Muonekano wa Giza:

Msaada

Foolish Age - Msimu wa Kwanza - Sehemu ya Nne (04)

*****Wakati uliopita.******

Katika familia yetu tulizaliwa watoto wawili tu mimi na Tayo.
Baba yangu aliitwa Samweli.
Baba yangu alikuwa akifanya kazi katika taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyokuwa ikijulikana kama Health Tanzania ambayo ilikuwa ikijishughulisha na maswala ya afya ya jamii.
Hivyo alikuwa akizunguka sehemu mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha huduma bora ya afya inatolewa katika vituo vya afya na katika maeneo ambayo huduma za afya zilikuwa hazipatikani.
Waliweka kambi kwa muda kutoa huduma kwa vile baba yangu alikuwa na taaluma ya udaktari.
Na pia walifanya takwimu ili kukusanya taarifa ambazo zingeisaidia serikali katika kutoa taarifa za kuhusiana na afya ya jamii kwa ujumla.

Mama yangu alikuwa ni mfanyabiashara, yenye alikuwa msambazaji wa bidhaa za kampuni ya A.L.L ambayo ilikuwa ikijishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za usafi.
Kwa mfano dawa ya meno, sabuni za kuogea, za kufulia, dawa za kusafishia na vitu vingine kama hivyo.

Nilimzidi mdogo wangu Tayo kwa kiasi kama miaka mitatu na wakati huo mimi nilikuwa kidato cha kwanza Tayo alikuma yuko darasa la saba.
Kabla sijafika kidato cha kwanza mimi na Tayo tulikuwa tukisoma shule moja ya The Heavenlight Academy ambayo ilikuwa Kahama mjini na hata baada ya kumaliza elimu yangu ya msingi nilienda kujiunga na The Hollywood High School ambayo ilikuwa huko huko Kahama.

Mwaka wangu wa kwanza shuleni nikiwa kama kidato cha kwanza nilikuwa mzuri sana.
Shule yetu ilikuwa ni ya kifahari sana ambayo ilikuwa ikishindana na The Underlake Ridges ilikuwa kama hoteli ya kifahari.
Wazazi wangu walilipa ada kubwa sana kwa sababu hawakupenda tuishi maisha ya shida.
Tulikula vizuri, tulikunywa tulichotaka, tulilala sehemu nzuri, mazingira yake yalikuwa ni mazuri sana.
Tulikuwa haturuhusiwi kutoka kabisa isipokuwa kwa jambo maalumu.

Wakati niko kidato cha kwanza nilipata marafiki wengi.
Shule yetu ilikuwa ni ya mchanganyiko.
Miongoni mwao walikuwa ni Christina, Janel, Dominic na wengineo wengi.
Nilifurahi sana kukutana nao.
Hata hivyo kati ya wote marafiki ambao walikuwa karibu na mimi zaidi walikuwa ni Christina na Janel.

Tulipendana sana hadi kutokea kuitwa mapacha watatu.
Kila sehemu tulifanya mambo yetu pamoja.
Mimi na Christina tulipangiwa chumba kimoja, vyumba vyetu vilikuwa ni vya watu wawili wawili.
Janel alikuwa akikaa kwenye chumba kingine na msichana mwingine ambaye alikuwa akiitwa Maria.
Kukaa kwetu chumba kimoja mimi na Christina kulizidisha mahusiano yetu.
Tulikuwa karibu zaidi na tulifanya vitu vingi pamoja.
Tuliambizana siri zetu za ndani, tukaambizana matatizo yetu na hata furaha zetu zilikuwa ni za pamoja.
Nilifurahi sana kupata rafiki mzuri kama Christina.

Christina alikuwa ni msichana mzuri sana.
Alikuwa na rangi nyeusi ya kuvutia, macho yake makubwa na sura yake iliyopambwa na midomo mizuri kabisa, alikuwa na pua yake ndogo, alikuwa mrefu kunizidi na alikuwa na umbo zuri sana.
Kutokana na sifa zetu pale shuleni mapacha watatu tulikuwa wazuri sana na warembo kuliko wote shule nzima.
Kati ya wote mimi nilikuwa mrembo zaidi yao nilibarikiwa mwili ambao watu walizoea kuita umbo namba nane.
Sura nzuri, macho makubwa ya duara, vilipsi vyangu vidogo hakika viliupamba uso wangu na zaidi ya yote sauti yangu nzuri ya kuvutia.

Walimu walinipenda sana kwa vile nilikuwa vizuri katika kuongea kingereza na pia nilijitahidi sana katika masomo yangu.
Pamoja na yote hayo mapacha watatu tulikuwa tukifanya vizuri sana na kulikuwa na ushindani mkubwa katikati yetu.
Maisha yangu wakati nipo kidato cha kwanza yalinifanya niwe maarufu sana pale shuleni.
Tulijulikana hadi kwa kidato cha sita.
Kila wadada wa kidato cha sita walipenda tuwe wadogo wao.

Sehemu 3 Sehemu 5
0
0