Hello! Karibu HASCAVELA

Muonekano wa Giza:

Msaada

Unseen - Episode 05

Nilitafuta ndizi mzuzu mbichi nzuri nikanunua nyanya na baadhi ya vitu vingine nilivyokuwa nikivihitaji na kisha kurejea nyumbani.
Nilizikaanga zile ndizi na ndani ya lisaa lizima nilikuwa nimeshamaliza hadi kukata kachumbari nikaweka mezani.
Nikachemsha chai na kisha kuiweka mezani.
“Tessa umeoga?”
Nilimuuliza.
“Nimeoga saa ngapi sasa?”
“Basi kaoge chakula tayari.”
Alienda kuoga huku akivaa baadhi ya nguo zake ambazo nilikuwa nazo hapo nyumbani.
Na mara baada ya kumaliza kuvaa alitoka na kuingia sebuleni.
Nilinyanyuka na kisha kuelekea bafuni na mimi kwaajili ya kuoga.
Nilitumia muda mrefu sana kuoga huku nikifikiria hili na lile.
Nilipomaliza nilirejea na kuvaa kiuvivu na kisha kuelekea sebuleni kuungana na Tessa kwa ajili ya kifungua kinywa cha asubuhi.
Nilimkuta Tessa akikodolea macho hotpot lililokuwa na chakula huku chai ambayo alikuwa amemimina ikiwa imeshapoa.
“Tessa mbona huli?”
Alibaki akiniangalia.
“Kwahiyo wewe unaona chakula cha kunipikia ndiyo hiki?”
“Aanh!! Tessa nimekosa chakula ndiyo maaana nimeamua kupika hivyo kwani ni kibaya? Sijakipika vizuri?”
Nilisogea na kisha kuchukua pande moja la nyama na kuliingiza mdomoni.
Niliambulia kofi kali lililotua kwenye mgongo wangu.
“Fyuuu….. Mshenzi wewe.”
Alinitukana na kisha kunyanyuka.
Aliondoka na kuingia chumbani na kuvaa nguo zake ambazo alikuja nazo siku ya jana.
Alikuja mpaka sebuleni.
“Naondoka.”
Tessa wala hakutaka kunisikiliza aliondoka.
Na alipofika nje nilisikia tena akizozana na wale watu.
“Mnanishangaashangaa hamnijui? Si mfanye mambo yenu.”
Na baada ya hapo nilisikia kimya.

Baada ya dakika tatu kupita mlango wa chumba changu uligongwa.
“Kaka Robert kwani kuna tatizo?”
“Hapana, hamna tatizo lolote.”
Aliingia mbinti mmoja wa mama mwenye nyumba ambaye bila shaka alikuwa ni binti wa mwisho umri wake ulikuwa ni takribani miaka ishirini na nne.
Alikuwa mpole sana kuliko mabinti wote.
Alikaa hapo sebuleni.
“Kwani huyu msichana ana matatizo gani?”
Nilivuta pumzi na kushusha.
Ingawa sikuwa nikimuamini lakini hata hivyo nafsi yangu ilinituma kumuambia.
“Huyu mimi ni mpenzi wangu.”
“Mna ugomvi wowote?”
“Hapana.”
“Mimi sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza tu kuwa na akili za hivyo bila kuwa na tatizo lolote, usikute kuna kitu unakifanya hakipendi.”
“Sikia nikuambie Diana, mimi namfanyia huyu mwanamke kila kitu ambacho napaswa kumfanyia na vingine vya kuzidi yani mpaka marafiki zangu wananiona mimi mume bwege lakini yeye hajali.
Just imagine anaamka anadai chakula nimempikia vyakula vizuri mimi mwenyewe sipikagi hivi halafu ananiambia hiki ndiyo chakula cha kumpikia anakasirika anaondoka.
Hivi mimi nimfanyie nini? Mimi ndiyo nakosea lakini sijui.”

“Kiukweli sina historia ya mahusiano yenu, lazima kuna kitu unafanya ambacho hakiko sawa au hata kama siyo wewe basi ni mtu mwingine atakuwa anafanya. Sijui labda kuna shida lakini hawezi tu kuwa hivi bila sababu yoyote ile.”
“Haaa…”
Nilivuta pumzi na kuzishusha.
“Sijui kwakweli. Labda nikukutanishe naye.”
Niliijiwa na wazo la ghafla.
“Labda, ujue nimeshawahi kuishi na watu wa namna hiyo.”
Hapo niligeuka na kumuangalia.
Hakuonekana kama wenzie hii ilionesha kati ya watoto wote wa mama mwenye nyumba peke yake alikuwa amesoma na siyo kwa level ndogo tu alionekana amesoma kwa level kubwa sana.
“Ok anyway niwakutanishe kwa namna gani?”
“Mwambie kuna msichana hapa nyumbani amempenda anataka muwe marafiki.”
“Basi sawa.”
Nilinyanyua simu yangu na kupiga haikupokelewa hadi nilipopiga mara nne.
Diana alikuwa akinitia moyo niendelee kupiga tu ingawa nilishaingiwa na hasira kwanini simu yangu haipokelewi.
“Unasemaje?”
Ndiyo neno alilolisema Tessa mara baada ya kupokea ile simu wakati nilikuwa nimeweka katika mfumo wa sauti mvumo.
“Tessa kuna msichana hapa tunakaa naye.”
“Kafanyeje?”
“Sasa si usubiri nimalize kuongea.”
“Eenhe endelea.”
“Kuna msichana hapa ni mtoto wa mama mwenye nyumba amekupenda anaomba muwe marafiki.”
Nilisema kwa sauti ya upole.
“Mwambie sitaki.”
“Daah Tessa…”
Niliongea kwa kukata tamaa.
“Hivi wewe mwanaume mbona unapenda sana kujipendekeza.”
Alinishushua nilishindwa hata cha kumuambia.
“Aliyekuambia mimi nina shida na marafiki ni nani?”
Aliendelea kunipaka.
“Nilishawahi kuja kwako nikakuambia mimi ninashida na marafiki? Mbona unapenda shobo hivyo.”
Aliongea Tessa kwa hasira.
Nilivuta pumzi na kushusha.
Kiukweli nilishidwa kabisa cha kumuongelesha.
Diana alikua akinionesha ishara kwamba niendelee kuongea.
Mdomo uliniwia mzito sana.
“Endelea kumshawishi.”
Aliongea kwa sauti ya chini.
Hata hivyo nilishindwa kuongea chochote.
“Sikia…”
Tessa aliendelea.
“Tena mwambie anikome.”
“Daah sawa.”
Diana alivuta pumzi na kushusha.
“Sasa utamuogopa mpaka lini?”
Diana aliongea mara baada ya kukata simu.
“Siyo kama namuogopa ila wewe Tessa humjui.”
“Sasa hapo kutakuwa kuna ugumu unaonaje kama utakutana nae. Kwanini usiende nyumbani kwake?”
“Nyumbani kwake? Mimi tena?”
Niliongea kwa jazba.
“Kwanini?”
“Tessa ameshanifukuza nyumbani kwake mara mbili tena ananifukuza kama mwizi.”
“Aisee hapo naona ugumu.”
Mwishowe Diana aliongea.
“Lakini usijali tutafikia mwisho.”
“Sawa.”
“Sawa ahsante.”
“Ngoja mimi nitoke nikipata namna yoyote ya kukusaidia nitakuja.”
Aliongea Diana na kisha kuondoka.
Nilibaki tu nikiwa na mawazo mengi.

Niliamua kutoka na kisha kuelekea ofisini siku hiyo niliamua kwa dhati kabisa kufanya kazi.
Nilishughulikia kazi zote zilizokuwepo mezani.
Wafanyakazi wangu walikuwa wakinishangaa.
Sekretari wangu alikuja kuniuliza.
“Bosi siku za hivi karibuni umekuwa sikuelewielewi.”
“Aah usijali si unajua tu mambo ya kawaida binadamu hatuko sawa kila wakati.”
“Naona, nimefurahi saa hizi umerudi kazini nilimisi sana uwepo wako.”
“Ulimisi nini…?”
Tessa huyu hapa alikuwa ameshafika.
Kwa bahati mbaya zaidi kulikuwa kuna wageni wawili ambao walikuwa wakisubiri kuonana na mimi.
Aliongea hayo akiwa mlangoni kiasi kwamba wateja wangu waliweza kumsikia.
“Naomba tupishe.”
Nilimuambia Pendo sekretari wangu.
Pendo aliniangalia na kisha kutoka nje.
“Hivi…”
Ilibidi ninyanyuke na kwenda kumziba mdomo.
“Tessa hapa tupo kazini cheki wateja wangu wapo hapo nje wakikusikia unapiga kelele si utaniharibia kazi.”
“Niache…”
Alitoa mkono wangu mdomoni kwake na kisha kuanza kuropoka.
“Aliyekuambia ninashida na marafiki ni nani? Wewe unajiona wewe ndiyo mama huruma sana wa kusaidia watu kupata marafiki.
Nakushangaa sana wewe mkaka nilishawahi kuja kwako kukutangazia shida?”

Aliendelea kupayuka.
“Tessa… Aaanh… Tessa hayo ni mambo ya kuyaongelea nyumbani.”
Niliongea.
Mlango ulibishwa.
“Tessa…”
Nilimuita kwa sauti ya upole.
Alibaki tu akiniangalia hakuonesha kujali kitu chochote.
Nilimuonesha ishara ya kunyamaza huku nikiwa nimepaniki.
Alinyamaza na mimi nilienda kufungua mlango.
Alikuwa ni sekretari wangu sura yake ilionesha kuhamanika.
Alitikisa kichwa huku akionesha kabisa kwamba amechanganyikiwa.
“Vipi?”
Niliangalia pembeni na wale wateja waliokuwa wamekuja ofisini kwangu hawakuwepo.
“Nini kimetokea?!”
“Bosi wateja wanalalamika sana siku hizi kazi zao hufanyi wanakuja ofisini unaanza kufanya kazi mnaanza kuleta migogoro ya kifamilia sijui nini, wameondoka wamesema watatenda kumtafuta mtu mwingine wewe kama umeshindwa kushughulikia mambo ya nyumbani kwako utaweza kushughulikia kesi zao au shida zao.
Wameondoka.”

Aliongea kiupole Pendo.
“Haaaa…”
Nilivuta pumzi ya kuchoka.
Tessa hakuonesha kujali.
“Na wewe ondoka unasubiri nini? Si umeshaona tuna mambo ya kifamilia.”
Pendo alikunja sura huku ameachia mdomo.
“Sawa nenda nyumbani kapumzike.”
Nilimuambia.
“Sawa.”
Aliondoka kiunyonge.
Niliingia ofisini kwangu na kisha kukaa.
“Bado sijamalizana na wewe.”
Tessa aliongea.
“Tessa hebu nitolee ujinga wako hapa.”
Niliongea sasa kiushujaa.
“Aanhaa…”
Alisema kwa ashuo.
“Kwahiyo wewe unaona kama vile mimi nafanya ujinga si ndiyo.”
Tessa aliongea.
“Tessa mimi niko nafanya kazi kwa ajili ya future yetu mimi na wewe mara ngapi nakuambia kwamba nataka kukuoa uwe mke wangu?”
“Kwani nilikataa?”
Aliongea Tessa.
“Sasa mimi si nafanya kazi, wewe mambo ya kifamilia unayaleta ofisini kiasi kwamba wateja wangu wanaondoka.
Hebu fikiria tutajenga vipi? Eee?! Hayo maisha ya baadae tukishaoana tutaishi vipi?
Unataka mimi nikae nyumbani tunaangaliana tutakula nini?”

Niliongea kwa jaziba.
“Yani umekuwa mwanamke mpumbavu sana Tessa, mimi nashangaa sana aisee… Hufikirii hata?!!”
Niliendelea kupayuka.
Niliamua kuongea yote siku hiyo kama akiamua kuniacha na aniache tu nilishachoshwa sana na vitimbi vyake.
Wakati nikiwa hasira imeongezeka nilishituka tu.
Tessa alikuwa akilia kilio kikubwa tena cha kwikwi.
“Kwahiyo unaniona mimi mjinga.”
Tessa aliongea.
“Mimi mkorofi.”
Alizidi kulalama.
“Tessa mimi si nakuambia ukweli hasa kwanini usingenisubiri turudi nyumbani na kwanini usingenipigia simu tukutane sehemu tuongee tuyamalize.”
“Eti kugombana mpaka tupange appointment, umeshawahi kuona wapi watu wanagombana kwa appointment?
Kwahiyo mimi kuja kuelezea hisia zangu nimeonekana mimi mpumbavu, nimeonekana mimi mchochezi, mimi mgomvi.
Kwahiyo mimi ndiyo sina future yoyote au unafikiri mimi sikupendi. Unanionea sana.”

Aliendelea kulalamika huku akilia.
“Aanh… Tessa sijamaanisha hivyo.”
“Umemaanisha nini? Mimi si mpumbavu, mimi si mjinga kwanini huniachi.” “Aanh…”
Nilishindwa cha kuongea.
Alishika kichwa kuashiria kwamba ana maumivu ya kichwa ilibidi nisogee karibu na kumkumbatia.
Tessa alikuwa akilia kiasi kwamba nafsini mwangu roho iliniuma sana kwa nilichomfanyia.
“Nimewezaje kumliza Tessa jamani.”
Tessa alishika kichwa na aliegemea meza ilibidi nimsogelee na kumkumbatia tena.
“Unajisikiaje Tessa.”
“Kichwa kinaniuma sana.”
“Basi nisamehe mke wangu, nisamehe sana.”
Niliongea.
“Wewe unanionea sana.”
“Sijui hata tutaishije kwenye hiyo ndoa mimi naona bora tu tuachane.”
“Aanhaa….. Usifike huko, usifike huko basi mama naomba nisamehe kwa yote sikutafutii tena rafiki wala sitakuja kukuletea habari za marafiki. Naomba tuondoke tuelekee nyumbani.”
“Nataka kwenda kwangu.”
Alisema.

Sehemu 4 Sehemu 6
0
0