani alinunua vocha na kisha kurejea nyumbani kwao.
“Sittii… Sittiii…”
Alisikia akiitwa aligeuka nyuma na kuangalia.
Alishangaa sana.
“Nani huyu anayeniita mbona mimi simfahamu.”
“We Sittii…”
Aliitwa tena.
Aligeuka.
Aliona mdada akiwa anashuka kwenye gari huku akimkimbilia.
Ilikuwa ni gari ndogo tu.
“Mambo Sitti.”
“Powa mzima.”
Aliitikia huku akikunja sura yake kumaanisha kwamba hakuwa amemtambua.
“Mzima tu sijui wewe. Hujanifahamu.?”
Alisema.
“Mimi ni Lucy umenisahau nilikuwa nakaa hapo kwa mama Sakina.”
“Aaanha Lucy mambo.”
“Powa.”
Lucy alimkumbatia.
Sio siri alionekana alikuwa anajiweza.
“Eenhe niambie za siku.”
“Safi tu.”
“Ulishamaliza chuo.”
“Muda mrefu sana vipi wewe uko wapi?”
“Mie hata sikai huku siku hizi nimeshahama baada ya kuolewa nakaa sehemu nyingine kwahiyo nilikuwa tu nimekuja kusalimia sema mama yako namuogopa
yule nikashindwa kuja kwenu nashukuru nimekuona.”
“Hongera…Hongera sana jamani.”
“Nimefurahi sana kukuona jamani. Chukua namba zangu za simu tutawasiliana.”
“Mtoto?”
“Niko nae nakaa nae anaendelea vizuri tu nina mtoto mwingine tena nae ni mkubwa tu.”
“Aanh hongera sana.”
“Ahsante… Mwanangu yuko darasa la pili saa hizi.”
“Hongera mwaya.”
Alisema Sitti.
Huku akichukua namba ya simu ya Lucy na kisha kuondoka.
“Mmmh mbona makubwa. Lucy ana maisha yake anaonekana anaishi vizuri.”
Mawazo yalimvaa.
Alitembea mpaka alifika kwao.
“Mama hukusikia kitu chochote kuhusiana na Lucy?”
“Yule binti kahaba mimi nisikilize habari zake za kazi gani? Sijui hata alitorekea wapi na mwanae hata sikusikia.”
“Nimekutana nae.”
“Eenhe kachoka eeenh, heheeee…
Nilijua tu utamkuta na mwanae kapaukaaaa amemvalisha sijui nguo gani.”
“Hapana Mama.”
“Hapana nini? Mtu alichezea maisha yake hivi unaweza jifananisha na yeye kweli umesoma una elimu eenhe… Mwanangu yani nashukuru Mungu sana
kwasababu yako haukuchezacheza.”
“Mama nimekutana na Lucy ana maisha mazuri anatembelea gari na ameolewa.”
“Unamaanisha nini?”
“Ndiyo nimekutana nae amenipa na namba yake ya simu yani ni ana maisha mazuri sio kwamba anaishi maisha ya ajabuajabu hapana.”
“Utakuwa umemfananisha.”
“Siyo nimemfananisha yani mimi nilikuwanapita kwenye kichochoro kaniita akaniambia mimi ni Lucy.”
“Hebu nitolee ujinga kaendelee na kazi zako huko, Lucy… Lucy...”
Mama yake na Sitti ni kama alitaka kuongeza neno lakini alishindwa baada ya kuona Sitti akikimbilia bafuni.
Baada ya kutoka bafuni aliingia ndani na kupitiliza moja kwa moja chumbani.
Aliwaza na kuwazua.
Alikumbuka simu yake aliivuta na kuingalia lakini hakukuta missed call wala meseji.
Aliamua kuunga bando ambalo lilimuwezesha kupata dakika, sms pamoja na MB.
Aliingia mtandaoni.
“Eenh sasa nifanyeje ila niendelee kusubiri.”
Mwishowe aliingia kwenye mtandao.
Aliona text nyingi sana zikiingia katika group lao la chuo.
Aliamua kwenda kuangalia ni nini kilichokuwa kikijadiliwa humo ndani.
La haula! Moyo ulimpasuka.
Picha za Baraka akiwa amependeza akiwa amevaa suti nyeusi huku pembeni yake akiwa amekaa msichana mwingine ambaye amevaa shela.
Ilionekana ni wazi kwamba Baraka ameoa.
“Mungu wangu Baraka!”
Alinyanyua simu yake huku mikono ikitetemeka na machozi yakimtoka.
“Ooh my God!”
Alipiga simu ya Baraka mara kadhaa lakini haikupokelewa.
“Ndiyo kusema yuko harusini.”
Machozi yalimchuruzika mfululizo.
Hakuamini kile ambacho kilikuwa kikitokea.
“Baraka Barakaaa…”
Aliita jina la Baraka kana kwamba yuko karibu nae.
“Ooh my god siamini mimi. Nimekosea wapi! Mbona ndie mwanaume wangu wa kwanza anawezaje kuniacha na ndo kanitoa usichana?? Sasa nani atanioa.”
Aliwaza.
Mara simu yake iliita.
Alifuta machozi na kisha kuipokea huku akijitahidi kukaza sauti yake.
“Halooo…”
“Haloo…”
“Bila shaka naongea na Sitti.”
“Eeee ni mimi.”
“Ok Sitti ahsante kwa ajili ya interview yako nzuri lakini tunasikitika kukuambia kwamba hatutaweza kukuajiri kwahiyo tunakutakia kila lakheri
katika kutafuta kwako kazi.”
Sitti alishindwa kujibu machozi yaliendelea kumchuruzika mfululizo.
Sitti ilikwama kila akitamani kuongea neno lilikuwa halitoki.
Simu ilianguka.
Ilidondokea kitandani huku yule aliyekuwa upande wa pili akiendelea kumuita Sitti lakini hakusikia lolote.
Aliichukua simu yake na kupiga namba za mwanaume yule ambaye hata jina lake hakuwa akilitambua.
Simu haikupatikana alijaribu tena na tena lakini majibu yakawa yaleyale.
Alihisi kuwehuka.
Ndani ya siku moja alikuwa amepata mapigo kadhaa yaliyomrudisha chini, alichanganyikiwa si kidogo.
Mama yake aliingia na kumkuta Sitti katika hali ya mshangao.
“Unalia nini?!”
Sitti aliangua kilio cha nguvu sasa.
Mama yake alienda kumkumbatia.
“Nini unacholia.”
“Niache mama wewe ndiyo uliyeniponza mnafiki mkubwa wewe.”
Sitti alianza kuongea.
“Ni nini kwani nimekuponza?! Nini Sitti?!”
“Umenijaza ujinga tuu sina lolote sahivi nazeekea tu nyumbani nimepoteza kila kitu.”
“Unasemaje mpumbavu wewe!”
Mama yake aliongea kwa sauti.
“Nini sasa Baraka mwenyewe ameoa, kazi nimekosa hadi Lucy amenipita maisha mimi niko na li degree langu la makaratasi nimeyakumbutia
sina mbele sina nyuma mpaka leo bado nakaa nyumbani nyie ndiyo mlionishawishi nisome hii kozi mpaka sasa sijapata ajira naa...”
Aliendelea kufoka Sitti huku akilia kwa nguvu mpaka mishipa ya shingoni ikaonekana na Mama yake alikaa kimya.
Baba Sitti aliingia mule ndani.
“Kuna nini?”
Si Mama Sitti wala Sitti ambaye alikuwa akiongea.
Mama Sitti alikuwa amejiinamia kimya huku Sitti akiendelea kulia kwa sauti.
“Najuta kuwasikiliza ni bora hata ningeishi maisha yangu tu.
Yani bora hata hata ningechezacheza na wanaume huko nikakosa hata hii degree lakini
ningekuwa nimefaidi maisha. Ona sasa nazeekea nyumbani sijaolewa sijapata kitu chochote sijapata maisha yoyote mpaka leo hela za matumizi napewa na
nyie hata kunipa hela ndiyo basi.
Siyo siri nimechezea sana maisha yangu.
Sijui yani sijui tu kwanini, sielewi, sijui nilikokosea, mmeniponza yani mpaka najiona sifai.”
“Kwani kuna nini kimetokea.”
“Hebu niache huko tokeni sitaki hata kuwaona.”
Aliendelea kulia Sitti.
Mama Sitti alinyanyuka kwa aibu akamshika mkono mume wake na kisha wakatoka.
Unaweza pia kusoma: