Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi tisa (9)
Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua au kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.
Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi tisa.
Kwa miezi tisa ubongo wa mtoto unakuwa kwa kasi, na anaanza kuonesha tabia zake.
Kwa umri huu unaweza kuanza kupata picha ya tabia za mwanao akikua.
Uwezo wa mtoto kutunza kumbukumbu nao unaendelea kukua, na sasa mtoto anaweza kuvutiwa sana kuwa na baadhi ya watu kuliko wengine.
Ila bado mtoto anaendelea kuwa na uwoga wa kutenganishwa na mzazi wake ni hali ya kawaida.
Kwa miezi tisa mtoto anakuwa na uwezo wa kuchukua chakula mwenyewe na kula.
Ni muhimu kumchanganyia vyakula vyenye virutubisho tofautitofauti.
Kwa mtoto wa miezi sita anaweza kusimama na kutembea kwa kujishikia kwenye vitu au ukuta.
Mtoto anakuwa na uwoga wa kutengana na mzazi wake, anaweza kulia kama akichuliwa na mtu mwingine au kama unataka kumuacha peke yake.
Hali hiyo inaweza kusababisha mtoto ashindwe kulala akihofia utamuacha peke yake.
Taratibu ataanza kujifunza kuwa mzazi wake akiondoka ni lazima atarudi na kuanza kujenga uaminifu na watu wengine wa karibu.
Mtoto anajisikia huru zaidi unapokuwa karibu yake na anakuwa na wasiwasi unapokuwa mbali nae.
Mtoto wa miezi tisa anaanza kuelewa maana ya baadhi ya maneno, na kama utamuonesha kitu anaweza kugeuka kukiangalia.
Mtoto anatoa sauti na kuiga sauti mbalimbali, anapiga makelele ili kukuita umsikilize na anaacha kama utamkataza.
Pia mtoto anakuwa analijua jina lake ukimuita.
Ili kumsaidia mtoto kukua na kuwa na maendeleo mazuri:
Ongea na mwanao, muimbia na msomee vitabu ili kumsaidia kuelewa lugha.
Muigizie sauti mbalimbali za kufurahisha, muelezee kile ambacho utakuwa unakifanya ukiwa nae na mjibu sauti zake anazozitoa.
Msaidie mwanao kujiamini anapotaka kutembea kwa kusimama au kupiga magoti mbele yake kumzuia asianguke.
Kwasababu watoto wanakua tofauti kuna wanaowahi na kuna wanaochelewa, ila kwa mtoto wa miezi tisa unapoona mambo haya ni muhimu kumuona daktari kwa msaada zaidi.
- Kama mtoto hajaanza kujisogeza kabisa au anashindwa hata kukaa.
- Haoneshi kuvutiwa kitu chochote au kutaka kushika vitu karibu yake.
- Anashindwa kukutambua mzazi wake, mlezi wake au anashindwa kukuangalia machoni mkiangaliana.
- Anashindwa kugeuka kuangalia sauti inapotokea au anapoitwa kwa jina lake.
- Mtoto anashindwa kutoa sauti au anashindwa kutambua sauti za watu wengine.
- Na kama mtoto anasumbua kwa muda mrefu na unashindwa kumbembeleza akatulia.
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi kumi (10)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi nane (8)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi saba (7)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi sita (6)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitano (5)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne (4)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)
Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)
Unaweza pia kusoma: