Mzimu Uliorudi Kulipiza Kisasi - Sehemu ya Tatu (03) 
“Baby…”
“Mmh!!”
“Ujue mi leo ndiyo mara yangu ya kwanza kwenda kuliona bwawa la Mtera?”
“Khaaah!! Mwongo wangu.”
“Hakika sijawahi kuliona nalisikiaga tu.”
“Sasa unakwenda kuliona.”
“Nashukuru sana mpenzi nakupendaa.”
“Asante nakupenda pia Ashuu…”
“Kweli Patrick?”
“Na ndiyo maana nafanya yote haya kwaajili yako.”
“Nashukuru sana kusikia hivyo.”
“Usijali wangu.”
Yalikuwa ni maongezi kati ya Patrick na mchepuko wake huyo ajulikanae kwa jina la Ashura.
Wakati huo gari imeikamata tambarale ya Nduli.
Yaani unaambiwa huyu mwehu anatembeza gari utazani yupo katika mashindano ya magari.
Lakini gafla wakapigwa mkono na traffic ( askari wa usalama barabrani ).
Kitendo kile kilimchukiza sana Patrick kwani aliona anacheleweshwa kwenda kula starehe na mtoto wa kishua huko aendako.
Patrick alianza kupangua gia taratiibu hatimae akasimamisha gari yake kisha akateremka na kuwaendea matrafic hao.
Wakati huo Ashura akabaki garini akiwa anakula burudani nene ya muziki kupitia earphone zilizounganishwa na simu ya bei kaliii aliyohongwa na Patrick.
“Ndiyo mwendo gani huu?”
Trafic alimuuliza Patrick huku akiwa kakunja uso.
“Mnisamehe wakubwa natakiwa kuwahi Dodoma mara moja kuna mgonjwa yupo katika hali mbaya.”
Patrick alidanganya hivyo.
“Hata kama hili siyo eneo la kutembelea spidi hiyo...”
“Lakini si nimekwambia nina matatizo?”
“Unasikia wewe? Mimi matatizo yako siyajui bali nalinda usalama wa barabara na watumiaji wengine sawa? Paki pale...!!”
“Sikia kaka…”
“Usinizingue kibao kileee kinakwambia pita eneo hili na spidi 50, wewe iweje uje na 200?”
Patrick akaona bila kutumia akili ya ziada atakesha pale hivyo alichokifanya ni kuingiza mkono mfukoni na kutoa waleti yake,
kisha akavuta laki tatu na kuwagaia trafic hao ili kuwazima.
“Sikieni kaka zangu najua sheria zote za barabara ila nimetenda kosa hili kutokana tatizo kubwa nililonalo,
naomba mpokee hiki kiasi cha pesa kama adhabu yangu.”
Patrick aliongea hivyo huku akiwakabidhi trafic hao kibunda chenye pesa takribani laki tatu.
Mbele ya pesa hakuna sheria tena, trafic walizipokea pesa hizo kisha Patrick akaruhusiwa.
“Basi tunakutakia safari njema.”
“Nanyi kazi njema waheshimiwa.”
Baada ya maagano hayo Patrick aliludi haraka garini na kuiwasha wakati huo Ashura anaburudika tu na muziki kupitia earphone zilizoziba masikio yake hana habari.
“Mmemalizana?”
Ashura aliuliza.
“Aaah wana njaa tu hao walikuwa wanataka hela.”
“Sasa hawajakupiga hela ndefu?”
“Ya kawaida tu.”
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Patrick na mchepuko wake huyo Ashura, wakati huo gari inasoma namba tatu tayari imeshaanza kupaa!!!
Maskini Saida kumbe alikuwa ameshaachwa kilometa nyiingi mnoo japo Patrick kasimamishwa takribani dakika tano lakini mpaka anaondoka hapo
Saida hakuwa amefika bado lakini kwa muda huu hakuwa mbali.
Trafic nao baada ya kupokea pesa ile walijisahau na kwenda kukaa kando kabisa na barabara na kuanza kupiga stori.
Saida nae gari ilikuwa imekubali kisawa sawa trafic wakiwa hawana hili wala lile walishtukia gari ikipita kama kimbunga cha Haiti.
Unaambiwa kwa spidi aliyopita nayo ilikuwa ni baraa tupu.
Trafic wenyewe walishindwa cha kufanya wakabaki kutizamana tu, wakati huo gari ya Saida ishapotea muda mreefu.
Kutokana na Patrick kusimama kwanza na gia zote kupanguliwa hii ilipelekea Saida kuwaona kwa mbali kwani yeye hakusimamishwa na trafic.
Hata hivyo pia ilikuwa ngumu kumkamata Patrick kwani tayari gari ilianza kwenda kwa kasi baada ya gia zote kupangwa kama awali na spidi kuludi palepale.
Hatimae msafara huu wa mwendo kasi ulifika katika makona ya Nyang'oro.
Hii sehemu ni hatari sana nadhani kwa wale ambao mmewahi kusafiri kati ya Iringa, Dodoma au kutoka mikoa ya kusini kwenda mikoa ya kaskazini mwa
Tanzania kupitia Dodoma mnaijua vyema hii sehemu ni sehemu moja mbaya sana.
Kwani ina kona nyingi na kali hatari pia kuna majabali ya mawe pamoja na mabonde ya kufa mtu.
Kiujumla hili eneo ni hatari kwani barabara imepita mlimani.
Sasa msafara ulikuwa umetinga katika maeneo haya.
Saida alikuwa kaachwa tena kwa mara nyingine, na mara ya mwisho Saida kuiona gari ya Patrick ni katika kijiji kimoja kijulikanacho
kwa jina la Kibaoni.
Hiki ndicho cha mwisho ukitoka hapo unaingia makonani na hakuna tena makazi ya watu hii ni pori kwa pori, kona kwa kona,
majabali kwa majabali, mabonde kwa mabonde mpaka unamaliza mlima huu wenye urefu wa kilometa takriban 40.
Sasa Saida kwa mara ya mwisho kuiona gari ya Patrick ni katika kijiji hicho cha Kibaoni na baada ya hapo gari hiyo
ikapotea katika upeo wa macho ya Saida.
Saida alijua moja kwa moja Patrick kashuka bondeni je anakwenda wapi? Dodoma au?
Saida alijiuliza bila kupata jibu sahihi.
Na bila kupoteza muda nae akajitosa makonani, hakutaka kukata tamaa kabisa alitaka mpaka aone mwisho wa safari ya Patrick.
Saida alizidi kuipa gari mafuta pasipo kujua mbele ni hatari yeye hakujali hilo mawazo yake yalikuwa kwa Patrick tu.
Tayari alishaingia mlimani sasa alianza kukumbana na kona za ajabu.
Na kila anavyozidi kwenda kona kali zinazidi kujipanga mbele nae hakutaka kupunguza
mwendo kwa kuhofia huenda akachelewa sana mpango wake kuingia dosari.
Hivyo aliendelea kwenda hivyo kwa mwendo wa kasi pasi na kujali kama anaweza kupata madhara mbeleni.
Na kibaya zaidi ni kwamba siyo mzoefu wa kuendesha magari katika barabara yenye kona kali kama hii huwezi amini gari
ilianza kumsumbua mwanamama huyu alijitahidi sana lakini mbeleni gafla akakukana na kona tatu dabo na kali baraa…
Ya kwanza alifauru, ya pili alibahatishia, eebwana! ee!! Ya tatu ikawa kimbembe kwake kwani gari ilitaka
kupitikiza haraka akaiwahi na kuirudisha kwa nguvu.
Jambo lililopelekea gari kupoteza mwelekeo kabisa kwani ilirudi kwa kasi na kuhama saiti na kibaya zaidi ni kona.
Saida akiwa bado kashikwa na bumbuazi mara ikatokea scania ikiwa na doble tela!!
Tena kibaya zaidi alikuwa katikati ya saiti ya semi hilo.
Nae dreva wa lori hilo alijua kabisa kigari hicho kimepoteza mwelekeo hivyo balaa ni muda wowote.
Dreva wa lori alijaribu kulikwepeshea lori lake saiti ya pili ili kunusuru asigongane.
Hata hivyo ilikuwa ni kazi bure tu kwani gari hii ya Saida ilikuwa spidi hatari, kabla lile lori halijaihama saiti hiyo kishindo kikubwa kiliskika nyuma.
Gari Saida ilikwenda moja kwa moja na kujigonga katika tairi za nyuma za gari hilo la mizigo.
Gari ya Saida ilirushwa mbaaali huko na kwenda kujigonga kwenye majabali yaliyomo pembezoni mwa barabara.
Kitendo kilichopelekea gari ya Saida kubondeka bondeka siyo kawaida.
Dreva wa scania alijitahidi sana kumkwepa mwanamama huyu ila tatizo ni kwamba gari yenyewe ni ndefu sana.
Kwa mbele alifanikiwa kumkwepa ila kutokana na mwendo mkali aliokuwa nao Saida ulipelekea aende kuvaa nyuma kunako matairi jambo
lililopelekea gari ya Saida kurushwa na kwenda kutua katika majabali ya mawe yaliyopo pembezoni mwa barabara hii.
Unaambiwa gari ilibondeka siyo kawaida...
Yote hayo konda wa roli hili aliyashuhudia moja kwa moja bila chenga kupitia kioo cha pembeni yaani (Site mirror)
“Tumeua!!”
Kondakta aliongea kwa wasiwasi huku akimtizama dreva usoni.
“Hebu ichungulie imeingia uvunguni???”
Yule konda akatoa kichwa na kutizama nyuma.
“Oya tusepe msala huu.”
“Amekufa???”
“Jibu ni hilo.”
Yule dreva alichanganyikiwa balaa.
“Sasa yupo uvunguni ama??”
“Hapana katua pembeni.”
Huyu dreva kusikia hivyo akaiondoa gari haraka na hawakuthubutu kusimama ili kuona mtu huyo yupo katika hali gani?
Wao walichojua ni kwamba mtu huyo hayupo hai kutokana na jinsi gari ilivyo haribiwa.
Njiani walianza kushauriana kuwa nini wafanye ili kuepukana na msala huu kwani ni rahisi sana kugundulika.
Pale ilipojigonga gari ya Saida na wakigundulika na police itakuwa habari nyingine tena hakutakuwa na maelewano zaidi ya kuwekwa ndani.
Hii semi ilikuwa ikitoka Mwanza kuelekea Songea na ilikuwa imebeba magunia ya dagaa.
Baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya konda na dreva wake walifikia uamuzi wa kuitelekeza gari hiyo kabla ya taarifa
za ajali hiyo kusambaa na ikagundulika kuwa nao walichangia.
Hivyo basi baada ya vijana hao kufika karibu na Nyang'oro walipaki gari hiyo ya mizigo pembezoni mwa barabara na wao
kushuka kisha wakaitelekeza hapo na kukimbia.
Yaanii kibarua kwao kikawa kimeota nyasi.
Unaweza pia kusoma: