Jabali - 04 
Taratibu walianza kurejea mahali walipomwacha Nkalo akiota moto, kumbuka kuwa Sango alimvuta chemba kidogo Mulah ili aweze
kumdodosea hali inayokwenda kutokea ikiwa watakwenda na mschana huyo.
Mulah alifikiria sana jinsi ya kumwingia Nkalo kwanza ni m’bishi pili hatoweza kumwelewa kabisa ikichangia na mazingira
yenyewe yatishavyo siyo rahisi kabisa Nkalo kushawishika kubaki peke yake katika sehemu ile.
Mulah hakutaka kuunzisha mjadala huo usiku, alitaka kukuche kwanza! Ndipo akianze kibarua hicho.
Kilichofuatia hapo ni maongezi mareefu ya hapa na pale ili kuusindikiza usiku, hakuna aliethubutu kulala mpaka kunakucha!
Ajabu ni kwamba eneo lote lile hakukuwa hata na ndege kwani walitegemea kusikia vijogoo vya ndege vikiwika, lakini haikuwa hivyo.
Mpaka jua linachomoza hakuna ndege wala mnyama aliesikika akilia au kuungurua katika maeneo hayo!
Baada ya kuwa kumekucha sasa! Ndipo Mulah alipokianza kibarua kile cha kujaribu kumshawishi Nkalo abaki maeneo yale mpaka warudi kwani ni hatari kwenda nae katika mji huo!
Aisee! Hapo alikutana na mwamba! Hakumwelewa hata chembe! Kwanza aligeuka mbogo!
“Unasikia Mulah?
Mi siwezi kubaki hapa hata iweje, Kwanza haya mazingira wayaonaje?
Siwezi nasema tena siweziii.”
Alisisitiza Nkalo!
“Haya yote umeyataka mwenyewe Nkalo ona sasa unakwenda kuniponza na mimi nife kweli?”
Mulah aliongea kwa sauti iliyojaa masikitiko! Nkalo akabaki akimtizama tu!
“Kweli Nkalo wewe baki hapa kule kubaya shemeji hakukufai wewe!”
Sango nae aliingilia kati na kuzidi kumshawishi Nkalo ili akikubali wamwandalie sehemu aweze kukaa pale mpaka watakapoweza kurejea na kumchukua iwapo atakuwa bado hai.
Ushawishi ulikuwa mkubwa sana hasa upande wa Mulah alim'bembeleza sana tena kwa kutumia maneno matamu matamu mpaka mtoto akalainika.
“Sawa, lakini kwa mazingira haya sizani kama mtanikuta nikiwa hai.”
“Usihofu eneo hili linatisha kimazingira tu! Lakini liko salama kabisa!”
Mulah alizidi kumshawishi Nkalo hatimae akakubali, alikubali kwa moyo mmoja kuwangoja katika eneo ambalo wangemwekea kambi mpaka pale watakaporejea kutoka mji wa wafu.
Ilikuwa ni siku ya 39 Sasa yalikuwa yamesalia masaa tu kuweza kufika katika eneo lenyewe!
Vijana hao walikuwa wameshaianza safari tangu kulivyokucha, kila walipokuwa wakipumzika njiani waliitoa ramani yao na kuipitia pitia kisha walirudisha begini.
Safari ikawa inaendelea,
“Tutafika saa mbili usiku eneo ulipo mlango huo!”
Mulah alisema..
Walitembea sana hatimae ilipotimu saa kumi na mbili kasoro walikuwa wamekaribia eneo lenyewe. Na hapo sasa ndiyo iliwabidi kutengana na Nkalo.
“Nkalo sasa tunakutengenezea kambi ndogo hakikisha unakaa hapa mpaka tunarejea sawa ee?”
“Haya!”
Nkalo alikubali, lakini moyoni alijawa na wasi wasi mno hakuwa na uhakika kama uhai wake ungekuwa salama kama angebaki peke yake katika eneo lenye kutisha kama lile?
Hata hivyo hakuwa na namna ilibidi akubaliane na hali halisi.
Tayari eneo lilipatikana, Sango na Mulah walianza kukata miti ya kujengea kibanda hicho kidogo kwa kutumia majambia yao.
Kazi haikuwa nzito mpaka inatimu saa moja kazi ilikuwa imekwisha, walikoka moto chakula kikapikwa wakala kwa pamoja mpaka wakatosheka.
“Hili ndilo eneo ambalo tuliambiwa tujipake dawa zile usoni ili tuweze kuuona huo mlango!”
“Ndiyo zitoe sasa tujipake hapa hapa.”
Mulah alisema, Sango akamuunga mkono.
Begi lilifunguliwa, kikopo kidogo chenye dawa kikatolewa!
Wote wawili wakaanza kupaka nyuso zao!
“Hebu tutoke nje kuona kupoje?”
Mulah alimwambia Sango, na wote wakatoka nje!
Kumbe wakati wanatoka kuna kosa kubwa walikuwa wamelifanya huku nyuma!
Aisee!
Baada ya kutoka nje walikutana na tawira mpya ya nchi, ile milima waliyokuwa wameiona mwanzo haikuwa hiyo tena! Milima ya ajabu zaidi ilionekana mbele ya macho yao!
Kubwa zaidi walikutana na taswira kubwa yenye umbo la fuvu la binadamu, fuvu hilo lilikuwa kubwa mno!
Pia kinywa chake kilikuwa ni mara tatu ya lango kuu la kuingilia katika ngome ya mfalme wa Katesh. Hakika ilikuwa ni zaidi ya maajabu mno.
“Mlango ndiyo ule pale!”
Sango alisema!
“Looh!”
Mulah aliishiwa nguvu…
Kama ni mlango tu unatisha hivyo je? Mji wenyewe ndiyo itakuwaje?
Walirudi ndani na kufungasha kila kitu, Mulah alimkumbatia mpenzi wake Nkalo na kumhakikishia kuwa angerudi salama na kuja kuondoka nae kurudi Katesh.
Nkalo alikubaliana nae huku machozi yakim’bubujika alijua wazi kabisa kurudi kwa vijana hao ilikuwa ni ndoto haikuwa rahisi kabisa.
Wakaondoka!
Na kuanza kuusogelea taratibu taratibu mlango huo.
Kwingineko...
Ndege aliekuwa amepangwa kutumwa siku ya 39 kwenda kuungana na vijana hao katika safari ya kufika katika mji wa wafu na kuchukua jabali la kifalme katika mji huo alishatumwa.
Ndege huyo alikuwa ni ndege wa kimaajabu sana!
Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuunganisha mawasiliano kati ya mfalme na vijana hao.
Ndege huyu alikuwa na uwezo wa kupotea na kuibukia sehemu.
Na sasa alikuwa amekwishawasili katika mlango wa mji huo kabla hata Mulah na mwenzake hawajafika!
“Katika utaalamu wako unaweza kuwaona vijana hao walipo mpaka sasa?”
“Ninaweza kutambua iwapo ndege huyu atarudi kutoa taarifa hapa.”
“Ahaa! Unamaanisha atakuwa akienda na kurudi?”
“Ndiyo atakuwa akienda na kurudi kutupatia taarifa juu ya kile kinachoendelea huko!”
“Sawa ndugu mtaalamu.”
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Mtaalamu au mganga wa mfalme na mfalme mwenyewe.
Ile wakiwa ndiyo wanamalizia kuongea yale ndege huyo akawasili na moja kwa moja akatua juu ya bega la mganga huyo tayari walianza kuwasiliana na mganga huyo kimiujiza!
Mfalme alikuwa kimya pembeni akingojea majibu.
“Mtukufu Mfalme! Ndege huyu anasema!
Vijana wamekwisha kufika katika mlango wa kuingilia katika mji huo lakini tayari kuna kosa kubwa wawekwisha litenda.”
Mfalme kusikia hivyo alitahamaki.
“Lipi tena?”
“Wamekwisha gawanyika mmoja kabaki duniani, na wawili wanakwenda, halafu kubwa zaidi ramani hawana jambo ambalo ni hatari kubwa sana kwao
wanakwenda kupotea na kugeuzwa kitoweo na wafu kwani watakwenda kichwa kichwa bila mwongozo wowote!”
Mfalme kusikia hayo alishika kichwa! Alijua sasa balaa linakuja wafu wakienda kuvurugwa wanapanda Duniani na kuja kusabisha maafa makubwa sana!
Ilitakiwa lifanyike jambo la haraka sana kabla mambo hayajaharibika!
“Hili ni tatizo kubwa sana! Yahitajika tufanye jambo vinginevyo linatukost hili.”
Mfalme alisema hayo huku uso wake ukionekana kukosa amani kabisa.
“Sasa mtukufu Mfalme ni jambo gani tunaweza kulifanya? Ikizingatia muda wenyewe umekwisha?”
Mtaalamu huyo wa mambo ya giza alihoji.
“Tukusanye askari wa kutosha tuchukue farasi wenye nguvu ya kukimbia kwa kasi na umbali mrefu kwa mda mfupi tuwahi mlangoni kule ili
litakapotokea la kutokea tunapambana nao hapo hapo.”
Mfalme alitoa wazo, wazo ambalo liliungwa mkono kwa asilimia zote na mtaalamu wake hapo.
Mara moja ndege huyo alitumwa kwa mara nyingine kwenda kuleta taarifa za huko, wakati huo ukifanyika utaratibu wa kukusanya askari wa kutosha na farasi waliotajwa.
Ndege huyo alipotea baada ya kutumwa.
Tarumbeta likapigwa!
Mara moja askari wengi wapatao elfu moja walikusanyika katika uwanja ulio mbele ya ngome ya mfalme.
Mulah na Sango walifanikiwa kuufikia mlango huo wa kuingilia katika mji wa wafu.
Hakika palikuwa panatisha mnoo!
Giza nene lilionekana kutanda ndani hali iliyowafanya kuanza kuogopa!
“Shika Silaha mkononi washa mshumaa.”
Sango alisema.
Mulah nae alifanya vile alivyoelekezwa na mwenzake, mishumaa ikawashwa unafuu ukapatikana kwani njia ilianza kuonekana!
Kitu cha ajabu ni kwamba mle ndani kulikuwa kama pango hivi halafu kulikuwa na umande umande flani wenye asili ya uozo uliokuwa
ukitoa harufu kali haijapata kushuhudiwa!
Na eneo lenyewe lilizidi kwenda ndani zaidi giza nalo lilizidi kipimo halafu kulikuwa kimyaa!
Hawakuogopa!
Walizidi kusonga wawili hao huku wakisapotiwa na mishumaa iliyo wafanya waweze kuona waendako…
Wakafika sehemu, kuna jiwe kubwa lililolala kuifuata njia ile!
Kwa juu kulikuwa kuna maji yenye utelezi yalikuwa yakichuruzika na kutua juu ya lile jiwe kisha hutililika kuelekea chini zaidi.
Maji haya yenye utelezi yalipelekea jiwe hili kuwa na utelezi wa ajabu na kibaya zaidi hawakuwa wakilitambua hilo! Wao wakajitupia tu!
Wewee!
Gafla Sango akateleza na kutulia magoti, mshumaa ukaenda kutua huko jambia ndiyo alijitahidi kulidhibiti lisimponyoke.
“Mulah nisaidie kuna balaa hapa!”
Ilibidi Sango amwombe msaada mwenzie kwani kila anapojaribu kushika anakutana na utelezi ilihali anazidi kwenda taratibu chini ambako ni giza tupu!
Mulah kusikia hivyo alianza kuhangaika namna ya kumuokoa mwenzake!
Mara nae kakanyaga pambaya! Huyo! Akateleza na kwenda kumvaa mwenzake!
Hapo ndipo ikawa kizaa zaa sasa! Kwani uzito uliongezeka mara dufu wakajikuta wakianza kwenda kwa kasi chini kuliko na giza la kutisha!
Unaweza pia kusoma: