Muonekano wa Giza:

Msaada

L and L (Msimu wa Kwanza) - Sehemu ya Pili (02)

Na siku iliyofuata alirudi klabu aliyoenda mara ya kwanza.
Alihudhuria klabuni hapo kwa wiki takribani mbili mfululizo bila mafanikio kabla hajakutana nae siku asiyodhani.
Hakutarajia kumuona siku hiyo, hali iliyompunguzia kujiamini.
Tofauti na faili lake na picha mtu yule alionekana mstaarabu sana.
“Ndo mana anatuchanganya sana tunashindwa kujua kama ni mhalifu ama hapana.”
Aliwaza Lissa kabla hajaingia kati kucheza kama kawaida yake na sasa wahudhuriaji wa kila siku walikuwa wakimjua.
Leo hii Lissa alikuwa akinengua hali akiwa hayupo katika hali yake ya kawaida.
Alishazoea kumkosa mtu wake na leo ni kama alikuwa hajui cha kufanya haswa ili kumvutia mtu wake maana amemsubiri kwa takribani wiki mbili sasa na hajui kama kesho mtu wake atarudi tena hapo wakaonana.
Hata pale alipokuwa akinengua alimtupia jicho la wizi alimuona mtu wake akimuangalia na kisha kunong'ona na mtu aliyekuwa karibu naye ambaye ndiye aliyekuwa mmiliki wa ile klabu maarufu.
Mwenye klabu hiyo alianza kuongea mfululizo wakati mtu wake Lissa akimsikiliza na mara kadhaa akicheka.
Lissa alihisi akiongelewa hivyo alizidisha kasi ya kunengua.
Zaidi ya kuhisi kuongelewa Lissa hakuona chochote kile.

Mpaka kufikia saa saba alikuwa amechoka na mtu wake hakuwa na dalili ya kuondoka.
“Ntachelewa kazini kesho, and i'm so tired... Mi naodoka bhuana.”
Alijiwazia.
Akapita kaunta akachukua savanna tatu na kisha akapita kiulevi mahali alipokaa mtu wake pamoja na marafiki zake huku akiutikisa mwili wake uliojaliwa shepu nzuri na rangi nyeusi ya kuvutia.
Ingawa hakugeuka nyuma lakini hisia zake zilimwambia kuwa watu wote waliokuwepo hapo waligeuka kumuangalia.
Hakukosea ijapokuwa mtu wake hakugeuka.
Aliendelea na mambo yake kana kwamba hakuna kiumbe kilichopita hapo.
Lissa alienda hadi garini kwake kabla ya kuondoka kwa kasi huku akijipongeza kwa hatua aliyopiga siku hiyo na matukio yaliyotukia siku hiyo pale klabuni yalianza kujirudia.
“Haonekani kama ni mtu mbaya but who knows, anyway sahivi mbivu na mbichi zitajulikana.”
Alifika kwake na kuweka chupa za savanna kwenye ndoo ya kukusanyia uchafu ambayo saa hiyo ilikuwa na chupa kadhaa za bia zisizofunguliwa.
Alikuwa akitoka nazo klabu na kuziweka hapo.

Shuleni Lissa hakuwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakifanya vizuri sana hata hivyo hakuwemo kati ya wale waliokuwa wakifanya vibaya.
Alikuwa wa wastani ila alikuwa mtukutu sana na yote ni katika kuishi ndoto yake ya upelelezi.
Akiwa shuleni aliwahi kuadhibiwa kwa kujaribu kushuka kutoka ghorofa ya tatu kwa kupitia dirishani na kuruka ukuta wa shule.
Baba yake alimsisitiza kupata shahada yake ya kwanza kabla hajajiunga na jeshi la polisi na ndipo alipojiunga na chuo cha TIA kwa masomo ya uhasibu.
Akiwa chuoni alipata mpenzi ambaye hakudumu naye kutokana na tabia ya Lissa ya ukorofi.
Na toka hapo Lissa hakuwa na mahusiano tena.

Alipomaliza chuo alijiunga na jeshi la polisi, alipata mafunzo kule Moshi na baada ya kufanya kazi kwa miaka 2 alipata nafasi ya kwenda kusomea upelelezi nchini Urusi.
Lissa hakuwa mnywaji wa pombe wala mtu wa klabu ijapokuwa alipenda kunengua.
Suruali ilikuwa vazi lake pendwa hakuzoea kuvaa nguo fupi lakini misheni aliyopewa ilibadilisha yote haya na kufanya Lissa aishi maisha asiyoyazoea ya kukesha klabu, kunywa pombe, kutokufanya usafi na mengineyo.

Asubuhi ya siku iliyofuata aliingia kazini kama kawaida na alikuwa na furaha sana.
Mara mkuu wake wa kazi mzee Mwalukani aliingia na baada ya saluti waliketi huku mkuu wake wa kazi akimuuliza juu ya maendeleo ya kazi yake.
“Inaendelea vizuri imenichukua muda kuonana nae ila nimefanikiwa na nilipofikia sio pabaya.”
“Nakutegemea usiniangushe Lissa.”
Na baada ya hapo maongezi mengine yaliendelea.
Usiku huo alirudi klabuni na hakumuona mtu wake na usiku uliofuata pia hakumuona mtu wake na usiku uliofuata pia hakumuona mpaka saa 8 za usiku alirudi kwake akiwa mnyonge.
“Does it mean sitamuona tena ama ndo mpaka wiki 2 zipite!?
Si nitapoteza sana muda mwisho wake nitaambiwa niandike hitimisho yani nimeshindwa.
No I can’t fail kama hii njia nikishindwa I will go for the next one.”

Aliwaza Lissa na kulala.

Na kesho yake hakwenda kazini jioni alivaa vyema na kwenda klabu.
Aliagiza savanna zake na kuzinywa kiukweli kweli tofauti na anavyofanyaga siku nyingine hata alipoambiwa akanengue alikataa.
Baada ya kunywa savanna nyingi alikuwa hoi kwelikweli japokuwa hakumuona mtu wake.
Aliamua kuondoka wakati akikaribia gari lake alishikwa mkono.

“Lissa kila siku nakutaka hunitaki leo utataka.”
Sauti ya kilevi iliongea ingawa hakuwa akimfahamu lakini alihisi alikuwa akimuona hapo klabu mara nyingi na inawezekana kila siku.
Huyu alikuwa mteja mzuri tu wa hapo ingawa habari za kutakwa yeye hakuwa nazo.
“Niache bhana.”
Lissa alijibu kilevi.
Na yule mtu kana kwamba hakumsikia aliendelea kumvuta wakivuka uwazi ambao watu waliutumia kutoka na kuingia klabuni hapo kulikokuwa na parking ya magari.
Lissa hakuwa na nguvu ya kujizuia kutokana na kuelemewa na kilevi alibakia kuongea kilevi akisisitiza aachwe huku yule mtu kama vile haelewi alizidi kumburuta kuelekea alipopafahamu yeye mwenyewe.
“Let her go.”
Sauti nzito ya kiume iliwashitua wote wawili na yule mwanaume aliyekuwa akimkokota Lissa.
Alimficha Lissa nyuma yake huku akijaribu kuzozana na mwanaume aliyeingilia kati.
Lissa hakuwa hata na nguvu ya kufumbua macho.

Mzozo haukuwa mrefu mwishowe Lissa alisukumwa kuelekea kwa jamaa aliyemuokoa na yule jamaa alimkokota hadi kwenye gari lake Lissa.
“Will you be able to drive?”
Yule mtu akamuuliza Lissa.
“Yes don’t worry buddy thank you.”
Lissa alijibu kiulevi bila kumuangalia yule mtu.
Baada ya kumuweka Lissa kwenye kiti chake yule jamaa akaondoka.
Na Lissa hakujishughulisha kuwasha gari bali alijiegemeza kwenye kiti na kulala.

Alikuja kushituka saa 11 alfajiri akiwa palepale klabuni na sasa ulevi ulikuwa umepungua ila kichwa kilikuwa kikimuuma sana.
Aliwasha gari na kuondoka hadi nyumbani kwake changanyikeni ambapo alibadili mavazi yake na kuelekea ofisini kwake.
Jioni alienda klabu alikuwa na uchovu na hakutaka kunywa tena kama jana.
“Siku hizi najiona kama nimenogewa na klabu, jana mtu wangu hakuja and I didn't mind leo despite of uchovu wote nimekuja but sijisikii kunywa pombe wala kulewa.
Achilia mbali kucheza mziki and I will leave early jamaa yangu simuoni…
Kwanza I have to change my plans its almost 3 weeks now na sijapiga hatua ya maana.”

Mawazo yalipita kichwani kwake huku kinywwaji cha apple punch alichoagiza hakikuwa hata kimefunguliwa.

“Hey cutie.”
Sauti nzito ya kiume ilimshitua na kumsisimua.
Sauti hiyo iliyomtoa mawazzoni ilimfanya ageuke na mara alimuona mtu wake.
Alipigwa na butwaa hakutegemea kumuona mahali hapo jasho lilimtoka huku akishindwa neno la kuongea.
“How are you?”
“Me?!”
“Yes, ama kuna mtu mwingine hapa?”
“Aah no niko mwenyewe I’m fine, it’s just unusual for someone you haven’t seen before kunijulia hali.”
Alijieleza kwa urefu Lissa huku hali ya kijiamini ikimrejea na kujikumbusha kuwa yuko kazini.
Yule jamaa alicheka tu kidogo cheko ambalo mtu angeweza kudhania ni dharau.
“Well za toka jana.”
Aliuliza yule jamaa.
“Nzuri.”
“Uliweza kufika nyumbani mwenyewe?”
Jamaa aliuliza maswali mengi.

Sehemu 1 Sehemu 3
0
0