Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Jabali - 03

Sango, Nkalo na Mulah waliendelea kutembea umbali huo mrefu sana ambapo kila siku ilipofika jioni waliweka kambi sehemu na kulala, hatimae kulipokucha siku ya pili waliendelea na safari.
Siku kumi na tano zikayeyuka, vijana hao wakiwa bado wakipambana na safari.
Migongoni mwao wakiwa wamebeba dhana na vyakula kwaajili ya safari.
Miongoni mwa dhana walizokuwa nazo ni majambia makubwa yaliyokuwa na hara zake, mishare kadhaa yenye sumu na pinde zake, vile vile kila mtu alikuwa na burungutu kubwa la kama ya kusokota.
Mahitaji yote hayo yalikuwa ni kwaajili ya kuikamilisha safari hiyo!

Tukija huku yaliko makazi ya chifu, yaani katika ngome ya Katesh, mkusanyiko mkubwa wa askari ulishuhudiwa ndani ya ngome hiyo.
Maongezi maalumu yalikuwa yakiendelea.
Mfalme alikuwa amewakusanya askari hao vile vile alimchukua na mtaatalamu mmoja mwenye ujuzi juu ya mambo ya giza ili aweze kuwasaidia katika kazi iliyokuwa mbele yao.
“Vijana watatu wamesafiri kwenda mji wa wafu kulifuatilia jabali hilo, na lolote linaweza kutokea huko tunahitajika kuwa macho mda wowote.”
Mfalme aliyasema hayo akiwa mbele ya umati mkubwa wa askari wake. Kila mtu alikuwa makini kumsikiliza.
“Nipo na mtaalamu wangu hapa, mtaalamu huyu atatumia ndege atakaekuwa anasafiri mpaka mji wa wafu kuchukua taarifa na kutuletea.”
Watu wote walipiga makofi.
Pembeni ya Mfalme alikwepo mtu mmoja ambae bila shaka alikuwa mganga wa kienyeji, hayo yalijidhilisha katika mavazi yake, kwani alivaa mavazi ya kutisha mno!
Kichwani akiwa kajifunga kitamba cheusi alichokuwa kimewekewa manyoya ya ndege kuzunguka kichwa kizima!
“Niliwaita hapa kuwataarifu inawezekana wengine hamkuwa na taarifa juu ya kile kinachoendelea.
Hivyo kaa ukitambua ukisikia tarumbeta ikipigwa usipoteze muda tumeelewana?”

“Ndiyooo!”
“Mnaweza kutawanyika sasa!”
Kufikia hapo mkutano huo mdogo ukaishia hapo na kundi lote la askari kutawanyikia maeneo mbali mbali.
Mda huo huo vikundi viliundwa, askari walikwenda kukaa katika vikundi na kuanza kujadiliana kuhusu kile kilichokuwa kimetokea.
Askari wengi hawakujua kama wanaweza kushirikishwa katika hilo.
“Huyu Mfalme hajielewi kabisa hivi nani atathubutu kupigana na wafu?
Maana huu ni msala sasa hiyo mijitu ikienda kutibuliwa huko itapanda duniani haraka sana sijui itakuwaje?”

Askari mmoja alisikika akiyasema hayo.
Ni wazi kabisa alikuwa akiliogopa jambo hilo!
“Lakini wewe ni mwanaume! Wewe ni askari utaanzaje kuwa mwoga kiasi hicho?”
Mmoja alimjibu.
“Hata kama! Angalia na vitu vya kufanya, siyo kutafta kifo makusudi.”
“Kwahiyo kwa kusema hayo unamaanisha hauko tayari kupambana na vita hii kuitetea ardhi ya Katesh na wakazi wake?”
“Nitajaribu lakini sina uhakika juu ya hilo, mambo yakiniwia ugumu ninaweza kwenda hata kujitosa kwenye mikono ya Kadevu ila niwe hai..!”
“Hahahaha! Mwehu wewe thubutu uone utauliwa!”
Hayo yalikuwa ni mazungumzo katika moja kati ya vikundi.
Hali hii inaashiria kuwa ikitokea vita baadhi ya askari ni waoga na watakimbia.

Kwingineko, Mfalme Katesh alikuwa pamoja na mtaalamu wake wakijadiliana jambo muhimu.
“Huyu ndege atatumwa mda gani mtaalamu?”
“Ndege huyo atatumwa maasaa 12 kabla ya kuwasiri katika eneo husika.”
“Naam! Nimekuelewa hapo mtaalamu, na je? Unavyojaribu kufanya utabiri unafikiri nini kitajiri huko?”
“Aaah! Utabiri wangu upo matatani maana mji huo kwa kweli una jeshi kubwa, vile vile kuna uangalizi wa hali ya juu! Hata kutabiri ni vigumu sana.”
“Sawa, nimekuelewa... Sasa fanya kazi hiyo ndani ya mda.”
“Ndiyo ninaifanyia kazi na ninahitaji ndege huyu atumwe siku ya 39 ya safari kwa vijana hao na atakwenda kuwakuta katika mlango wa kuingia katika mji huo.”
“Basi hakuna neno fanya kazi.”
Alikuwa ni Mfalme na mtaalamu wake wakiwa katika chumba kimoja ndani ya ngome hiyo, mpango wa kutumwa kwa ndege huyo ndiyo ulikuwa ukisukwa ndani ya chumba.

Ilikuwa ni asubuhi na mapema, katika eneo moja lililo kati kati ya milima, anga lote la mashariki lilikuwa limepambwa rangi nyekundu iliyosababishwa na mwanga wa jua uliokuwa karibu kuutawala ulimwengu baada ya giza kuachia ngazi.
Vijana hawa watatu walio na safari moja ngumu sana, sasa walikuwa wakijiandaa kuendelea na safari.
Hii ni baada ya kuweka kambi sehemu hiyo jioni ya siku iliyopita.
Na hiyo ilikuwa ni siku ya 38, siku moja tu ilikuwa imesalia vijana hao kufika katika eneo lenye huo mlango.
Kama ilivyokuwa kawaida, baada ya maandalizi safari iliendelea.
Sasa kitu kilichoanza kuwatia mashaka katika safari ya siku hiyo ni kwamba kila walivyozidi kwenda mbele, hali ya hewa na mazingira vilianza kuwatia uoga kwa jinsi kulivyoanza kutisha kila walivyozidi kwenda.
Hali hiyo pamoja na mazingira vilikuwa ni mabadiliko ya hewa yaani kila walivyozidi kwenda hewa ilianza kutoa harufu mbaya iliyokuwa ikizidi kila walivyozidi kwenda mbele.
Mazingira pia yalianza kuwa kituko taratibu, yaani milima ya ajabu ajabu ilianza kuonekana!
Hata baadhi ya milima ilikuwa imebeba taswira za mafuvu ya watu!
“Mmmh!”
Kila mmoja alianza kuguna kivyake moyoni.
Hatua zilizidi kushuhudiwa! Walizidi kwenda tu pasipo kujali chochote! Walipiga mioyo konde kuwa liwalo na liwe!
“Nkalo.”
“Mmmh!”
“Nimekwambia lakini kuwa huku hakufai baki? Ukakata! Ona sasa.”
“Mulah nipo tayari kufa nikiwa nawe kuliko ufe uniache!”
“Alaaaa!! Hivi nyie kumbe ni wapenzi?”
Sango aliuliza kwa taharuki huku akiwageukia!
Yaani kilikuwa ni kitu cha kustaajabisha mwanaume kwenda na mke wake au mpenzi wake katika maeneo kama hayo! Kwani ni hatari.
“We twende bwana! Huyu hakutaka kunielewa tangu kule ukumbini sasa namuona sasa hivi anakunja ndita za uoga! Na bado lazima ajute kunifuata!”
Mulah alijibu.
Ni dhahili kabisa hakupendezewa na uwepo wa Nkalo katika safari hiyo.
Ila hakuwa na namna maana alikuwa wa kwanza hata kujitambulisha mbele ya ule umati mkubwa wa watu katika ukumbi wa mfalme wao siku ile wanaianza safari hiyo.
“Mulah leo wewe umekuwa wa kuniambia mimi kuwa nitajuta kukufuata?”
“Hebu wacha wivu wa kijinga, unakumbuka nilikwambiaje siku ile tukiwa pale kitini?”
“Eti uende mji wa wafu sasa ukifa huku je?”
“Kwahiyo wataka tufe wote?”
“Mara mia.”
“Mwehu kweli wewe!! Sasa tulia! Hahaha!! Unakwenda kukutana na mijitu meno puani…!!”
“Wee! Mulah acha bwana usimwogopeshe huyu atatuletea balaa.”
Sango aliamua ugomvi huo...
Kumbe katika safari hii ndani yake kuna wapendanao! Nao ni Nkalo na Mulah.
Inasadikika wakati wa mkutano Mulah alipojitoa mhanga kusafiri mji wa wafu ikiwa ni sehemu ya kuwaokoa wananchi wa Katesh katika balaa lililokuwa linatazamiwa kutokea pia akiwa na imani ya kurudi salama na kuwa Mfalme wa katesh, Nkalo alimpinga vikali ambapo Mulah aliamua kutoka kibabe!
Katika jambo lisililo la kawaida! Alishangaa na Nkalo akijitambulisha kuwa mmoja kati ya watu watakaosafiri kwenda katika mji huo wa siri.
Mulah alikosa pozi maana kama ni kumzuia alishashindwa kilichokuwa kimesalia ni kwenda nae tu!
Sasa ndiyo kama hivyo tena! Wamekaribia maeneo! Binti kaanza uoga!
Hahaha!!
Yajayo yanafurahisha!!

Siku ya 38, ikawa inaelekea ukingoni taratiiibu! Hali ya hewa ilianza kubadilika upyaa!
Baridi ya jioni kutokea anga la mashariki ilianza kuwapuliza watu hawa.
Hata ikabidi watafute sehemu ya kuweka kambi ili kuweza kupumzika na kuingoja siku ya pili yake.
Hawakupata tabu, katika kutafuta tafuta walipata kuona sehemu moja nzuri sana iliyokuwa chini ya jiwe kubwa!
Hiyo sehemu ilikuwa ni kama mfano wa pango hivi, lakini halikuwa pango kubwa saana!
Ilikuwa ni kama proti hivi iliyoweza kuwasitili vyema na baridi kali ya jioni katika eneo hilo.
Moto mkubwa wa magogo ulikokwa, chakula kikandaliwa wote kwa pamoja wakakila.
Sango alimshika mkono Mulah na kumvuta chemba kidogo.
“Ndugu yangu yaani mlichokifanya siyo kabisa!”
“Kipi hicho?”
“Haitakiwi kabisa kukanyaga ardhi ya mji wa wafu ukiwa na mpenzi wako!”
“Sasa mi nifanyaje ndugu yangu? Lijitu lenyewe king'ang'anizi kama kupe”
“Doooh! Huu ni mtihani sasa!”
“Wacha akafe hakuna namna.”
“Siyo yeye tu! Hata wewe pia!”
“Ee?”
“Sikia... Nijuavyo mimi katika huo mji hakuna mwanamke!
Pia nimesimuliwa kuwa hakuna mwanamke amewahi kwenda kule na kurudi akiwa hai.
Hivyo nilichokuwa nikikitarajia ni kwamba Nkalo angeuliwa punde tu utakapokanyaga mji wa wafu.
Sasa kama ni mpenzi wako basi mnakufa wote!”

“Wacha utani Sango!”
“Nakwambia mimi.. Fanya maarifa tumuache huku huyo dada atakuponza!”
“Daaah! Sijui kama atanielewa aisee!”
“Fanya hivyo.. Mkomalie vinginevyo kazi itatushinda nakwambia!”
Dooh!
Ulikuwa ni mkasa mpya kwa Mulah ilitakiwa afanye jambo akiweza amshawishi Nkalo aweze kubaki duniani ili wao waende katika mji huo na watakaporudi wampitie waondoke nae.

Sehemu 2 Sehemu 4
0
0