Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mtoto wa kike akiwa amekaa kwenye kochi akiangalia juu

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi kumi (10)

Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua au kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.

Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi kumi.

Mtoto wa miezi kumi uimara wake unaongezeka, tarajia kuona unakimbizana nae kwasababu anatambaa na kutembea kwa kujisikilia kwenye vitu.

Baadhi ya watoto wanaweza kuwa wanapungua uzito katika kipindi hiki, sababu zinaweza kuwa ni kucheza cheza sana, kuumwa, au kuwa busy na michezo kuliko kula.

Watoto wa miezi kumi wanaweza kutambaa vizuri ila usiwe na wasiwasi kama mwanao atakuwa bado kwasababu kuna watoto wengine wanatembea moja kwa moja bila kutambaa.

Mtoto anaweza kukaa chini mwenyewe kwa kujiamini, na ana uwezo wa kutembea kwa kujishikilia kwenye vitu au ukuta.

Mtoto anaendelea kuvutiwa na kuchunguza vitu mbalimbali vinavyomzunguka.
Anakuwa na uwezo wa kutafuta vitu vilivyofichwa, anasogelea vitu na kuvishika na anaweza kuvirusha.

Anaweza kunesanesa akisikia mziki, anaweza kuigiza sauti na anaweza kushika vitu kiurahisi na vidole vyake.

Kwa miezi kumi uwoga wa mtoto kutenganishwa na mzazi wake unaanza kupungua, na unaweza kumuacha na watu wengine asisumbue.

Baadhi ya watoto wa miezi kumi wanaanza kupata uwoga kwa sauti za ajabu ambazo hawajazizoea, kumkumbatia itamfanya ajihisi yuko salama.

Ili kumsaidia mtoto kukua vizuri na kuwa na maendeleo mazuri:

Katika kipindi hiki mtoto anapenda kufanya mazungumzo, hivyo ongea na mwanao muda wote utakapokuwa nae.

Kwasababu anakuwa hawezi kutamka maneno vizuri rudia kumtajia neno sahihi ili kumfundisha lugha.
Muelezee mwanao unachokuwa unakifanya ukiwa nae, na tumia maneno na ishara kumuelewesha.

Msomee vitabu mtoto ili kumuongezea uelewa wa vitu mbalimbali.

Ni muhimu kumuhimiza mtoto kutembea hata kama ataanguka na kuumia.

Japo ukuaji wa watoto ni tofauti sana kuna wanaowahi na kuchelewa, ila kwa mtoto wa miezi kumi unapoona mambo haya ni muhimu kumuona daktari kwa msaada zaidi.

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi kumi na moja (11)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi tisa (9)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi nane (8)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi saba (7)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi sita (6)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitano (5)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne (4)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)

0
0
1