Foolish Age - Msimu wa Kwanza - Sehemu ya Tano (05) 
Tulikuwa gumzo vinywani mwa kila mwanafunzi Hollwood High School.
“Yani hapa shuleni kuna warembo wengi lakini Naomi, Christina na Janel wamewazidi wote, hawa watoto ni very hot.”
Ni mazungumzo ya kila siku yaliyokuwa yakisikika hapo shuleni.
Hata hivyo hatukujali, tulipendelea sana kusoma.
Mara nyingi sana Janel alikuwa akitumia muda wake mwingi kukaa kwenye chumba chetu.
Alikuja, tulipiga stori mpaka muda wa kwenda kulala mara baada ya kutoka prepo na siku za mwishoni mwa
wiki alikuwa akikaa chumbani kwetu muda wote.
Siku nyingine alilala kabisa ingawa matroni alikuwa akizuia sana kulala kwenye vyumba ambavyo sio vya
kwetu lakini kiubishi ubishi tu alilala.
Alipoamka asubuhi, Janel alikuja kwetu kuanza kutuamsha.
“Amkeni nyie mnapenda sana kulala.”
“Aanh wewe asubuhi asubuhi yote hii unaenda kufagia madarasa? Au leo zamu yako?”
“Aanh amna bwana amkeni tujiandae.”
Janel alipenda sana kuamka mapema ingawa alikuwa anapenda sana kulala.
Kati ya wote mimi nilikuwa nikiongoza kwa kulala, nilipenda sana.
Muda wangu wa usiku niliutumia kusoma.
Christina alipenda sana kulala hata hivyo alikuwa akiamka usiku wa manane kusoma, alisema huo muda
ndiyo ambao anaelewa vizuri.
Sikuweza kumpinga kama ni muda wake ambao alikuwa anasoma na kuelewa nilimuacha awe huru kwa ajili ya matokeo mazuri kwetu wote.
Ilikuwa ni sheria yetu mtu anaposoma hakuna kumsumbua.
Mimi na Christina tulikuwa ni waromani katoliki wakati Janel alikuwa ni mlutheri ambaye yeye alikuwa akisali katika Umoja wa
Wanafunzi wa Kikristo Tanzania. (UKWATA.)
Walimu walitupenda sana na pia tulifanya vyema katika masomo yetu.
Katika tatu bora tulikuwa tukibadilishana tu namba, hii ilifanya walimu wazidi kutupenda.
Hata hivyo ilifanya shetani pia azidi kutupenda.
Nilienda nyumbani wakati wa likizo baada ya kumaliza kidato cha kwanza.
Mdogo wangu Tayo naye alitaka kuja kusoma shuleni kwetu hasa baada ya kusikia sifa za shule yetu.
“Na mimi nataka kwenda kusoma Hollywood na dada.”
“Mimi nilikuwa nataka nikusomeshe shule ya tofauti.”
Mama yangu alisema.
“Hapana mimi nataka kwenda kusoma huko huko.”
“Sawa kama unataka mtaenda wote.”
Hatua za mwanzo kabisa za kumpatia nafasi katika shule yetu zilikamilika.
Likizo yangu ilikuwa nzuri sana kwani tulienda kutembea maeneo mengi ya burudani tulijifunza
mambo mengi.
Ingawa kwetu haikuruhusiwa kutoka bila kuwa na uangalizi maalumu nilijihisi kama mfungwa.
Shuleni nabanwa, nyumbani nabanwa.
Hata hivyo kwangu ilikuwa kawaida sana.
Baada ya likizo tulirejea shuleni nikiwa nimeongozana na Tayo.
Mwaka huo ulikuwa wa tofauti sana sio kama uliopita.
Kila kitu kilichokuwepo kilibadilika.
Takribani saa kumi na moja za jioni mimi na familia yangu yote akiwemo msichana wetu wa kazi Sabina
ambaye wote tulizoea kumuita Bina tuliwasili shuleni kwetu The Hollywood High School.
Familia yote tulifunga safari kutoka Shinyanga mjini mpaka Kahama kwa ajili ya kutupeleka shule mimi
na mdogo wangu Tayo.
Tulichelewa sana, shule ilikuwa imeshafunguliwa wiki moja kabla.
Nadhani marafiki zangu wote Christina, Janel na Wengineo walikuwa tayari wameshawasili.
Tulipofika baba alitupeleka moja kwa moja hadi ofisini kwa mwalimu na baada ya maelezo machache
walielekezwa kutuacha na kisha kuondoka.
Baba alitukabidhi kila kitu ambacho kilihitajika.
Niliagana na mama na baba kwa huzuni pamoja na dada yetu wa kazi.
Waliondoka na kisha nilimuongoza Tayo.
Hatukupiga hatua chache tulikuja kupokelewa na Christina ambaye bila shaka alikuwa amenimisi sana
alikuja na kunikumbatia kwa nguvu huku akinirukia alimanusra tuanguke.
“Waooo!! Naomi nilikumisi jamani.”
Tulikumbatiana takribani dakika moja nzima huku Janel alikuwa amesimama pembeni bila shaka alikuwa akiona wivu jinsi tulivyokuwa
tumekumbatiana kwa furaha.
Unaweza pia kusoma: