Muonekano wa Giza:

Msaada

L and L (Msimu wa Kwanza) - Sehemu ya Tatu (03)

“Alikuwa akinifuatilia ama amenigundua?!”
“Naona umekuja na surprise tu.”
Alisema Lissa baada ya kushindwa kumalizia lengo la swali la yule jamaa.
Jamaa alicheka tu.
“Well my name is Leonard I was the one who helped you last night.”
Lissa alishituka sana.
Usiku wa jana alikuwa amelewa sana hakuweza kumtambua mtu aliyemsaidia na hakuisi kama angekuwa ni mtu ambaye aliyekuwa akimuwinda kwa muda wote.
“You …”
“I mean…… You were very drunk yesterday nilivyoondoka i was asking myself, if you made it home safely.”
“Well I didn’t go, I slept here inside my car yesterday.”
“Ulifanya uamuzi mzuri sidhani kama ungeweza kuendesha gari vile…
But why unalewa vile wakati huna mtu wa kukusaidia! Best friend, boyfriend or others.
Unafanya kazi?”

“Naona maswali ni mengi.”
Alisema Lissa huku akitabasamu kabla ya kuendelea.
“Nnasoma kuhusu company I don’t have any.”
“You seem stressed, vipi boyfriend kakuacha, masomo au ndo stress zenu watoto wa kishua?”
“Nani kasema mi wa kishua.”
Alisema Lissa akicheka.
“Nikikuangalia tu najua.”
“Basi you are wrong.”
“Unasoma but you are driving your own car.”
Lissa alikwama kidogo.
“Ni hilo tu?”
Aliuliza Lissa.
“Why unajiachia klabu driking and throwing ass inaonekana ulikuwa unafungiwa na sasa umepata uhuru, you are nasty, a bad girl.”

Moyoni mwake Lissa alifurahia sana hatua hiyo.
Mtu wake ambaye sasa alimtambua kwa jina la Leonard na sio lile jina lake la uficho la Lux alikuwa akitamani kumfahamu.
Alijipa hongera kwa uvumilivu aliokuwa nao na sasa mpango wake unaendelea vizuri.
“Hamna baba yangu alikuwa mtumishi wa serikali alifariki last year mirathi ilipotoka ndo nilinunua gari yangu ya kutembelea.”
“Aaah pole na hongera… Kwahiyo unaishi na mama?”
“Hapana nimepanga karibu na chuo…”
“Umeniuliza mambo mengi, I hope you won’t mind I ask you some questions too?”
“I won’t mind so go on.”
Lissa alifurahi alijiweka sawa huku akijionya kutokufanya papara ili asijekushitukiwa.
“But before hujauliza please tell me your name.”
“Ooh my name is Lissa ninasoma pale UDSM.”
“So Leo unapenda sana bata…”
Leonard akamkatisha.
“I love how you call me Leo but I don’t like bata, pork is my favorite.”
Akasema Leonard na Lissa akaangua kicheko cha nguvu sana mpaka watu walioketi jirani wakageuka kuwaangalia.
“Okay unajishughulisha na nini?”
“Hili swali wadada mnalipenda.”
“No mi nimekosa tu chakuongea.”
“hahaha…”
“Ni mfanyabiashara tu mdogo mdogo.”
“Kwa jinsi unavyokesha klabu ungekuwa ni mwajiriwa ungeshafukuzwa kazi.”
“You too.”
Alijibu Leonard kwa kifupi na wote wakacheka.
“Mkeo hacomplain?”
“Ningekuwa nae angeshaniacha.”
“Hahaha so hutarajii kuoa.”
“I will… When I will meet a woman whom I will fall in love with unconditionally.”
Alijibu Leonard na wote walibakia kimya.

“Leo you can drink all you want ukilewa nitakubeba nikakuache pale chuoni kwenu wakiamka asubuhi waone wamedahili mlevi mmoja.”
Alisema Leonard huku akinyanyuka na Lissa alicheka sana.
“Am going to join my men, enjoy your drink ntalipia.”
Alisema Leonard nakwenda bila hata kusubiri jibu.
Lissa alimsindikiza kwa macho mpaka alipopotelea kwenye kundi la watu.
“Ni mpole anaweza kushika bunduki kweli huyu?!
Ana sauti nzuri halafu anachekesha.”

Aliwaza Lissa.

Mpaka saa sita Lissa hakumuona Leonard na siku hiyo alikuwa amechoka sana.
Aliamua kuondoka huku akijilaumu kutochukua hata namba ya simu ila alijifariji kwa hatua aliyopiga.
“Ningemuomba namba ningezingua.”
Kesho yake aliingia kazini na kuripoti alipofikia kwa mkuu wake wa kazi.
Alipotoka kazini aliamua kumtembelea mama yake huko Kijichi ambako mama yake alilalamika kuwa siku hizi mwanaye huyo wa kwanza amebadilika sana.
Lissa alimtoa hofu na kumuambia kuwa yupo kazini tu.
“Lini utaleta mkwe nyumbani?
Umri umeenda Lissa.”

“Mom bhana nikipata mtu sahihi nitamleta usijali.”
“Ama bado una ule ukorofi wako?”
“Hahaha… hamna mama nimebadilika.”
Waliongea na Lissa alimpikia chakula mama yake kabla ya kurudi kwake.

Alifika akiwa amechoka na nyumbani kwake kulikuwa kuchafu sana.
Siku hiyo alitamani kupumzika na kufanya usafi.
Mpaka kufikia saa 2 hakuwa amefanya lolote aliamua kwenda klabu Mwenge ili akale na nyama choma.
“Yani mimi kati ya kufanya usafi na klabu nimechagua klabu hii misheni haitaniacha salama.”
Alifika klabu na hiyo usiku alikuwa amechangamka sana.

Aliagiza bia moja aina ya smirnoff akainywa haraka haraka kisha akanyanyuka ili aweze kujichanganya na watu wanaocheza mziki.
Kabla hajafika katikati alivutwa mkono na mwanga mdogo kwenye "dance floor" ulimfanya ashindwe kumtambua aliyemvuta mkono.
Alivutwa hadi pembeni ya kaunta kwenye mwanga mkali kidogo na alimtambua Leonard kuwa ndiye aliemvuta mkono.
“Leo.”
“My bad girl Lissa.”
Lissa alitabasamu.
Mambo yalikuwa yanamuendea vyema.
Kwa pamoja walikosa cha kuongea wakabaki wanaangaliana.
Macho yao yakaongea kile ambacho hata midomo yao haikuwaza kama inaweza kukiongea.
Akili zao zilikabiliana na kile ambacho macho yalizungumza na midomo ikaamua kutekeleza kile ilichoambiwa na akili zao.
Midomo yao ikakutana taratibu na mikono yao ikaungana nayo na kuanza kupapasana.
Mwanzo Lissa alijiona yupo kazini lakini kadri sekunde zilivyozidi kusogea hisia zilitamalaki na msisimko mkubwa uliofuatia busu hilo lililochukua takribani dakika kadhaa lilifikia tamati na wakaachiana huku wakitweta huku wasijue nini kifuate.
“Don’t throw you, as I don’t like it.”
Alisema Leonard na kuondoka Lissa alibakia ameduwaa akili yake ilivurugika kabisa.

Aliketi pale kaunta na mhudumu alimpa smirnoff.
Lissa hakuwa na habari na kinywaji alichowekewa akili yake ikiwaza kuhusu busu lile kali alilopewa na namna mikono ya Leonard ilivyokuwa ikitembea maeneo yake hatarishi.
Alitabasamu, tabasamu lililoratibiwa na medulla oblongata kwani hakuwa na habari na tabasamu hilo na wala hakujua kama ametabasamu.

Sehemu 2 Sehemu 4
0
0