Muonekano wa Giza:

Msaada

L and L (Msimu wa Kwanza) - Sehemu ya Nne (04)

Mezani pale kaunta aliona bia mbele yake. Aliinyanyua na kuibugia mdomoni.
Alikujakushitukia kuwa bia ile haijafunguliwa, akaanza kujicheka mwenyewe na mhudumu wa pale kaunta nae alicheka kwakuwa alikuwa akimuangalia kwa kitambo kidogo.
Alifungua kwa meno na kunywa funda kadhaa.
Alikaa pale huku mawazo yote ya kimuelekea Leonard.
“Lissa usijisahau kuwa upo kazini, fanya unachotakiwa kufanya.”
Alijishauri mwenyewe.
Punde si punde Leonard alitokea.
“Lissa lend me your phone I want to reach someone.”
Lissa alitoa simu yake na kumpa Leonard nae alitoa yake akabonyeza namba kwenye simu ya Lissa na kupiga na mara simu yake ikaita.
“I will give you a call later.”
Alisema Leonard huku akiirudisha simu ya Lissa.
Naye Lissa aligundua kuwa alitumia njama ya kutaka kumpigia mtu simu ili kupata namba yake ya simu.
Kwa mara nyingine Leonard alikuwa amemvutia Lissa.

Lissa alikaa mpaka saa sita bila kumuona Leonard naye aliondoka kurudi nyumbani kwake.
Alipofika tu simu yake iliita ijapokuwa namba ilikuwa mpya na haikuwa imehifadhiwa kwenye simu lakini Lissa aliitambua tu kuwa ni ya Leonard na kupokea akiwa tayari kitandani.
“Hello.”
“Hello prettie.”
Alijibu Leonard kwa sauti ya upole.
“Mmh… Mambo.”
“Yanabadilika… Niambie umefika nyumbani salama?”
Alijibu Leonard na Lissa alicheka...
“Una vituko, yes nimefika salama.”
“Unafanya nini now?”
“Ndio nimeingia bed.”
“Don’t you wish ningekuwepo hapo?”
“I wish.”
“So why did you leave early.”
“Niliona hutokei nilidhani umeshaondoka.”
“Ningeondokaje bila kukuona.”
“Kwahiyo bado hujaondoka?”
“Yes, na nisipokuona nalala hapa hapa.”
Alijibu Leonard na wote wakacheka. “Kwani ulienda wapi?”
“Nilikuwa na kikao.”
“At club?”
“Kwani haiwezekani?”
“Sijui.”
“Anyway nilikuwa nachek kama umefika salama acha nikuache ulale upumzike.”
“Haya asante na wewe pia.”
“Lissa…”
“Abee…”
“You are that woman who made me fall uncontrollably.”
Alisema Leonard na kukata simu.
Lissa alibakia na tabasamu.

Alinyanyuka kitandani na kuelekea kilipo kioo alijiangalia huku akiweka mapozi ya kike kisha akaenda kwenye redio aina ya subwoofer.
Akawasha na kuanza kucheza taratibu akiwa mbele ya kioo.
“I said hakuna msamiati wa kushindwa kwangu, now that he fall for me.
Nitamchimba siri zake cha msingi nisiruhusu ni do nae, maana inawezekana akawa player akishapata anachotaka anasepa.
Natakiwa nimzungushe anipe siri kabla mambo hayajawa mengi.
Leonard you are over.”

Alijisemea Lissa kwa furaha.

Asubuhi alienda kazini kwake kumueleza bosi wake juu ya hatua aliyofikia.
Bosi wake alimpongeza huku akimuonya kuwa makini.
“Safari hii ni lazima tuujue ukweli nitakuwa nakujulisha hata kwa simu juu ya kila ugunduzi nitakao ufanya.”
Alisema Lissa na mzee huyo aliahidi kumpatia kila msaada atakae uhitaji.
Lissa alitoka ofisini kwa mkuu wake wakazi kuelekea ofisini kwake.
Alichukua simu yake na kukuta simu isiyopokelewa kutoka kwa Leonard.
Aliwasha data za internet na kuingia kwenye whatsapp.
Alimuona leonard akiwa hewani aliamua kumtumia text.
“Hi nimekuta missed call.”
“Hi nilikuwa na maswali kidogo si unajua mimi sio msomi kivile.”
“Eenhe niulize.”
“The opposite of you.”
“I”
“The opposite of hate.”
“Love.”
“The opposite of me.”
“You.”
Lissa alikuwa akiandika ujumbe kama Leonard alikuwa akifundisha mtoto.
Ndiyo ujumbe kutoka kwa Leonard ulipoingia.
“I LOVE YOU TOO LISSA”
Kwanza alishangaa na kujiuliza na akaelewa mara,
“Thank you Lissa.”
Kisha Leonard akaongeza ujumbe mwingine.
“Yaani daah.”
Lissa alishindwa cha kuongea.

Ukurasa wa mapenzi ukafunguliwa rasmi.
Leonard alionekana kuzama penzini na Lissa muda mwingi alitamani wawe wote hata alipoambiwa kuhusu kusubiri, alielewa.
Alimpeleka Lissa katika vitega uchumi vyake vingi.
Alimzuia kwenda klabu mara kwa mara na mara nyingi alikaa nae nyumbani kwake huko Mbezi beach.
Walienda klabu mara mbili kwa week tu.
Lissa alimchunguza sana Leonard lakini hakupata kiashiria chochote iwapo alikuwa mhalifu ama anajihusisha na magenge ya ujambazi na uuzaji wa madawa ya kulevya na ujangili kama ambavyo taarifa za ki-intelejensia zilivyodai.
Asubuhi hii wakiwa wamepumzika chumbani ndani ya nyumba ya Leonard simu ya Lissa iliita.
Simu hiyo ilikuwa upande alioko Leonard naye alichukua na kumpa Lissa.
Jina lilisomeka kama mkuu.
Lissa alimtazama Leonard kabla hajapokea simu hiyo baada ya kusita sita.
“Hello mkuu.”
“Niambie mwanangu unaendeleaje?”
“Niko poa za kwako?”
“Nzuri tu. Leo sijakuona ofisini.”
“Niko kwa boyfriend wangu.”
(Kwa ukali ) “Lissa mimi ni bosi wako hata kama umepewa kazi iliyowashinda wengine haimaanishi unikosee heshima.
Stupid.”
“Mkuu….”
“Fika kazini mara moja.”
Alisema mkuu na kukata simu.
Leonard alikuwa amesinzia na Lissa akamuamsha.
“Baby.”
“Vipi.”
“Ni huko chuoni huyu ni kiongozi wetu wa group la discussion.”
Alisema Lissa na simu iliita tena.
Alikuwa mkuu wake Lissa…
Leonard alikuwa akimtolea macho yaliyokuwa yakisema “mbona hupokei simu?”
Lissa alitamani kulia, aliona vile anavyoenda kushitukiwa.
Aliwaza endapo Leonard atamshitukia atamfanyaje.
Simu iliita mpaka ikakata ikaanza kuita tena na Lissa hakuonesha dalili ya kupokea.
Lissa pokea simu mbona hivyo?
Kiunyonge aliamua kuipokea.

Sehemu 3 Sehemu 5
0
0