Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Mzimu Uliorudi Kulipiza Kisasi - Sehemu ya Tano (05)

“Hapana mkuu hii gari inaonekana ilikuwa inashuka bondeni sasa cha msingi tunatakiwa kuwahi Ndolela kwenye mzani ili tukapate orodha ya magari yote yaliyopita hapo kuanzia saa tatu zilizopita huenda tukapata information yoyote.”

Aliongea kijana mmoja wa kikosi hicho cha polisi wazo lililokubalika kwa asilimia mia na kikosi kizima.
Kwa kuwa mtu alikuwa kashatolewa ndani ya gari iliyokuwa imepata ajali polisi hawa hawakushughulika kuanza kuliinua gari hilo kwa mda huo, wao walichokihitaji kwa mda huo ni chanzo cha gari hiyo kupata ajali.
Basi askari wote walijazana ndani ya difenda zao na safari kuanza huku wakiwa wapo kasi baraa ili kujaribu kuokoa mda.
Baada ya kutembea takribani mda wa dakika ishirini na sekunde kadhaa waliweza kufika katika eneo la Nyang'oro ambapo sasa ndipo ilipotelekezwa scania hiyo.

“Oya!! oya!! Ebu simamisha kwanza gari.” Aliongea askari mmoja huku akiwa tayari kwa kuruka.
Dreva alisimamisha kisha askari wote kushuka na kulizingira gari hilo huku wakiwa makini kulikagua kila kona!
“Wanangu gari iliyomsabishia huyu mama ajali hii hapa.”
Aliongea polisi mmoja na polisi wote wakakusanyikia mahali alipokuwa kasimama polisi huyo.

Patrick tayari alishaukamata mlima wa Nyang'oro wenye kona kali baraa lakini hakuwa akijali hilo mwanaume alikuwa akilala nayo baraa!
Ashura yeye bwana alikuwa akiuchapa usingizi pasipokujua kuwa safari yao imeingia dosari.
Sasa kibaya zaidi ni kwamba hakuwa amefunga mkanda na gari iko moto siyo mchezo kitendo kilichopelekea kujigonga kwenye vioo afikapo konani.
Hali ilianza kuwa tete kwani kila dakika walizidi kuingia kwenye kona kali kiasi kwamba mzee mzima Patrick akilala nayo Ashura huhama mpaka siti na kwenda kumlalia jamaa.
Na akiigeuzia upande wa pili Ashura huhama kwa mara nyingine na kwenda kujigonga kwenye vioo jambo lililopelekea kuzinduka usingizini.
Alikutana na kivumbi cha mwaka halafu hakujua kama wapo wapi??

“Patrick mbona mwendo mkali hivyo?? Kwani bado mbali sana??”
“Kuna dharura imetokea mjini hivyo nahitajika mara moja.”
Patrick alijibu hivyo huku akibadili gia na gari kuzidi kwenda kwa kasi ya ajabu.
Ashura alibaki mdomo wazi asijue aongee nini na gari iko mafuta kweli.
Ashura alichokifanya ni kuvuta mkanda wa siti yake na kuuvaa kwa usalama wake maana si kwa mwendo huu ni shiida.
Mdau ukisikia neno AMBULACE ujue ni muunganiko wa vitu viwili hatari sanaa!
Kwanza madreva wa gari hizi wanakuwaga ni shiida halafu na gari zenyewe zinakuwaga siyo za mchezo mchezo.
Sasa AMBULACE ya kituo cha afya Ismani ni Rand rover zile za kijapan.
Unaambiwa ni shiida aiseee.
Ni ndani ya dakika 35 Tayari gari hii ya wagonjwa ilikuwa imetinga katika hospitali moja maarufu sana hapa mkoani Iringa ali maarufu kama IPAMBA.

Madaktari na manesi baada ya kusikia king'ora nje ya hospitali wakajua moja kwa moja kuna mtu yupo katika hali mbaya ya kukumbwa na mauti, hivyo kila mhudumu aliacha kile alikuwa anakifanya kwa mda huo na kukimbili nje kuona kupo vipi.
Kitanda cha matairi kilitolewa na kusukumwa mpaka karibu na gari hiyo.
Saida alitolewa.
Aisee unaambiwa kwa hali aliyokuwa nayo madaktari walianza kukataa tamaa.

"Sasa mnatuletea mtu keshakufa wa kazi gani???”
Daktari mmoja alimuuliza yule dreva wa AMBULACE iliyomleta Saida.
“Samahani daktari mimi nimeagizwa na mkuu wa kituo cha polisi Ismani nimlete huyo mtu.”
Dreva nae alijitetea.
“Ebu mpelekeni chumba cha upasuaji haraka sana.”
Daktari huyo aliamuru hivyo baada ya kujua kuwa mtu huyo yupo chini ya serikali.

Saida alipelekwa moja kwa moja katika chumba cha upasuaji huku pilika pilika zikianza.
Kitu cha kwanza ilikuwa ni kukagua mapigo ya moyo kama yanasikika au laa.
Daktari mmoja nguli sana alikuja na kifaa chake cha kusikilizia mapigo ya moyo ili aweze kubaini i wapo mtu huyo ni mzimaa au apelekwe mochwari.
Taratibu akaweka kifaa chake kifuani mwa Saida upande wa kushoto kisha akaanza kusikiliza kwa umakini daktari huyo alisikilizia zaidi ya dakika tano pasipo kutoa majibu yoyote hali iliyozua wasi wasi mkubwa kwa baadhi ya mdaktari waliokuwa hapo.

Huku Nyang'oro tayari polisi walishalipata gari ambalo wao wanaamini kuwa ndiyo lilimsababishia Saida ajali ile mbaya na ya kutisha.
Basi msako mkali wa kuwasaka dreva na konda wake waje kujibia na kutoa maelezo jinsi ajali hiyo ilivyotokea.
Msako ulikuwa ni mkali saana, unaambiwa ilikuwa ni nyumba kwa nyumba, Chumba kwa chumba, Kitanda kwa kitanda lakini msako huo haukuwa na maana yoyote wala faida yoyote kwani waendeshaji wa gari hilo walishatembea kitambo sana.
Walishalitambua hilo na wakayeya kabla ishu haijabuma.

Polisi walikuwa wameweka msako makini sana wakijua kuwa waendeshaji wa gari hilo huenda wapo katika migahawa ya hapo Nyang'oro hivyo msako mkali uliendelea huku gari hilo likiwa chini ya ulinzi mkali.
Baada ya msako wa muda mrefu na bila mafanikio waliamua kurudi ilipo scania hiyo ili kukaa pamoja kujua nini wafanye.
“Nani ana wazo?”
Mkuu wao aliuliza.
“Hapa kamanda nadhani tupekue gari huenda tukapata hata docment zozote ambazo huenda zikawa na picha za dreva huyo.”
Wazo hilo liliungwa mkono kwa asilimia zote, basi bila kupoteza muda wakaingia ndani ya gari na kuanza kulikagua kila kona kuanzia chini ya siti na sehemu zote walizohisi huenda wakaona karatasi yoyote lakini waliambulia patupu.
Kwani watu hao waliondoka na kila kitu waliacha funguo za gari tu.
Askari walikata tamaa.

“Oya! Oya! Tusihangaike saana kumbe hii gari imefungwa camera ya CCTV mbele.
Hapa cha msingi ni kumtafuta bosi wa gari hili atupatie laptop iliyounganishwa na camera hii tutapata kuona kila kitu!”
Aliongea polisi mmoja huku akiitizama camera ile iliyofungwa kwa ustadi wa hali ya juu mbele ya kioo.
Askari wote walifurahi kuona uchunguzi wao unakwenda kuzaa matunda.

Patrick huku akiwa moto kama ilivyo kawaida yake na safari hii alionekana kuchafukwa siyo kawaida kwani mwendo aliokuwa nao ni mara dufu ya ule unaotumika katika mashindano ya magari.
Ashura alishindwa kuvumilia kabisa mwendo ule, tumbo lilianza kuvuruga vibaya mnoo na hatimae alianza kutapika hovyo.
Gafla bin vuuuh!!
Wanafika katika eneo alipopatia ajali Saida.
Patrick alipunguza mwendo aone ni nini tena.
Sasa kutizama vizuri haaaaaa!!!!!
Patrick hakuamini macho yake alihisi huenda yupo katika ndoto moja ya kutisha saana!
Siyo kwa vile Saida kapata ajali au kafa au nini??
Kilichomuuma Patrick kwa mda huo ni gari hiyo aliyoinunua kwa bei ghari halafu cha kushangaza hata mwezi haijamaliza kiasi kwamba hata kutengeneza sidhani kama itawezekana!!

Patrick alijawa na hasira ya gafla gafla na moyo kuanza kumwendea kasi huku akihisi kama moyo ukitaka kusimama.
Pumzi zilianza kukata kata jambo lililopelekea Patrick kuanza kupumua kwa nguvu huku pumzi zake zikitoa vijimlio flani hivi.
Wakati yote hayo yakitendeka Ashura mtoto wa kishua toto lililomzuzua kijana Patrick yeye alikuwa kaduwaa tu asijue afanye nini.
Patrick alivua mkanda wake kisha akateremka garini na kusogea mpaka sehemu gari hiyo ilipo. Kisha akaitizama kwa mda wa dakika tatu huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga lenga.

“Weweee!! Saidaaa!! Upo wapi?? We malaya umeua gari yangu!! Ulikuwa unakwenda wapi we mwanamke??? Nauliza upo wapi????”
Patrick alianza kupayuka peke yake kama mwenda wazimu.
Mwanaume gari imemuuma kweli kweli baada ya kuona hakuna chochote moja kwa moja akatambua kuwa Saida katolewa hapo.
Nae akarudi mpaka kwenye gari na kuwasha na kuingiza gia kisha huyoo akachomoka hapo kama mzimu.

Uamuzi ambao polisi walikuwa wameafiki mpaka hapo ilikuwa ni kumtafuta bosi wa roli hili la mizigo ili waweze kupatiwa laptop iliyounganishwa na camera hii ndogo iliyofungwa mbele ya kioo ambayo kazi yake ni kurekodi safari nzima.
Polisi waliamini ya kwamba uchunguzi wao unakwenda kukamilika na huenda ikawa rahisi hata kumkamata dreva wa roli hilo kwani ni lazima bosi wake akawa na pasport za dreva huyo hivyo ni lazima atawapatia.

“Kijana wazo lako zuri tunatakiwa kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo..”
“Asante mkuu.”
Yalikuwa ni maongezi kati ya mkuu wa kituo cha polisi pamoja na mmoja kati ya vijana wake.
Basi mkuu huyo akatoa simu yake kubwa ya mkonga kisha akaipiga na kuiweka sikioni.
Hatimae ilianza kuita na baada ya sekunde kadhaa ilipokelewa.
“Haloo mkuu.”
“Wapi sajent?”
“Tupo Mtera bwawani.”
“Mnafanya nini huko??”
“Tulipata simu ya dharura kuwa kuna uvuvi haramu umefanyika.”
“Vipi mmewatia mbaroni wahusika??”
“Ndiyo tupo nao hapa.”
“Kazi nzuri vijana wangu basi hakikisheni mnawaleta huku pamoja na samaki hao.”
“Sawa sawa.”
“Ni tenga ngapi??”
“Ni tenga thelathini mkuu.”
“Duuuh!! Waleteni haraka sana.”
“Nimekupata mkuu.”
Simu zikakatwa huku mkuu huyu akiwageukia vijana wake hao alionao hapo.
“Hili ni tatizo kubwa vijana wengi wapo mtera je? tufanyaje??”
Mkuu huyu wa polisi aliuliza huku akitafakari na kusubili mchango kutoka kwa vijana wake.
Kijana yule yule akapata wazo tena!!

Sehemu 4 Sehemu 6
0
0