Mzimu Uliorudi Kulipiza Kisasi - Sehemu ya Pili (02) 
Mawazo mengi sanaa yaliyompata mlinzi wa geti Emanuel yalipelekea kusahau hata kunywa chai hiyo ambayo baada ya kuifuata na
kumkuta mwaandaaji akiwa katika hali ya majonzi.
Hata yeye hamu ya chai hakuwa nayo tena kwani alifika kibandani kwake na kuiweka chini kisha akajiinamia na kushika mashavu yake
jambo lililopelekea akili kuhama kabisa na kusahau kama alikuwa na chai hapo na baade kuja kushtua chai imeshapoa kama maji...
“Baby!!”
“Mmmh!!”
“Mimi leo nataka unipeleke Mtera.”
“Ukafanye nini uko tena?”
“Aaa! Baby mi nataka kwenda kula samaki jamani.”
“Khaaa!! Baby nae kwani mjini hapa si zimejaa tu?”
“Mimi leo nataka kufurahi kuona sehemu zinakovuliwa.”
“Sawa usiwaze wangu tutaenda kesho.”
“Babyyy!!! Jamani mi nataka leo kwani kesho hiyo unayosema wewe mimi nasafiri kuelekea Nyang'oro mama ni mgonjwa.”
“Aahaa! tena ndiyo itakuwa vizuri zaidi tunampitia hapo kisha tunapitiliza.”
“Sikia baby siku nzuri ni leo kwani leo yupo hospitalini Ipamba na na kesho analudi hivyo ni lazima niwahi na nikashinde kule hivyo
sitokuwa na muda tena….”
Ilikuwa ni katika nyumba moja maarufu sana ya kulala ijulikanayo kama PATRICK GEST HOUSE mwanadada ajulikanae kwa jina la Ashura.
Toto la kishua, toto la mjini, toto lililomchanganya Patrick mpaka kufikia kumsahau mkewe wa ndoa.
Ndiye aliekuwa akimpanga Patrick hapo.
Baada ya mwanadada huyo kum'bembeleza kwa muda mrefu sana hatimae Patrick alikubali siku hiyo wakalie starehe katika bwawa la Mtera
lililopo mpakani kati ya IRINGA Na DODOMA.
Tukija huku nyumbani sasa!! Ni shiiida aseee...
Saida nae aliacha kulia na kujiandaa haraka haraka kisha akachukua ufungungo wa gari yake na kutoka nje...
Kichwani alipania kumfuatilia mumewe kwa siri ili kubaini kisa na mkasa...
Baada ya kulia kwa mda mreefu sana mpaka macho kuwa mekundu Saida alipata wazo jipya kichwani ambalo yeye kwa upande
wake aliamini huenda likawa utatuzi katika ndani ya ndoa yake ambayo imeingia dosari na kumsababishia matatizo makubwa sana.
Saida hakutaka kulaza damu haraka akainuka na kuingia bafuni na kuoga haraka haraka na kurudi ndani.
Dakika tano zilimtosha mwanamama huyu kujiandaa.
Akachukua mkoba wake mdogo na kuweka simu yake ndani pamoja na kiasi kidogo cha pesa ambacho aliamini kingemsaidia kwa mchana wa
siku hiyo kwani hakuwa na tegemeo la kurudi nyumbani mchana.
Baada ya kujiridhisha na maandalizi hayo taratibu alijongea kabatini na kuchukua funguo za gari yake kisha akatoka mpaka sebleni.
“Nimesahau nini?”
Saida alijiuliza huku akiwa bado kasimama sebleni.
“Aahaa ok.”
Haraka akarudi ndani kana kwamba kuna kitu kasahau.
Kwa hatua za haraka akajongea mpaka chumbani moja kwa moja mpaka kabatini akafungua na kutoa bastola yake na kuikagua kama ina risasi ndani.
Alipojiridhisha akatoka na kufunga mlango.
Bila kupoteza muda akaenda moja kwa moja mpaka eneo la maegesho ya magari akatoa gari moja makini sana aina ya VX
Mayai na kusogea nayo mpaka getini.
“Pi..piiiiiiiiiiip!!!!!”
Sauti kali ya honi ya gari ilipenya vyema kabisa katika ngoma za masikio ya mlinzi wa geti hilo Emanuel.
Jambo lililomtoa katika dimbwi kubwa la mawazo.
Haraka akainua kichwa na kuchungulia katika kijidirisha kidogo kilicho katika kijibanda hicho ambacho humwezesha mlinzi
huyo kumwona aliyepo getini kabla ya kwenda kufungua.
Mlinzi alishituka kuona gari ya mke wa bosi wake.
“Anakwenda wapi huyu sasa hivi?”
Mlinzi alijiuliza pasipo kupata jibu.
“Pi.. Piiiiiiiiiiiph!!!!”
Honi ililudia tena.
“Nakuja nakuja dada yangu...”
“Wahi wahi.”
Mlinzi akatoka mbio mbio ila kabla ya kwenda kufungua alimwendea kwanza mke wa bosi wake huyo.
“Samhani dada yangu unakwenda wapi kwani?”
“Emanuel lini nawe umeanza maswali kama hayo?”
“Samhani kama nimekukwaza ila naona leo hauko sawa ndiyo maana nikauliza.”
“Hebu fungua geti huko!!”
Saida aliongea kwa hasira kidogo huku akipandisha kioo cha gari yake.
Mlinzi kuona hivyo hakuwa na jipya zaidi ya kufungua geti ili kuepuka longo longo maana huyu mwanamke leo hajatulia kabisaaa.
Taratibu Saida akakanyaga mafuta na gari kuanza kuondoka eneo hilo huku Emanuel akimsindikiza kwa jicho flani lenye mashaka.
Mwendo aliotoka nao saida ulitosha kabisa kumdhibitishia Emanuel kuwa mwanamama huyu hakuwa sawa kabisa kiakili.
Hivyo alianza kumuombea asije akapatwa na ajali maana siyo kwa spidi hiyo.
Baada ya kuona saida amepotelea Emanuel alifunga geti lake kisha akarudi kwenye kijibanda chake na kutulia tuli.
Huku mjini mambo yalikuwa yamepamba moto.
Mwanadada Ashura alikuwa amefanikiwa kumpanga Patrick na tayari walikuwa wamekubaliana kwenda kushinda bwawani Mtera siku hiyo.
Kwa upande wa Ashura ilikuwa ni furaha tele kwani hakuwa amewahi kukanyaga bwawani huko tangu azaliwe hivyo leo itakuwa mara yake ya kwanza.
Basi kwa pamoja walitoka hapo PATRICK GEST HOUSE Na kuelekea benk ili Patrick akatoe pesa itakayowasaidia katika safari hiyo.
Kutoka hapo walipo mpaka benki hapakuwa mbali hivyo haikuwapa shida kufika.
Walifanikiwa kufika benk Patrick akatoa kiasi cha shilingi milioni mbili za kitanzani kisha akazichimbia mfukoni.
Wakatoka hapo taratibu wakapitia katika pub moja na Patrick kupata moja moto ili kuzimua akili huku Ashura akipata pepsi bariidi.
Baada ya kutosheka wakatoka na kuingia garini na safari kuanza...!!
Lakini kabla hawajaenda mbali zaidi Patrick akakumbuka kitu.
“Hebu tupitie sheli nijaze mafuta maana hii barabara haina sheli tukitoka hapa mjini sioni sehemu ya kujaza mafuta.”
“Sawa fanya hivyo.”
Basi papo hapo wakakatiza na kuingia sheli ili gari ijazwe mafuta!
Hapo sheli walikutana na kijana mmoja wa kiarabu lakini ni muongeaji mzuri wa kiswahili.
“Habari kijana?”
“Salama karibu boss.”
“Ok hebu nijazie lita 30 hapo.”
“Sawa.”
“Itakuwa sh ngapi?”
“Elfu sitini tu boss.”
“Changamka basi.”
“Sawa sawa boss.”
Baada ya dakika kadhaa ilikuwa tayari.
Patrick alilipa kisha akapanda ndani ya gari na kumkuta Ashura akiwa anachati na smartphone yake kubwaaa!!
“Tayari?”
Ashura aliuliza...
“Ndiyo.”
“Sawa.”
Basi bila kupoteza muda gari iliondolewa hapo kwa mbwembwe nyiiingi, huku yule dogo wa kiarabu akimtizama jamaa anavyoondoka kwa mkwara mkali mpaka
kijana alicheka peke yake.
Patrick aliingia sasa na kuikamata vyema barabara kuu ya IRINGA to DODOMA.
Ikichangia na pombe ilishaanza kupanda kichwani aaaaaa!!!
Masikini Saida baada ya kutoka nyumbani akilini mwake aliwaza mumewe atakuwa katika nyumba yao moja ya kupangisha ambayo
ilikuwa katika ukarabati hata hivyo aliambulia patupu!!
Kwani baada ya kuwakuta mafundi walimwambia bosi wao huyo mara ya mwisho kwenda hapo ilikuwa ni juzi na alishawalipa na
kuwambia yeye ametingwa hivyo muda wa kwenda hapo mara kwa mara hana hivyo akaamua kuwalipa ujira wao na kuwaahidi kuwa angekuja
baada ya siku tatu muda ambao angehisi kazi itakuwa imekamilika.
Saida kusikia hivyo alichoka kwani mahali pa kumkuta Patrick kwa muda huo hakupajua.
Akili ikangukia alikumbuka wakati mwanaume huyo anaaga alisema anakwenda PATRICK HOTEL Hotel yao maarufu...
“Hebu nikajaribu kuangalia na kule.”
Saida baada ya kupata wazo hilo aliagana na mafundi hao na kuingia kwenye gari lake na kuondoka.
Saida aliipa gari mafuta kisawa sawa kuhakikisha anamuwahi Patrick katika hotel hiyo bila kujua mumewe huyo mda huo alikuwa safarini.
Saida alifika Sehemu ambapo ni kivuko na pia ndiyo kutaniko kati ya barabara kuu iendayo dodoma na njia za uchochoro.
Saida alilazimika kusimama ili kutizama kushoto na kulia kabla ya kuingia barabara kuu.
Sasa akiwa anatizama kushoto mara aliona gari ambayo bila shaka ilikuwa ni ya Patrick.
Saida alishituka na kushusha kioo ili kuona vizuri.
Macho hayakudanganya alichokiona ndicho kilichokuwa, gari ilikuwa ni ya mumewe na ilikuwa moto haijawahi tokea.
“Mungu wangu!!! Patrick anakwenda wapi na spidi hi?”
Saida alijiuliza maswali mengi bila kupata majibu, alichokifanya ni kupandisha kioo ili mumewe asimuone maana kama atapita
na spidi hiyo itakuwa ngumu kugundua kama gari hiyo ni ya mkewe.
Sekunde kumi..!!
Patrick alipita hapo Kama upepo.
Saida nae hakushangaa alitizama pande zote baada ya kuona hakuna gari nae akajitosa barabarani kumfukuzia Patrick...
Saida kumkamata Patrick lilikuwa ni jambo gumu sana kwani Patrick gari ilikuwa imechanganya kwa muda mrefu na hapo alikuwa
yupo spidi 200 sasa mpaka Saida aje afikishe spidi hiyo itakuwa ni shughuli kumkamata jamaa na ikichangia tayari
alikuwa amepiga moja moto duuh!!
Ebu tusikiliziee.....
Unaweza pia kusoma: