Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Jabali - 01

Kunako nchi ya Katesh inayotawaliwa na mfalme Katesh…
Mvua kubwa ikiwa inanyesha, radi na nguvumo za kutisha zikiwa zinarindima nje.
Ndani ya jengo moja kubwa ambalo ndiyo ngome kuu ya mfalme Katesh wa nchi ya Kateshi ambapo jina la nchi hiyo lilibadilishwa jina pindi alipoweza kuingia madarakani na kuamuru jina la nchi hiyo liwe Katesh, ikiwa ndiyo jina lake.
Mkutano mkubwa ulikuwa ukiendeshwa ndani ya ngome hii, mkutano huo ulikuwa unahusu agenda ya kupungua kwa nguvu ya mfalme katika tawala yake.
Nguvu ya mfalme ilikuwa imepungua kwa kiasi kikubwa ndani ya muda mfupi jambo lililozua hofu kubwa katika tawala ya Katesh na wananchi wake.
Tatizo hilo lilianza kutokea miezi michache kabla ya mkutano huo mkubwa kuitishwa.
Chanzo cha tatizo hakikuwa kimejulikana mpaka hapo.
Kupungua kwa nguvu ya Mfalme Katesh kulizua maafa makubwa sana ndani ya hiyo miezi michache kabla mkutano huo mkubwa kuitishwa.
Baadhi ya maafa yaliyokuwa yameikumba himaya hiyo mojawapo ni kuvamiwa na kushambuliwa vibaya sana na ngome jirani.
Ngome hiyo ilikuwa inamilikiwa na Mfalme Kadevu, mfalme huyo alikuwa hapatani na Katesh hata chembe.
Tatizo la kutoelewana kwao lilikuwa ni mgogoro wa mipaka kati ya Katesh na himaya ya Kadevu iliyoitwa Kijito.
Himaya hiyo ilikuwa ndogo mara kumi zaidi ya Katesh.
Inasadikika himaya hiyo ilijitenga baada ya majeshi ya Mfalme Kadevu kuidhibiti himaya hiyo kutoka kwa majeshi ya Katesh.
Sasa siku hii ya leo mfalme anaamua kuitisha mkutano mkubwa ili kuweza kulizungumzia swala hili na hata kulifikia muafaka.
Mamia ya watu walifulika katika ukumbi huo mkubwa katika ngome ya mfalme wao, ukumbi ambao ulikuwa ni mahususi kwa maswala ya mikutano pamoja na sherehe mbali mbali zilizokuwa zikifanyika katika ngome hiyo.
Jeshi kubwa lililokuwa na askari wapatao mia tano! Waliweza kuizingira ngome hiyo ili kuhakikisha usalama wa raia wote waliokuwa wameshiriki mkutanoni.

Mfalme alisimama katika kiti chake kikubwa cha kifalme kuwasalimia watu wake.
Kelele kubwa za kumshangilia zikazuka! Watu walishangilia kwa kumpungia mikono juu!
Ikiwa na ishara kubwa kuwa walikuwa wakimpenda mfalme wao kutokana na utawala wake mzuri aliokuwa akiuendesha.
Baada ya shamra shamra za salamu kukoma, wananchi pia walitulia.
Lakini mfalme yeye aliendelea kusimama.
Pembeni yake kukiwepo na Askari kazaa waliokuwa wameshika mikuki ya maana kumlinda.
“Ndugu wananchi ninashukuru sana kwa utiifu wenu mkubwa mlioweza kuuonesha katika kutii wito huu wa kukusanyika mahali hapa.
Bila shaka kiu yenu kubwa ni kutaka kujua mmekusanyika hapa kwa lipi?”
Mfalme alisema na kuweka kituo.
Yowe kubwa likalipuka ukumbini.

“Ndiyooooooooooo!!!”

Watu walitandaza viganja vyao hewani kumpungia mfalme wao mkono, mioyoni mwao wakiwa na shaukuu kubwa ya kutaka kujua kinaga ubaga hasa kilicho ndani ya agenda ya mkutano huo.
“Asanteni sana! Sasa tusikilizane!”
Ukumbi mzima ukatulia kimyaa! Mvua ndogo ya manyunyu ndiyo ikawa ikisikika huko nje!
“Agenda kuu ni kuhusu hali ya usalama ya Katesh ambayo imeanza kudidimia kwa kasi sana kuanzia siku za hivi karibuni.”
Maneno hayo ya mfalme yaliwatia kiwewe watu vibaya mnoo!
Kila mmoja moyo ulianza kumdunda kwa fujo ikiwa ni hamasa ya kutaka kujua kile kitajadiliwa au kuzungumzwa katika agenda hiyo.
“Tumeshuhudia ndugu zetu wengi sana hasa walioko karibu na mpaka wa Kijito wamekuwa wakiuliwa sana! Sana! Sana!
Hii imetokana na kupungua kwa nguvu ya jeshi na uongozi kiujumla!”

Mfalme aliweka kituo na kuwafanya watu watu wake wajawe na shaukuu kubwa ya kutaka kusikia na kujua sababu ya kupungua kwa nguvu ya jeshi na utawala ndani ya Katesh.
“Miezi mitatu iliyopita, kulitokea mfarakano hapa ndani ya ngome.
Mke wangu mmoja alipokea hongo kutoka kwa watu walio na makazi katika mji wa siri, mji ambapo wakazi wake siyo watu wa kawaida bali ni wafu!
Mji huo uko chini ya ardhi lakini siyo usawa huu bali ni kwamba mlango wa kuufikia mji huo uko magharibi ya mbali saana.”

Kila mmoja alishtuka kusikia hivyo! Wengi walianza kuogopa!
“Mmmmh! Wafu tena!”
Minong'ono ya hapa na pale ilizuka!
“Ngu! Ngu! Ngu!”
Ngoma yenye mlio mkubwa iligongwa mara tatu kuashiria utulivu unahitajika.
“Jamani tunaomba utulivu uchukue nafasi yake ili tuweze kusikilizana.”
Mfalme alisema.
Utulivu mkubwa ukajitokeza, na hata mvua ilishakatika nje hivyo kukawa kimyaaa!
“Mfarakano huo na mke wangu ulihusu mambo ya kifamilia, mfarakano ambao ulidumu kwa muda mrefu kidogo pasipokuwa na suluhu hali iliyopelekea mke wangu kutorokea mji wa siri waishio wafu!”
Maneno yale ya Mfalme yakawafanya wananchi wote kushika vinywa vyao alama za viulizo zikawajaa vichwani mwao!
Hawakutaka kuamini kile walichokisikia! Kwani ilikuwa ni ajabu mno mtu mzima kwenda kuungana na wafu kwanza angeishi vipi?
Ikiwa wafu chakula chao ni nyama za binadamu je? Huyo yeye asingeliwa?
Lakini pia licha ya hilo! Wananchi walijiuliza mara kadhaa ni sababu gani haswa iliyopelekea mwanamke huyo kufanya jambo la kimaajabu namna hiyo!
Lakini yote kwa yote! Swali kubwa lililogonga vichwa vya wengi ni kwamba mwanamke huyo alitoroka na nini mpaka kupelekea nguvu ya utawala na jeshi kupungua?
Hawakuwa na majibu yoyote zaidi ya kusubili maelezo kamili kutoka kwa mfalme wao.
Je? Sababu kubwa ni nini? Na alitoroka na nini? Kwa sababu gani? Eee!
“Ninajua wote mnahitaji kupata kujua kwanini ilikuwa hivyo? Na alitoroka na nini?
Kiufupi sitoweka bayana matatizo yangu ya kifamilia yaliyopelekea mke wangu kuchukua uamzi huo, isipokuwa nitaelezea dosari aliyoisabisha mpaka himaya yetu kuyumba katika nguvu ya utawala na kijeshi.”

Mfalme alisema na kuweka kituo.
Watu wakazidi kushikwa na kiwewe cha kutaka kujua sababu hiyo inayotarajiwa kuwekwa bayana.
Utulivu mkubwa ukatawala ukimbini.

Sehemu 2
0
0