Muonekano wa Giza:

Msaada

Foolish Age - Msimu wa Kwanza - Sehemu ya Tatu (03)

Nilikula kwa uwoga sana ingawa nilikuwa na njaa sana.
Ni muda mrefu sana umepita sijapata lishe ya kueleweka.
Baada ya kumaliza chakula hicho tulinyanyuka na kisha kuelekea sebuleni.
Nilijaribu kumsaidia yule mama kuondoa vyombo hata hivyo alinizuia.
Nilijua kabisa mahali hapo hapanihusu hivyo nitulie tu kama mgeni mara baada ya kusikia kitu ambacho nimeitiwa niondoke na kurudi tena kwenye kibanda umiza changu.

Baada ya kukaa peke yangu muda mrefu, hatimaye mwanamama yule na baba yule walikuja.
Safari hii walikuwa hawana mtoto mikononi mwao, walikaa.
Mwanaume yule alianza kwa kuvuta pumzi, nilizani angeanza kuongea na mimi hata hivyo alianza kuongea na mwanamama yule.

“Simuoni Tayo.”
“Nimempigia simu lakini hapokei.”
Walianza kujibizana wenyewe.
“Ngoja nijaribu tena.”
Wakati mwanamama yule akihangaika kumtafuta Tayo, mwanaume yule alinigeukia mimi na kuanza kuniuliza maswali mbalimbali kuhusu hali niliyokuwa nikiishi.
“Maisha yanaendeleaje mwanangu?”
Nilimjibu tu kwa aibu.
“Yanaendelea vizuri.”
“Kama yanaendelea vizuri basi tunashukuru.”
Wakati huo mwanamke huyo alikuwa akihangaika kutafuta mawasiliano na Tayo aliweza kumpata.
“Hallo.... Tumekaa hapa tunakusubiri wewe mbona hufiki hospitaliii...?!!!”
Kila mtu alishituka, hata mimi pia nilipatwa na woga.
“Hospitali gani? Kuna nini?”
Aliuliza maswali mfululizo.
“Sawa tunakuja sasa hivi.”

Kumbukumbu ya matukio yaliyopita yalianza kupita kichwani kwangu.
Na hasa niliposikia Tayo yupo hospitali moyo ulinidunda kwa kasi.
Tulinyanyuka harakaharaka, tulijizoazoa na kisha kuelekea hospitali.
Bila kupoteza muda tulikurupuka tukikimbiakimbia huku mimi nikibaki tu nikikimbia pasipojulikana.
Nilifanikiwa kutoka hadi nje ya nyumba ile na kusimama getini.
Mwanamke yule ambaye alikuwa mama yangu mzazi alitoka nje akiwa amembeba mtoto na kufuatiwa na mwanaume yule ambaye alikuwa ni baba yangu mzazi.
Tuliingia kwenye gari la familia na kisha safari ya kuelekea hospitali ya mkoa ilipoanza.

Baada ya mwendo mfupi tulikuwa tumeshafika hospitalini hapo watu wengi walikuwa wakiongelea tukio hilo lililotokea, wakiongea kwa vikundi.
Mimi na familia yangu bado hatukuwa tukijua hasa ni kitu gani kilichokuwa kimetokea.
Tulipitiliza moja kwa moja mapokezi.
Mama alienda kuulizia pale mapokezini na kisha kuelekezwa.
Alitoka mbiombio huku na mimi nikimfungia tela hali nikiwa sijui chochote.
Kila mara picha ya Tayo ilinijia akilini kwangu.
Nilijikuta tu machozi yakinidondoka.
“Sijui atakuwa katika hali gani, sijui kama naye yupo kama mimi?”

Baada ya kukimbia kimbia kwa takribani dakika moja, hatimaye tulifika mahali ambapo Tayo alikuwepo.
Hakika hali yake haikuwa nzuri.
Mama alipomuona Tayo alianza kulia.
Aliangua kilio kikubwa sana.
Tayo aliponiona mimi na mama na baba, naye alianza kulia.
Daktari alitutoa nje.
“Sasa nyie mmekuja kumfariji mgonjwa au mmekuja kumuongezea maumivu?
Mtu kama yule anahitaji faraja kutoka kwenu lakini nyie mmekuja mnaanza kulia si mnamkatisha tamaa mwenzenu anahisi anaumwa sana ingawa hali yake siyo mbaya, hampaswi kulia mbele ya mgonjwa.”

Daktari aliongea.
“Samahani dokta.”
Mama alijibu.
Akili yangu haikuwepo hapo kabisa.
Ilinirudisha miaka kumi nyuma.

Sehemu 2 Sehemu 4
0
0