Real Love - Episode 04 
Aliongea Charles kwa hisia.
Hakuna aliyeongea kimya kilitawala.
Happy aliinua mkono wake kuashiria Charles asogee karibu.
Charles alitii.
Happy alimkumbatia kwa nguvu sana.
Mama Happy machozi yalimbubujika alinyanyuka na kuelekea chumbani kwake na kisha kuruhusu machozi yamtoke tani yake.
Pamoja na hayo bado Happy alimsisitiza Charles kuwa waachane japokuwa Charles hakutaka kubadili msimamo wake.
Mpaka Charles anaondoka Changanyikeni bado hakukuwa na suluhu kati yao.
“Umechelewa sana baba ulipitia Wap?”
Aliuliza mama Charles maara baada ya kumuona mwanaye huyo akiingia ndani Charles alipitia sebuleni hapo na kwenda kukaa kwenye moja kati ya
masofa mazuri yasiyomchosha mkaaji huku akitabasamu.
Kila mtu alikuwa na amani kumuona yule Charles waliyemzoea kabla ya miezi miwili nyuma.
Furaha yao iligubikwa na woga kuhofia Charles anaweza kurudi kama alivyokuwa hapo awali.
Walijitahidi kwa kila namna kumpa furaha.
“Kuna sehemu nilipitia mama.”
Alisema Charles baada ya kuwa amesalimiana na watu wote hapo.
“Eeer Charles tunaomba umlete mkwe wetu tumuone.”
Baba Charles aliongea.
Charles alishindwa kung’amua kama ni utani au mzee wake huyo alikuwa akimaanisha.
Maneno hayo yaliendelea kurindima kichwani kwake hata baada ya kuondoka sebuleni hapo.
“Najua mzee wangu huwa hanaga utani usikute wamejadili kama familia wameona nifanye hivi...duuh...but wataelewa kweli?? em tutaona.”
Charles aliwaza na kuwazua.
Aliamua kuongea na mama yake Happy juu ya mpango wa familia yao kumtambulisha Happy.
Mama Happy alipinga hilo swala.
“Hakuna kitu ambacho sitafurahia kukuona kama mwanangu kusemwa wala kudhihakiwa na mtu yeyote yani sitamvumilia kabisa.”
“Mama familia inayajua haya yote na imekubali Happy aende na pia kwanini unamkosea mwanao kupata ajali haimaanishi Happy afungiwe tu ndani,
haimaanishi kwamba maisha yake yameishia hapo, haimaanishi watu hawamtaki tena As long as I’m living Happy ataishi vizuri kabisa.”
Maneno haya yalionekana kumuingia sana mama Happy ambaye tangu mwanaye apatwe na haya matatizo amekuwa mtu wa kukosa amani na furaha wakati wote.
Mara nyingi machozi humtoka na kukumbuka mambo yote mabaya yaliyowahi kumpata.
Charles alipanga siku ambayo ni mwisho wa wiki kwa ajili ya kumpeleka Happy nyumbani kwao.
Aliwaambia wazazi wake kuwa atakuja na zawadi kwahiyo wajiandae kuipokea.
Alimfuata Happy kwao na kumuahidi mama yake kumrejesha salama.
Happy alikua akitabasamu tu huku akiona kwa jicho moja.
Njia nzima palitawaliwa na ukimya mpaka walipowasili Mikocheni.
Waliposhuka kwenye gari Charles alimsaidia Happy kutembea kutokana na miguu yake kutokuwa sawa.
Happy alikuwa amejifunika ushungi uliozuia uso wake kuonekana vizuri.
Walitembea mpaka mlangoni.
“Uko nyumbani feel free.”
Alisema Charles huku akisogeza mtandio wake na kufanya sura ya Happy ionekane vizuri.
Alifungua mlango na kumsaidia Happy kuingia ndani.
Hatua chache mbele walikuwa wamewasili sebuleni lakini mtafaruku uliotokea uliwafanya wasimame kwanza.
Careen aliyekuwa amekaa kwenye sofa la peke yake wakati huo aliweza kuruka na kwenda kusimama nyuma ya wazazi wake.
Mama Charles akipepesuka kidogo kabla hajadakwa na mumewe, siku za karibuni presha ilikuwa ikimsumbua sana.
Kwake Happy alikuwa na taswira ya kutosha kiasi cha kufanya BP yake ipande kwa kasi.
Hata baba Charles Mr Katesh alionekana kutetereshwa na taswira ya Happy.
Charles alibabaika kidogo hakujiandaa kwa tukio hilo, alipohisi tayari familia yake imeshamuona Happy alimshika tena Happy na kuanza kumkokota kuelekea sebuleni.
Happy alimzuia lakini Charles alilazimisha kumkokota kwenda sebuleni.
“Noooo hapana inatosha tumeona tunaomba muende nje msije hapa.”
Mama Charles alisema.
Charles alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa akijiuliza afanye nini.
“Nendeni nje tafadhali nisije kufa Mimi uwiii.”
Alisema mama Charles huku akiishiwa nguvu na kuangukia kwenye sofa kiasi cha kumkandamiza Careen ambaye alijinasua na kusogea pembeni.
Careen na baba yake walianza kumpepea mwana mama huyo.
Happy alimfinya Charles mgongoni kuashiria watoke nje.
Sio siri Charles alijisikia vibaya sana.
Alimgeuza Happy na kisha kutoka nae nje kwa mwendo wa taratibu.
Alimpandisha kwenye gari na kisha kuegemea usukani mawazo mengi yalipita kichwani kwake.
“Charles tuondoke.”
“I’m sorry Happy sik......”
“Mimi nilitegemea...hii hali hata mimi mwenyewe inanitisha wao ni kina nani wasiniogope?? Najua hawa sio watu wa kwanza na nimejiandaa kwa hili
wala siumii hata na nakuomba uzoee kama utaendelea kuwa na mimi.”
Alisema Happy kwa hekima zake alizojaliwa na Mungu.
Charles hakuongea neno lolote aliwasha gari na kutoka.
Waliofika mataa ya mwenge.
Charles alikata kushoto.
“Charles unaenda Wapi?”
“Wacha twende kwa rafiki yangu Salim nimekuchukua sasa hivi tu nyumbani sitaki mama ajue kilichotokea acha tukapoteze muda.”
Happy hakuongeza neno lolote lile alibaki kimya na safari iliendelea.
Walifika kwa Salim na kwa bahati nzuri walimkuta kwa vile ilikuwa mwishoni kwa wiki, Salim alikuwa akitazama televisheni akiwa peke yake
aliwakaribisha na wala hakumuogopa Happy.
Mkewe aliyekuwa ndani alitoka baada ya kusikia wageni.
Almanusura atoke nduki aliishia kupiga yowe huku akiangukia kwenye kochi.
“Huuuuyuu ndiioo uulikuuwaaa unnaaamsemeeea muummmeee wwaaangu?”
Aliongea kwa sauti ya kitetemeshi.
“Ndio anaitwa happy.”
Alisema Salim.
Happy alikuwa akitabasamu tu muda wote.
Mke wa Salimu alijitahidi sana kumzoea Happy ingawa kwa upande mmoja alitishwa ila utu wake ulimfanya amzoee.
Vinywaji vililetwa na maongezi yalinoga.
Happy alikuwa akiongea mara chache lakini mara zote aliongea maneno ya busara.
Charles alikumbuka alipomuona mara ya kwanza Happy kwenye mdahalo wa hali ya kisiasa uliofanyika mara ya kwanza pale ukumbi wa
Nkurumah chuo kikuu cha Dar es salaam Happy akiwa mwakilishi kutoka chuo cha mzumbe.
Kila aliposimama aliongea maneno ya maana kiasi cha kupigiwa makofi na wanasiasa nguli waliokuwepo huko ndani.
Hakusita kwenda kumsalimia wakati wakipata chai na kuomba mawasiliano yake mengineyo yalibaki kama hadithi.
Wakiwa wanaendelea na mazungumzo sauti kali ya mtoto ililia kiasi cha kuwashtua watu wote hapo.
Mariamu alinyanyuka na kuelekea chumbani ambapo baada ya muda kilio kilikoma.
Huku wakiendelea na mazungumzo mke wa Salim aliwasili akiwa amebeba mtoto aliyekuwa akichezea nywele za mama yake huku
akicheka na kuruka ruka kwa furaha.
Ghafla kicheko na furaha vilikoma mtoto aliangua kilio kikali huku akimng’ang’ania mama yake kwa nguvu na kuifunika sura yake kwenye vazi la mama yake.
Hakukubali kufarijiwa wala kubembelezwa.
“Acha sisi tuondoke nimuwahishe bibie kwao.”
Alisema Charles huku akijilazimisha kutabasamu.
Ingawa Salim hakupendezwa lakini hakuna na namna ili kumfanya Happy asijisikie vibaya.
Aliwatoa mpaka nje na kuagana nao kabla hata hawajaondoka walisikia mtoto yule akiacha kulia jambo lililowapa uhakika alikuwa akimuogopa Happy.
Salim alihuzunika sana kwani kwake Happy alikuwa kiumbe wa kawaida kabisa na alishamzoea.
Waliagana na kisha Charles aliondoka na kumrudisha Happy kwao akiwa kimya kabisa.
Alirudi nyumbani baada ya kuwa amemfikisha Happy nyumbani kwao.
Alipofika alikuta familia yake yote sebuleni.
Hapakua na cha maana walichokuwa wanakifanya bila shaka walikuwa wakimsubiri yeye.
Alipoingia hakutaka kuwaangalia akiendelea kutembea kuelekea chumbani kwake.
“Charles ni nini umeleta hapa una ujasiri wa kumuita mchumba kweli? Ni yeye amekung’ang’ania au ni nini? Tafadhali mwanangu naomba achana na
yule msichana haraka.”
Aliongea mama yake Charles.
“Umemaliza??”
Alijibu Charles.
Kila mtu alipigwa na butwaa, hakuwa Charles waliyemzoea.
“Semeni kila mnalotaka kusema lakini mwisho wa yote mimi ndiye nnayebakia kuwa mwamuzi wa mwisho and I’m sorry maamuzi yangu yanaweza kumuumiza
mtu lakini sasa hivi I will be more selfish ntajijali mimi kwanza......goodnyt.”
Aliongea na wala hakusubiri kujibiwa alijitoma chumbani kwake.
Ukimya ulitawala kila mtu alinyanyuka kivyake baada ya dakika tano mlango wa chumbani kwa Charles ulibisha na bila kusubiri
kuitikiwa mgongaji alinyonga kitasa na kuingia.
“Kaka sishangazwi ma maamuzi yoyote utakayoyafanya fata moyo wako yule msichana mbali na makovu ya moto ni mzuri sana najua nikikutana
naye tena sitamuogopa nitamzoea.”
Careen aliongea na maongezi mengine yakifuata.
Mwishowe Careen alitoka na kumuacha kaka yake alijipumzisha na yeye kuelekea chumbani kwake kupumzika.
Hali ya maisha ndani hapo ilibadilika palitawaliwa na ukimya mzito.
Charles hakutaka kuongea na wazazi wake na wazazi wake hawakutaka kuongea nae.
Careen alikuwa akiogopa kuongea na kaka yake kwa hofu ya wazazi wake.
Careen alitamani aondoke na kwenda alipopanga, hamu ya kukaa hapo nyumbani ilimuisha.
Charles alikosa uchangamfu wake, ilikuwa wazi kuna tatizo linamsibu.
Baada ya Yvonne kujua tatizo la Charles alianza kujinyenyekesha kwa Charles.
Alijua hiyo ndiyo nafasi pekee ya kumpata Charles.
Hata hivyo Charles hakumjali Yvonne kabisa ni kama vile alizidisha kumchukia.
Yvone hakukata tamaa alijipendekeza mpaka kwa familia ya Charles.
Akijifanya kwenda nyumbani kwa akina Charles kumjulia hali wakati asipokwenda kazini.
Mama wa Charles alivutiwa na Yvonne na kumshauri mwanaye amgeukie Yvonne na aachane na Happy.
“Yes Yvonne ni mzuri sana anafaa mno, kama anafaa sana mwambie baba amuoe ili awe mke mwenzake. Kuna mtu aliyekushauri kuolewa na baba?
Kwanini unishauri na unichagulie wewe mchumba? Jukumu lako la kunileta duniani na kunilea umelimaliza sahivi nimekuwa nina maamuzi yangu sitaki mtu aniingilie.”
Aliongea Charles maneno yaliyomuumiza sana mama yake.
Aliondoka kwa ukimya na kujifungia chumbani akilia.
Kamwe hakutaka kuamini kuwa ni akili za mwanaye au alikua kuna mchezo kachezewa.
Alimtuhumu Happy na familia yake kumroga mwanaye.
Aliamua kutokuongea tena na Charles na alijawa na masikitiko mno.
Tangu wakati huo Charles hakuhesabiwa kuwa mwanafamilia hiyo.
Hata baadhi ya mali alizoandikiwa kama sehemu ya urithi zilibadilishwa na kupewa Careen.
Hakuna aliyekuwa akimuongelesha zaidi ya Careen ambaye alikuwa akimpigia simu kwa siri pale anapokuwa mbali na nyumbani.
Careen alimtahadharisha kuwa pasionekane kwamba wanawasiliana maana wazazi wangemfutia mirathi na yeye.
Charles alipokonywa gari aliyokuwa akiitumia kwa shughuli zake binafsi na kutakiwa kuhama pale nyumbani.
“Kuanzia leo sisi sio wazazi wako katafute wazazi wengine wa kuwafanyia dharau na kuwajibu unavyotaka wewe.
Hatuwezi kukaa na mtu mzima mwenzetu ndani ya nyumba yetu si unaweza kujiamulia na hapa nyumbani uondoke ukakae kwako.”
Aliongea mama Charles kwa kumaanisha.
Alimtafuta Yvonne na kumuelezea.
Yvonne alikasirishwa sana maana yeye alitegemea kwamba mama Charles ndiye atakayemsaidia kumpata Charles.
Sasa Charles amefukuzwa hakukuwa na namna tena ya kumpata kupitia familia yake.
Alimtukana sana mama Charles ambaye hakuamini kama huyo ni Yvonne aliyekuwa akimfahamu kwa siku chache zilizopita.
Alijuta na kubaki na maumivu tu.
Charles aliamua kwenda kwa rafiki yake Salim kumuelezea.
Alimkuta akiwa na Razak rafiki yao waliyesoma wote shule ya sekondari Makongo.
“Daaaah sasa utafanyaje bro? Hii ishu ni serious aseee.”
“Me nahama ila kiukweli siwezi kumuacha Happy kwasababu mimi ndiye niliyesababisha akawa vile kama nisingemuita mlimani city basi yasingempata
hayo na kama nisingemlazimisha kuingia ndani asingeungua.”\n
“Wewe siye uliyepiga Bomu pale kwanini ujibebeshe mzigo mzito.
Mimi sijamuona huyo zombie lakini kwa kusimulia tu anatisha sasa wewe utakaaje naye? Kwanini usimuache tu ukatafuta mwanamke mwingine
utakayeweza kwenda nae sehemu mbalimbali? Em waridhishe wazazi wako basi wasije kukupa radhi muache yule zombie amalizie maisha yake
machache yaliyobakia.”
Razak alisema.
“Naona huna ushauri wa maana bora ukae kimya tu rafiki angu, bado hujakuwa tafadhali usichangie lolote hapa.”
Salim aliongea kwa ukali.
“Sikiliza Charles najua unavyojisikia nakuombea kuwa na ushujaa. Happy ameungua lakini haijamuondolea utu wake yeye ni binadamu anahitaji kupendwa na
kuheshimiwa usimkatili jua kuwa usipompenda wewe atatokea tu mtu atampenda na utaumia sana. Kama unampenda kweli usimuache nakusihi Allah atafanya njia
katika hili.”
Charles alibaki kimya tu akiyachambua mawazo hayo.
Baadaye kidogo aliaga na kuondoka akiwa ameshapata mwanga.
Aliyaanza maisha yake mbali na nyumbani tena kwenye chumba kimoja.
Kila alipotoka kazini jioni alipitia kwao akina Happy kumsalimia na kumpelekea vizawadi vigodovidogo.
“Happy nataka kuchukua mkopo ninunue gari...kupanda daladala napata shida sana marafiki zangu wamezoea kuniona na gari maswali yao yananichosha.”
“Kwahiyo unanunua gari kwa ajili ya marafik zako?”
“No sio hivyo ni kwa ajili yangu.”
“Baby sahivi hulipiwi bili na wazazi wako mshahara wako inabidi uulipie kodi ujinunulia chakula, mavazi, mahitaji mengine na bado uweke hela ya tahadhari.
Ukinunua gari bado litakudai mafuta na matengenezo na kodi pia huoni itakuwa unaongeza gharama? Kama unataka kuchukua mkopo nakushauri uufanyie biashara
hiyo faida utakayoipata kwenye biashara utanunulia gari ila hakikisha hiyo hela inazunguka.”
“Mbona hata gari linazunguka baby??”
“Ntakuchapa muone.”
Aliongea Happy akicheka.
“Okay sasa nafikiria nitafanya biashara gani namimi ni mfanyakazi.”
“Biashara hauchagui wewe Karls, ni mazingira ndio yanayokuchagulia biashara. Kabla hujaanza kufikiria faida ya biashara angalia ni akina nani
utakuwa umewasaidia kutatua shida zao.”
“Huuh sijawahi kufikiria hivi, you are so smart my cute girl.”
“Fikiria kuhusu hili.”
Happy alimalizia.
Mawazo yalikuja mengi sana kichwani mwake aliwaza ni biashara gani afanye.
Mawazo hayo yalimrudisha kwa Happy kuomba ushauri tena, alifanikiwa kupata na kuufanyia kazi.
Baada ya miezi kadhaa ya kuhangaikia biashara hatimaye iliweza kuimarika na kuleta faida kubwa.
"Happy hours cafe."
Iliweza kujulikana kila sehemu ya Mikocheni na Dar es salaam.
Ilikuwa ni mgahawa ambao unauza vitafunwa na vinywaji vilaini na vyakula vichache.
Kila siku mgahawa ulifurika watu waliopendezwa na huduma za pale.
Hata wazazi wa Charles walipendelea kupata kuku kutoka Happy hours kwa vile walikuwa watamu sana ingawa hawakujua kuwa ule mgahawa
unamilikiwa na mtoto wao.
Maisha yalizidi kumnyookea Charles huku akisahau kabisa kuhusu familia yake.
Dada yake Careen alikuwa akiwasiliana naye na mara nyingi alimletea maweaving kwaajili ya Happy, maweaving yaliloficha uso wa happy na sehemu iliyoungua kwa kiasi
kikubwa na kumfanya atazamike mbele ya watu.
Mara kwa Mara alikuwa akimueleza jinsi familia ilivyokosa furaha.
Hakuwa na jinsi ya kufanya maisha ya kujitegemea yalikuwa mazuri kwa upande wake.
Alifurahia kilichotokea maishani mwake kwakuwa kilimfanya apate akili na kujitegemea na kufanikiwa aliweza kurejesha mkopo aliouchukua kwa ajili ya
biashara, alinunua gari na pia alianza ujenzi wa nyumba yake mdogo.
Kila mara alimshukuru Happy kwa kuwa mshauri mzuri kwake.
Mara kwa Mara alimuwaza Happy aliyemuona kama malaika hivi, na hapo wazo lilimjia aliamua kuwashirikisha watu wake wa karibu wakiwemo
Salim na Dada yake Careen.
Nao walikuwa bega kwa bega na yeye mpaka mwisho.
Siku moja kati ya Jumamosi kadhaa za mwezi wa tisa Charles alifunga ndoa na Happy.
Ni watu wachache sana waliohudhuria kanisani hapo akiwemo Careen ingawa alihudhuria kwa kutoroka kwa vile familia yake haikumruhusu.
Ndoa ilifungwa salama na baadae kufuatiwa na chakula cha usiku katika hotel ya nyota tano ya White pearls huko Oysterbay.
Baada ya honeymoon kuisha walihamia kwenye nyumba yao mpya iliyokuwa imemalizika.
Upendo wao haukupungua hata kidogo Charles alimheshimu Happy na kumpenda mno, walizidi kubarikiwa na baraka zilizidi katika mwaka wa pili wa
ndoa yao Happy alipojaliwa mtoto wa kiume.
Kila mtu aliyekuwa upande wao alimfurahia mtoto yule.
Alikuwa mzuri kuliko kawaida kadri alivyozidi kukuwa ndivyo alivyozidi kuwa mtoto mzuri.
Mtoto Myles hakumuogopa mama yake wala hakuchukizwa naye familia ilijaa upendo.
“Kama wazazi tu naona tumekosea na tunaomba radhi kwa hili hatuna namna ya kusema kiukweli tumekosea sana....”
Baba Charles alisema wakati walipokuwa wamemtembelea Charles na familia yake huko kawe.
“Wakati mnamuona Happy hawezi mimi nilikuwa namuona anaweza sana na hata yeye alijichukulia hivyo, sura sio roho ulioharibika ni ile mwili
wa nje tu sio wa ndani.”
“Hakika tumeona na tumejifunza.”
Alisema mama charles.
Real love exists.
***** MWISHO *****
Unaweza pia kusoma: