Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Formula - Episode 04

Alipofika chumbani alimsimulia yote ambayo alikuwa ameyasema.
Baba Sitti aliguna.
“Sasa tutafanyeje?”
“Mmmh hata sielewi.”
“Lakini hii yote ni mipango tu ya Mungu hamna kuwahi wala kuchelewa asikate tama atapata mwanaume atamuoa na kazi atapata.
Nakumbuka vile ambavyo tulikuwa tukimtisha mtoto wetu sio siri hata sisi kama wazazi tulikosea.
Tungemuacha achague mbali na kumpa ashauri halafu maisha mengine yangebakia yakwake.
Bora angechagua kitu ambacho anakipenda yeye hata kama angekosa ajira bado angekuwa na tumaini lakini sisi tulimuaminisha kabisaa kwamba akisoma hii kozi atapata ajira.”

“Kilichotokea hata mimi nasikia aibu huko mtaani nitawaambia nini watu, miaka sasa inaenda miaka inarudi amemaliza chuo na bado yuko hapa nyumbani. Siyo siri nimeumia sana mimi kama mzazi.”

Usiku huo ulipita kila mtu akiwaza lake.
Kwa upande wa Sitti hali haikuwa nzuri alilia mpaka alipopitiwa na usingizi.
Asubuhi alimka hakutaka hata kuongea na mtu.
Baba yake alipoondoka kwenda kazini alibaki na mama yake bila kusemeshana.
Wakati akiwa anaosha vyombo alihisi kichefuchefu kikali.
“Hiki ni nini nacho.”
Aliwaza huku akinyanyuka na kukimbilia pembeni kutapika.
“Ni malaria au nini?”
Akiendelea kuwaza huku akirudi kuendelea kuosha vyombo.
Alipomaliza alibeba beseni lililokuwa na vyombo na kuliingiza ndani.
Alipofika mlangoni alimkuta mama yake akiwa ameketi hapo mlangoni.
Michirizi ya machozi iliupamba uso wa mama yake na Sitti.
Ndipo Sitti alipogundua kuwa mama yake amekuepo hapo kwa muda mrefu akimtazama huku machozi yakimtoka.
Ubaridi ulimtambaa kuona mama yake akilia kwa huzuni.
“Unalia nini mama?”
Sitti aliuliza.
Mama Sitti alikunjua upande wa kitenge aliyojifunga na kufuta machozi uso wake sasa ulionesha vile alivyokuwa akiumia moyoni.
“Katika maisha haya tunakosea sana kuamini kuwa sisi ndo wapangaji wa mambo wakati kuna aliyejuu yetu.
Swala la wewe kukosa ajira au mchumba wako kuoa lipo nje ya uwezo wetu sisi tumekutunza tukakufundisha kila ambalo ni jema na tukakuonya lakini...”

Machozi mfululizo yalimtoka mama yake na Sitti kiasi cha huzuni kumkaba hadi akashindwa kuongea.
Alilia mfululizo.
Sitti alikuwa ameshikilia beseni lake la vyombo hali akimtazama mama yake kwa kuchanganyikiwa asielewe alichokuwa akikizungumza.
“Sitti na ujuzi na uzoefu wangu wote ni wazi una mimba na Mimi ni...”
Mama Sitti alikatisha alichokuwa akikizungumza baada ya Sitti kuachia lile beseni lenye vyombo huku kukifuatiwa na kelele kali ya vyombo kugongana na vingine kupasuka.
Sitti alilishika tumbo lake asiamini alichokisikia.
"No, haiwezi kuwa kweli. Nimefanya mara chache vile.”
Aliropoka sitti.
Hapana shaka alichanganyikiwa sana.
Alimruka mama yake na kukimbilia chumbani kwake kisha kuurudishia mlango alizunguka humo chumbani akiwa haelewi cha kufanya.
Sio siri alihaha.
Alishika hiki na kile akaacha hiki akagusa hiki mwishowe alikaa kitandani.
Akachukua simu na kupiga namba fulani.
Japo simu haikupokelewa lakini aliendelea kupiga mara kadhaa huku akilia kwa sauti iliyoelekea kuzidi wakati wowote.
Simu ile ilipokelewa.
“Halloo.”
“Baraka ni nini hiki umenifanyia???!”
Sitti alibwata.
“Hakuna kitu kibaya nimefanya au ni nini nimekufanyia?”
Alijibu baraka kwa kebehi.
“Kwanini ulinidanganya??”
“Mi sijakudanganya Sitti wala sijawahi, uliniuliza sababu ya kutoacha kukusumbua nikakuambia kwasababu nakupenda, unanipa ofa niuchezee mwili wako.
I was just flirting with you hii ni kawaida yetu wanaume ukanitunuku.
Unluckily tayari nilikua na mchumba wangu nisingeweza kumuacha kwa ajili yako.
Tatizo lako you had a wrong idea about love, sex haimaanishi mapenzi wala upendo, yaani haujui tofauti ya sex na love.
After all sikujua kama upo serious na mie.
Mimi mpaka uliponiambia kuhusu kupelekana kwa wazazi nilikuwa nashangaa yaani unikatae siku zote halafu ghafla unikubali na ukubali kuja kunitembelea na kunipa mwili wako.
Mi nilijua ni one night stand and i had no idea if you were virgin.
I am sorry asee najua ulijitunza sana sema hukuwa na hakika ni nani unayemtunzia I’m really sorry thou you were so sweety but I can’t be withy...”

“Nina mimba yako Baraka.”
“Nini???!”
“Ndio hivyo na...”
“To cut it short abort tu usifikiri niko tayari kuleta migogoro kwenye ndoa yangu changa, yaani wewe ni mshamba sana, ulidhani kunitegeshea mimba ndo utanipata?? Hangaika na mimba yako mi hainihusu na nikikata hii simu......”
Tayari Sitti alishakuwa amekata simu akairusha kitandani na kuangua kilio cha nguvu.
Mama yake aliingia na kumkumbatia mwanae.
Waliunga na kulia wote huku mama Sitti akimfariji mwanaye huyu kitindamimba wake.

“Maisha hayana formula eti kwamba ukifanya hiki basi maisha yako yatakuwa bora au usipofanya basi itakuwa umeharibu maisha yako, hujui yatakayozaliwa na siku moja.
Kila mtu ana namna yake ya kufanikiwa na kwa wakati wake.
Usikate tamaa baada ya kile ulichokitegemea kukuangusha.
Maisha hayakuhitaji wewe uwe legelege simama na uanze upya ukifeli hapa jaribu pale.
Ila usiache kujaribu maisha hayana formula kwahiyo ishi uwezavyo ila hakikisha una furaha na amani na unalinda afya yako.”

Ni mwaka huu Sitti amefikisha umri wa miaka thelathini na moja.
Bado yupo kwa wazazi wake anajishughulisha na biashara ya duka la vipodozi ambalo linafanya biashara ya uwakala pia na vinywaji laini.
Baraka alikubali kumhudumia mwanaye Geovin baada ya muda mrefu kupita na hakika Geovin alikuwa akilandana na baba yake.
Ni mwaka huu ndio ambao Sitti anatarajia kuolewa na mwanaume aliyekutana nae katika harakati za kimaisha.
Anampenda Sitti na mwanaye Geovin.

***** MWISHO *****

Sehemu 3
0
0