Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mtoto akiwa anatambaa sakafuni

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi nane (8)

Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua au kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.

Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi nane.

Kwa miezi nane usumbufu wa mtoto unaongezeka kwasababu anahitaji kuyajua zaidi mazingira yanayomzunguka.
Hapo unahitaji muda wa ziada kumuangalia kuhakikisha anakua salama.

Kwa sasa mtoto yuko vizuri kula vyakula tofautitofauti ila bado unaendelea kumnyonyesha.
Maziwa ya mama bado yanaendelea kuwa ni chanzo kikuu cha virutubisho vya mtoto .

Kwa miezi nane mtoto anafurahia zaidi kushika vitu na kula mwenyewe mfano vipande vya matunda.

Unaweza kuona jino linaaza kuota, ila hauna haja ya kuwa na wasiwasi kama haijatokea hivyo kwasababu ni kawaida pia kwa meno kuchelewa mpaka miezi 12.
Na kama meno yanaanza kuota tarajia kumuona mate yanazidi kutoka kwa wingi.

Kwa miezi nane watoto wanaanza kukaa wenyewe bila kushikiliwa, wengine wanaanza kutambaa au kutembelea makalio.

Kuhusu kutambaa huna haja ya kuwa na wasiwasi kama bado, kuna baadhi ya watoto hawatambai wanaanza kutembea moja kwa moja.

Watoto wa miezi nane wanakuwa na nguvu na usumbufu mwingi, na wanaweza kusimama wenyewe kwa kujishikilia kwenye vitu.
Jitahidi kuweka mazingira salama, ondoa vitu hatari karibu na mtoto.

Kudondoka au kujigonga ni sehemu ya kawaida ya utoto, jitahidi kuweka mazingira salama ila siku kumlinda sana kupitiliza.
Mtoto anahitaji kuyajua mazingira yake vizuri kwa uhuru.

Watoto wanakuwa na uwezo wa kutafuta vitu vilivyodondoka au kufichwa, na wanaweza kunyooshea kitu kidole.
Wanajifunza kuokota vitu kwa vidole vyao na wanakuwa na uwezo wa kugoganisha vitu alivyovishika.

Pia wanakuwa na uwezo wa kurusha vitu ila bado wanaendelea na tabia ya kupeleka kila kitu mdomoni.

Uwezo wa mtoto kuona unakuwa umeimarika vizuri kwasasa kama mtu mzima, na anaweza kukuonesha picha sahihi ya kitu unachomtajia.

Mtoto anakuwa na uwoga wa kutengana na mzazi wake, anaweza kulia kama akichuliwa na mtu mwingine au kama unataka kumuacha peke yake.
Taratibu ataanza kujifunza kuwa mzazi wake akiondoka ni lazima atarudi na kuanza kujenga uaminifu na watu wengine wa karibu.

Mtoto anaanza kulitambua na kuitikia jina lake, pia anaanza kuyatambua majina ya wanafamilia wengine.

Ili kumsaidia mwanao kukua na kuwa na maendeleo mazuri:

Muongeleshe mtoto mara kwa mara kadri unavyoweza inamfanya aendelee kupenda kujifunza kuongea.

Mara nyingi zaidi unavyoongea nae ndivyo anaendelea kujua maana ya maneno.
Jitahidi kumfundisha namna ya kufanya mazungumzo kwa kuitikia na kumjibu sauti zake anazotoa.

Tumia hisia na ishara mbalimbali ili kumrahisishia mtoto kuelewa nini unamaanisha.

Unaweza kucheza na mwanao michezo mbalimbali na wanapenda sana kengele na vitu vinavyotoa sauti.

Mfanyishe mazoezi mbalimbali kama kumsaidia kutembea inamsaidia kuimarisha misuli yake.

Kwasababu watoto wanakua tofauti kuna wanaowahi na kuna wanaochelewa, ila kwa mtoto wa miezi nane unapoona mambo haya ni muhimu kumuona daktari kwa msaada zaidi.

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi tisa (9)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi saba (7)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi sita (6)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitano (5)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne (4)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)

0
0
1