L and L (Msimu wa Kwanza) - Sehemu ya Tano (05)
“Vipi mwalimu katoa tena assignment ama anataka tufanye ile nyingine mi nipo mbali mean nipo kwa mtu wangu sijui unanielewa
sitaweza kufika hivi karibuni.”
Lissa aliongea haraka haraka na kwa kiherehere.
“Aanh.”
Upande wa pili wa simu uliguna na kisha simu ikakatwa.
Lissa alishusha pumzi kwa nguvu.
Leonard alimuangalia Lissa na kucheka.
“Ndo shida ya vyuo kudahili walevi ona wanavyowapa tabu wanafunzi waliokuja kusoma.”
Alisema Leonard kiutani na Lissa akakasirika.
Akaanza kumrushia mito huku Leonard akiikwepa.
Wakaanza kukimbizana na ilionekana ni jambo la kuvutia.
Walikimbizana...
Wakakimbizana wakaishia tena chumbani.
Katika harakati za kukimbizana na Leonard alikimbia akielekea kitandani lakini ghafla akabadili uelekeo na
kupita pembeni ya kitanda.
Lissa aliekuwa akija kwa kasi alichelewa kujua nia ya Leonard akashindwa kujizuia na kuanguka kitandani.
Leonard akawa anamcheka na Lissa akazidi kufura kwa hasira.
Leonard hakuwa na budi ila kumbembeleza kipenzi chake.
Alisogea pale kitandani na kulala kwa pembeni yake Lissa.
“Baby I’m sorry.”
Alisema Leonard kwa sauti yake nzuri.
Lissa aligeuka kwa hasira na kumvutia kwake.
“Nimekukamata.”
Alisema Lissa huku akicheka lakini ni kama vile Leonard hakuwa na habari na mchezo ule tena.
Alimtazama Lissa kwa kumkazia macho.
Lissa nae alikosa ujasiri kutokana na muangalio wa Leonard alijikuta akiachia shati la Leonard.
Leonard alinyanyua mkono wake mpaka shavuni kwa Lissa na kumpapasa taratibu na busu kali lilifuatia.
Busu hilo lililojaa hisia zote liliwafanya washindwe kujizuia na kuvunja miiko waliyoiweka katika penzi lao hilo
ambalo kila mtu alikuwa na lengo lake.
Ni hadi baada ya saa moja mbele kila mtu alikuwa akiwaza lake.
Leonard alikuwa jikoni na Lissa alikuwa kitandani.
“Lissa haonekani kama she is a bad girl like I used to think she is a wife material.
Akimaliza kusoma mi namuoa walah sijawahi hisi hivi kwa mwanamke yoyote na sikutegemea mimi kumpenda mwanamke hivi.
I used to hate them so so much but love is powerful.
Mapenzi yana nguvu kuliko mauti.
Look at me now hahaha.”
Leonard alikuwa akiwaza mwenyewe wakati akisubiri maji yachemke.
“I lost my virginity trying to catch culprit.
That doesn’t make me fall for him.
Nitafanya chochote kile endapo tu hakivunji sheria ili kuhakikisha namtia mbaroni.
Wacha ajihakikishie kuwa nampenda but it hurts uuh!
Now that I gained his trust kazi imekuwa rahisi zaidi.”
Aliwaza Lissa na ujumbe ukaingia kwenye simu yake.
“Sikiliza Lissa kuna taarifa kutoka kwa mwalimu mkuu quiz mpya inayopangwa kufanyika leo.
Ni muda mzuri wa kupitia pitia ili upate kitu chochote kichwani hiyo quiz take care of mtu wako.”
Ujumbe kutoka kwa mkuu uliosomeka hivyo aliucheka ujumbe ule na kuuelewa.
“Someka.”
Alijibu.
Baada ya dakika chache Leonard alirejea na Lissa alijifanya akiugulia maumivu makali.
Ijapokuwa maumivu alikuwa nayo lakini hayakuwa makali kiasi cha kumtoa machozi.
Leonard alimkanda kwa maji ya moto na kusaidia kupunguza maumivu kwa kisi fulani.
Siku hiyo walishinda wote hapo nyumbani mpaka usiku.
Lissa alikuwa makini kumchunguza Leonard kwenye kila anachofanya na simu anazozipokea.
“Pia kuna taarifa kuwa semina zitaanza hivi karibuni room 04 uhudhurie.”
Ujumbe uliingia kwenye simu ya Lissa.
Ingawa hakuelewa lakini alidhamiria kufanya uchunguzi kwenye nyumba yote.
Mpaka saa sita usiku Lissa hakuwa ameona chochote wala kusikia chochote cha kutia mashaka.
Hii ilimpa imani kuwa Leonard sio mhalifu japokuwa bado hakuthibitisha.
“Kama nitamkamata akiwa mhalifu nitakuwa sijapoteza kitu nimelinda nchi yangu.
Na kama nitajidhirisha sio mhalifu nitakuwa nimepata mapenzi jamaa anajuaa kupenda.”
Aliwaza Lissa na kucheka mwenyewe.
“Tumechelewa quiz imefanyika.”
Ujumbe kutoka kwa mkuu uliingia kwenye simu ya Lissa.
Lissa aliamua kutoujibu kwani alielewa kilichotokea.
Asubuhi na mapema Lissa aliamka na kuanza kukagua nyumba ya Leonard kabla Leonard hajaamka.
Alizunguka vyumba vyote ambapo vitatu kati ya vitano vilikuwa na vitanda na vilionesha havitumiki.
Lissa alikagua hadi uvunguni na maliwatoni kwani vyumba vyote vitatu vilikuwa vinajitegemea.
Na chumba cha nne alikuta fenicha mpya zimejaa zikiwa na vumbi sana.
Alizichunguza na kujidhilisha ni salama akatoka nje.
Alipokuwa katika kutoka akakutana uso kwa uso na Leonard.
“Vip baby?”
“Nimeamka mapema nikawa natembea tembea.”
“Ooh ok leo unarudi chuoni saa ngapi?”
“Asubuhi hii naenda kujiandaa hivyo.”
Lissa alijianda na Leonard alimpeleka na kumuacha utawala chuoni UDSM.
Lissa wala hakuenda kwake alipitiliza ofisini kwake.
“Jana ilikuwaje.”
Lissa aliulizwa na mkuu wake wa kazi baada ya kuwasili na salamu.
“Nusu tubambwe ila hajashitukia.”
“Daah ulitumia akili nyingi sana…
Jana tulipata taarifa tena kuwa jamaa anaingiza mzigo wa madawa na silaha ndo nikakwambia umchunguze na sisi tulikuwa tunategemea
sana taarifa yako baada ya kuchelewa ikabidi tuende kule tukakuta washaondoka.”
Mkuu alijieleza.
“Yani hata hakuna kiashiria nimekagua nyumba yote hadi simu yake na sehemu anazoenda lakini hakuna chochote cha mashaka.
Nadhani mtoa taarifa ni mhalifu ambaye lengo lake ni kutupoteza anatuelekeza kwa mtu sio huku akifanya shughuli zake za kihalifu.”
“Nadhani nakubaliana na wewe Lissa andaa ripoti na sasa tutaanza kufuatilia chanzo chetu cha habari.”
“Mkuu nipe muda kiasi nikusanye ushahidi zaidi ili pasiwepo shaka tena hapo baadae kumbuka ni miaka mingi mnamfuatilia
nataka tukiachana nae iwe mwisho.”
“Sawa Lissa kazi nzuri sana umefanya mpaka hapa.”
Baada ya maongezi Lissa alimalizia siku hiyo ofisini na jioni alifika nyumbani kwake.
Alipoingia tu simu yake iliita.
Alikuwa ni Leonard.
“I miss you wife.”
“Me too.”
“Usharudi kwako? Vipi masomo leo?”
“Poa tu niko kwangu.”
“Niko hapa Changanyikeni chuo cha takwimu.”
Lissa alishituka kidogo.
“Mbona umekuja bila taarifa.”
“I missed you Lissa.”
“Ngoja nikufate...”
Lissa alitoka na kumfuata Leonard hapakuwa mbali na anapoishi.
Alipofika aliingia garini akamkumbatia akaongoza kwenye "apartment" aliyokuwa amepanga.
Walipofika alimkaribisha ndani.
Japokuwa alimudu kufanya usafi, chupa za bia aina mbalimbali ambazo hakuwa amezifungua zilikuwepo nyingi sana.
Leonard alipoziona zikiwa zimejaa kwenye dustbin jikoni na nyingine kwenye makabati alimgeukia Lissa na kumuambia.
“You are not a bad girl like i used to think Lissa why ulikuwa unakesha klabu vile, unakatika katika ovyo.”
Lissa alijiinamia, kabla hajainua uso wake.
“I was stressed, lakini I met you ukanisahulisha stress zangu zote.”
Lissa alijieleza huku akiweka sura ya huzuni.
“Come here.”
Alisema Leonard.
Unaweza pia kusoma: