Muonekano wa Giza:

Msaada

Picha inamuonesha mtoto akiwa na amama yake kitandani na wote wanaonekana wakiwa kwenye furaha

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi kumi na moja (11)

Baada ya kujifungua shauku ya wazazi ni kujua au kuona maendeleo na ukuaji mzuri wa mtoto.

Katika makala hii tufahamu kuhusu ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi kumi na moja.

Kwa miezi kumi na moja sasa mtoto anauwezo wa kuona vitu vya mbali na karibu, udhibiti wa mikono yake na macho nao umekua na anaweza kuona kitu mbali na kukifuata.

Uwezo wa mtoto kunusa umeongezeka na anaweza kuanza kuchagua vyakula.

Baadhi ya watoto wa wanaweza kuanza kujifunza kutembea, japokuwa bado anapendelea kutambaa.

Kwa watoto wa miezi kumi na moja wanaweza kuchukua chakula na kula peke yao, na wengine baadhi wanaweza kushika kikombe na kunywa peke yao.

Watoto wa miezi kumi na moja wanapenelea sana vitabu vyenye picha pia hufurahia kusikiliza mziki na kuchezea matoy yanayotoa sauti.

Kuna baadhi ya watoto wanaendelea kuwa na uwoga wa kutengana na mzazi, ila wengi katika umri huu wanaanza kuona kawaida hata unapomuacha peke yake.

Mtoto anajihisi huru zaidi ukiwepo wakati anacheza, wakati anaendelea kucheza mara kwa mara anageuka kukuangalia.

Uwezo wa mtoto kujifunza lugha unakuwa kwa kasi na unaweza kuanza kumsikia akijaribu kutamka maneno.
Wanaweza kutumia njia nyingine za kuwasiliana kama vile, kunyooshea kitu kidole, kutikisa kichwa, kupunga mkono na kuunguruma.

Wanaanza kuelewa baadhi ya maelekezo na kuonesha ushirikiano wakati wa kuvaa nguo.

Muda huu ni muda ambao unaweza kuanza kumuwekea mtoto mipaka kwa kumkataza vitu hatari.

Jinsi ya kumsaidia mtoto kukua na kuwa na maendeleo mazuri:

Jitahidi kuongea na mwanao mara nyingi zaidi kadri unavyoweza.
Mara nyingi zaidi unavyoongea nae ndivyo anazidi kujifunza zaidi maneno.
Na muoneshe kuwa unamuelewa anachokisema.

Pia unaweza kuongeza uelewa wake wa mambo kwa kumsomea vitabu na kumuimbia.

Ni muhimu kumhamasisha mwanao kutembea, msaidie kusimama na kujaribu kutembea ila hakikisha mazingira yako salama.

Licha ya kuwa watoto wana ukuaji na maendeleo tofauti ila unapoona mambo haya kwa mtoto ni muhimu kumuona daktari kwa msaada zaidi.

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi kumi (10)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi tisa (9)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi nane (8)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi saba (7)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi sita (6)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi mitano (5)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto wa miezi minne (4)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi mitatu (3)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa miezi miwili (2)

Ukuaji na maendeleo ya mtoto mchanga wa mwezi mmoja (1)

0
0
1