Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Mzimu Uliorudi Kulipiza Kisasi - Sehemu ya Nne (04)

Mwanaume Patrick yeye alikuwa ni mzoefu sana wa kuendesha gari na barabara hiyo anaijua mwanzo mwisho hivyo kona hizo kwake ilikuwa ni burudani tuu.
Tayari walishaumaliza mlima hatari wa Nyang'oro ambao ni tishio kubwa kwa madreva wote wanaotumia barabara hiyo.
Patrick na mchepuko wake tiari walishatinga Migori, inamaana wakitoka hapo basi ni Mtera moja hiyo.
Basi walipumzika kidogo pale Migori na kupata vinywaji ili kuipa nguvu miili kwaajili ya kujiaanda na safari upya.

“Sasa ngoja nifanye mpango tuoge kabisa au??”
Patrick aliongea.
“Sawa fanya hivyo.”
Patrick kusikia hivyo akachangamka mpaka wakapata bafu ambalo ni spesho kwa wasafiri hasa abiria.
Baada ya dakika kadhaa walikuwa wameshaoga tayari walitoka na Patrick akalipia na taratibu wakaanza kuondoka kuelekea kwenye gari, lakini Patrick akaona ngoja kwanza.

“Ashuu tangulia kwenye gari nitakukuta huko.”
“We unaenda wapi tena?”
“Nakuja sasa hivi.”
“Sawa.”
Ashura hakuwa na kipingamizi alitangulia zake kwenye gari na kama kawaida yake akaendelea kuburudika na mziki mnene.

Huku nyuma Patrick akaenda moja kwa moja mpaka kwenye kijipub kimoja hivi.
Nahisi aliona kichwa kinaanza kuwa kizito.
Bila kupoteza muda akaagiza CASTLE mbili na kuanza kuzibwia kwa fujo kweli kweli.
Wahudumu waliokuwa mule ndani walianza kumchanganya jamaa hasa ikichangia na uvaaji wa wahudumu wa baa duu.
Patrick alijiapiza kuwa ipo siku atakuja kuwazoa wotee!!
Aliwaza hivyo huku akiinyonya chupa ya mwisho mfululizo mpaka inaisha.
Hakika mpaka wahudumu walishangaa.
Kwa kuwa Patrick alikuwa na mtu anae msubili garini kule hakuwa na muda wa kupoteza hapo zaidi ya kulipa pesa ya bia alizokunywa na kuanza kuondoka.

“Kaka mbona hujachukua chenchi??”
Mhudumu aliuliza baada ya kuona Patrick katoa hela ya chenchi ila anaanza kuondoka pasipo kuichukua.
“Iyo baki nayo tu!!”
Patrick aliongea huku akitokomea nje!

Alikwenda mpaka kwenye gari ambapo alimkuta Ashura akiwa kakaa kihasara hasara hukua akiwa kalala fofofo.
Patrick hakushughulika nae alimwacha aendelee kuuchapa usingizi hapo, yeye akavuta mkanda wa gari na kuuvaa akachukua funguo na kuichomeka kisha akawasha gari.
Ila kabla hajaiondoa akakumbuka kitu.
Haraka akachukua simu yake na kuanza kuitafuta namba ya moja kati ya wafanyakazi wake wa ujenzi maana alikumbuka kuna aliyempigia ila hakupokea.
Aliiona kisha akapiga na sekunde chache simu ilianza kuita.

“Ngrrr!!! Ngrrr!! Ngrr....”
“Naam boss!!”
“Kuna muda niliona ukinitafuta vipi? Nilikuwa nimetingwa kidogo.”
“Mke wako mmeonana??”
“Wapi? Saa ngapi?”
“Mida kama ya saa mbili hivi alikuwa anakuulizia sana mpaka hapa amepita.”
Patrick kusikia hivyo roho ikapiga paah!!
“Sasa ameelekea wapi??”
“Alisema atakwenda kukuangalia PATRICK HOTEL nami nikaona ngoja nikushitue ili kama haupo hapo uende mkutane.”
“Ahaaa asante kwa taarifa.”
“Sawa boss kazi njema.”
“Kazi njema pia.”
“Asante.”

Simu zikakatwa kisha muda huo huo patrick akaitafuta namba ya mlinzi wake wa geti bwana Emmanuel, simu iliita mara mbili ikapokelewa.

“Boss!”
“Naam kaka upo hapo nyumbani?”
“Ndiyo boss wangu.”
“Shemeji yako yupo karibu hapo?”
“Hapana boss kaondoka tangu mda ule ule.”
“Alaaaa!! Hajakwambia wapi anaelekea??”
“Hapana boss ila alipokuwa anatoka alionekana kuwa na hasira sana."
“Duuuh!! Sawa atakaporudi nijulishe.”
“Hakuna shaka.”

Simu zikakatwa huku Patrick akiwa na maswali lukuki kichwani kwake.
“Huyu mwehu kaenda wapi???”
Patrick alijiuliza huku akianza kuitafuta namba ya Saida haikuwa kazi ngumu aliipata kisha upesi akaitwanga.
“Namba unayoipigia haipatikani kwa sasa tadhari jaribu tena baadae......”
Hilo ndiyo jibu alilokutana nalo bwana Patrick alipojaribu kumpigia mkewe Saida.
Patrick akavuta pumzi ndefu na kuishusha huku mapigo ya moyo yakianza kumwendea kasi baraa!
“Daaah!! Kama atabuni akili ya kwenda Sumbawanga nimekwisha mie kwani mashart yote anayo yeye mwenyewe.”
Patrick aliwaza hivyo huku akipiga hesabu ya haraka afanye nini.
Hapana ngoja nimwahi huyu mwanamke atakuwa kaondoka kihasira hasira na anakwenda Sumbawanga kuharibu kila kitu na jina la Patrick linakwenda kufa.

Basi bila kupoteza mda Patrick aligeuza gari kwa Kasi ya ajabu kuanza kurudi walikotoka.
Lengo lake ni kumwahi Saida iwapo amepanga kwenda kuharibu siri nyeti ambayo wanaijua wao wenyewe.

Tukija huku kwa mwanamama Saida ni kwamba baada ya kupata ajali ile ya kutisha alizima kabisaa.
Haikupita muda mreefu tangu ile scania aliyokumbana nayo kuondoka.
Kuna gari ndogo ambayo ndani alikuwepo mmama mmoja wa makamo kidogo mwana mama huyu ni mfanyabiashara hivyo alikuwa akitokea Dodoma kurudi kwao Mbeya.
Sasa baada ya kufika eneo hilo la ajari aliona gari ndogo ikiwa imeharibiwa siyo kawaida.
“Hee yupo hai kweli???”
Alijiiuliza mwanamke huyo huku akitoa simu yake ya mfukoni kisha akaanza kutafuta namba za simu za police kituo cha Ismani.
Haikuwa kazi ngumu alifanikiwa kuiona na bila kupoteza akapiga.
Simu ilita mara mbili ikapokelewa.

“Unaongea na mkuu wa police kituo cha Ismani karibu.”
“Naitwa Anjerina Mwasy natokea Dodoma ila njiani nimekutana na Ajali.”
“Nini?”
“Ajali mbaya Sana.”
“Iyo ajali imehusisha gari gani?”
“Ni VX.”
“Sawa tunakuja.”
Basi simu zilikatwa huku mwanamama huyu akiteremka kutoka katika gari yake ili aweze kukagua vizuri.

Baada ya kushuka alikutana na michirizi mingi ya damu ikitokea ndani ya gari hiyo kwenda chini.
Mwanamama huyo aliendelea kukagua kagua mara akaiona sura ya kike ndani.
“Toobaaa!! Ni mwanamke?? Halafu keshakufa yule.”
Alikuwa akiongea peke yake mwanamama huyo huku machozi yakimtoka kwa kasi baada kugundua aliepatwa na ajali hiyo ni mwanamke.
Dakika kumi na tano mbele ving'ora vya magari ya police pamoja na gari ya wagonjwa (AMBULANCE) kutoka katika kituo cha afya Ismani viliskika vikikaribia eneo hilo.
Mwanamama huyo alikwenda kupanda katika gari yake na kukaa kimyaa.
Mara gari ya kwanza ya polisi iliwasili hapo huku ikiwa spidi baraa ikifuatiwa na AMBULANCE ya wagonjwa kutoka kituo cha afya Ismani.
Baada ya dreva aliyekuwa akiiedesha gari hii ya police iliyokuwa mbele kuona ameshafika katika eneo la ajari aliwasha taa za tahadhari kuwaarifu walioko nyuma kuwa wameshafika.

Bila kupoteza muda police walisimamisha magari yao na kuweka vibao vya tahadhari kila upande wakati huo wengine wakiwa wanashughulika kutoa mwili wa Saida ambao ulikuwa katika hali mbaya.
Dakika tano ziliwatosha kuhakikisha mwathilika huyu wa ajali ameshatolewa katika gari yake.
Ebwana eeee!!
Huangalii mara mbili kwa jinsi Saida alivyokuwa amechakaa.
Yaani ilikuwa ni baraa na haijabainika kama ni mzima au amekufa, police walisaidiana kum'beba na kumpakia katika gari ya wagonjwa kisha gari hiyo ikawashwa tayari kwa kuondoka.
“Mfikishe Ipamba haraka!!”
“Sawa mkuu.”

Mkuu wa polisi alimwagiza dreva wa AMBULANCE hiyo kumfikisha mgonjwa huyo katika hospital ya Ipamba kwani mgonjwa yupo katika hali mbaya kiasi kwamba hata polisi wameshindwa kutambua kama ni mzima au kafa?
Dreva alikubaliana na mkuu wa polisi na bila kupoteza muda gari ikaondolewa kwa kasi hapo kama upepo.
Saida alikuwa katika hali mbaya sana kiasi kwamba hata polisi walishindwa kubaini kama kafa au yu hai.
Hivyo walichoamua ni kwamba majeruhi huyu awahishwe katika hosptali ya Ipamba.

Basi yule dreva wa gari ya wagonjwa iliyokodiwa kutoka katika kituo cha afya cha Ismani aliambiwa amwahishe Ipamba mara moja.
Bila kupoteza muda AMBULANCE iliondolewa kwa kasi kama upepo eneo hilo.
Polisi nao walianza kuchunguza eneo la ajali ili kubaini hii ajali imesababishwa na nini.
Hata hivyo ilikuwa ngumu kidogo kwani hakuna breki yoyote iliyopigwa kabla ya gari hiyo kupata ajali.
“Hii ajali tumeshindwa kugundua chanzo yaani ili mradi tu tunaona gari iko msingini ila chanzo tumeshindwa kubaini.”
Kamanda wa polisi kituo cha Ismani aliongea.

Sehemu 3 Sehemu 5
0
0