Muonekano wa Giza:

Msaada

L and L (Msimu wa Kwanza) - Sehemu ya Saba (07)

“Honestly speaking niko kwako kik...”
“Noo…”
Leonard alimkatisha.
“Sihitaji unijibu leo nenda kafikirie Lissa I love you I can’t live without you.”
Leonard alilalama.
“Sina haja ya kufikiri hili lipo wazi mbona?
Nilianza kuja klabu ili niwe karibu na wewe.
Lengo langu kuanzisha uhusiano na wewe ili nikuchunguze lilifanikiwa.”

Leonard alifinya macho kwa uchungu asiamini anachokisikia kutoka kwa mwanamke yule aliyempenda kuliko mtu yoyote hapa duniani.
“So are you going to arrest me?”
Hatimaye aliongea kinyonge Leonard.
“No you are not a bad person…”
Leonard alimkatisha.
“I am… I am a bad person its just umeshindwa kwenye uchunguzi wako.
Yote ambayo umetumwa kwangu kuyachunguza ni ya kweli.”

Aliongea Leonard huku akikaa chini na kukipakata kichwa chake kwenye mikono yake akimlaani shetani kwa kuiharibu siku yake vibaya hivyo huku akiamini mambo hayawezi kuwa sawa tena.
Kwa upande mwingine Lissa masikio yake yalimuwasha kutokana na kile alichokisikia kwa Leonard.

"Leon...what did you just say? Did I hear you wrongly?”
Mwishowe Lissa aliuliza.
“You heard it right.”
Alijibu Leonard kwa kifupi.
“Leo… How…?! You… No bhana don’t joke.”
Alisema Lissa huku akishusha bastola yake aina ya berreta M9 chini.
“Ni kweli naongoza magenge ya uhalifu wanaoiba kwenye mabenk, malls, naingiza na kusambaza madawa ya kulevya na some shits ukitaka ushahidi nitakupa…”
Alisema Leonard akiwa kama hayupo kwenye akili yake.
Ni kama alisahau kama anauza siri za kambi kwa waasi.
“But Lissa I love you what are you going to do about it.”
Lissa alikuwa amekaa chini akiwa haelewi cha kufanya, cha kusema wala cha kuamua.
Mwishowe alipata cha kuongea.

“Tell me about it.”
“I have done it for years and I’m the one who notify police nachofanya nikuwapa taarifa za uongo zenye ukweli ndani yake na mimi huwezi kunitambua because siichafui mikono yangu nina watu sehemu nyingi na hata hawajui kuwa ni mimi ndo kiongozi wao.
Ile kampuni yangu ya furniture ni kama kivuli tu na shughuli zote zinazofanyika pale.
Na pale chumbani kwangu kuna mzigo inside those furnitures.”

Alijieleza Leonard.
Machozi yalimtoka Lissa alilia, alilia sana hakuamini kama angejikuta kwenye dilemma.
Na mwishowe alilia kwa kuufahamu ukweli uliomgharimu vitu vingi.
Kiunyonge alinyanyuka pale alipokuwa amekaa.

“Lissa niambie kama unanipenda despite of everything my love for you is real nitafanya lolote kwaajili yako please sikuambii cha kufanya but jua nakupenda.”
“I… I’m going to report and arrest you.
Hata nikupende kiasi gani mi nipo kazini na wewe ni mhalifu na mimi sipatani na wahalifu I’m sorry Leonard we are over.”

Alisema Lissa kisha akakimbia kutoka nje ya nyumba ya Leonard alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.
Alisita pale mbele ya nyumba kabla hajatoka nje ya geti na kupanda gari lake na kutokomea.

Alizunguka tu mjini huku akilia.
Alipoona kunakaribia kuchwa aliamua kwenda nyumbani kwake baada ya kuingiza gari ndani ya apartment ile yenye nyumba tatu za kuishi lakini ni mbili tu ambazo zina wapangaji.
Alibamiza mlango wa gari lake kwa hasira na kuingia nyumbani kwake.
Alipitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwake akatupa kila kitu kitandani na kisha akasogea mezani kwake.
Palikuwa na kompyuta yake ndogo (Laptop).
Alivuta kiti kukaa.
Pale juu ya meza pia palikuwa na ripoti aliyotarajia kuikabidhi siku chache zijazo.
Alichukua na kuiangalia akaanza kuisoma kuangalia jinsi alivyokuwa akimsifia Leonard kama raia mwema ambaye sasa alikuja kugundua kuwa siyo raia mwema tena.
Alianza kulia tena kwa uchungu alivyochanganyika na kukata tamaa.
Aliichana ile ripoti na kisha kufungua na kuwasha kompyuta yake na kuelekea sehemu ya kuandikia na kichwa cha habari kilianza...

RIPOTI…
Lissa alianza kuandika kwa hasira sana utasema alikuwa na ugomvi na kicharazio kile.
Aliandika kurasa 2 na nusu na alishindwa kuendelea aliangua kilio kwa sauti.
“Ooh Mungu wangu what should I do?”
Alilia akiongea maneno hayo.
Kila alipokuwa akiandika kuwa Leonard ni mtuhumiwa ilimuuma.
Kwa takribani miezi mitatu sasa amekuwa karibu nae na hakuona kiashiria chochote cha uhalifu na tayari alikwisha anza kuwa na mapenzi nae.
Leo hii Leonard amekiri mwenyewe kuwa ni mhalifu.
“Ananitania tu, Leo wangu jamani ni nini hiki? Uwii.”
Alilia Lissa.
“But do I have any choice than to report him?”
Alisema Lissa na kufumba macho yake.

Kumbukumbu za mapenzi mazito aliyokuwa akipewa na Leonard zilimjia na alihisi alitaka kuwehuka.
Alitamani kulia na kucheka kwa wakati mmoja.
Alifumbua macho yake na kukilaza kichwa chake pale mezani.
Kabla ya dakika moja kuisha Lissa aligutuka kana kwamba amekumbuka kitu.
Aliangaza huku na huko kabla ya kunyanyuka kwa kasi.
Aliukimbilia mkoba wake na kuujaza vitu vilivyomwagika akahakikisha bastola yake ipo ndani ya pochi na alitoka nje mbiombio na kuliendea gari yake kabla ya kuiweka kwa kazi na kuiondoa na kutokomea pasipojulikana.

Kwa upande wa Leonard toka Lissa alipoondoka alikuwa akinywa pombe kali kutoka kwenye kabati lililokuwepo hapo kwake.
“Nilisema sitamuamini mwanamke nikajisaliti na sasa mwanamke anaenda kuniangamiza.
Wanawake wana nini?
Aagh mama yangu alimkimbia baba yangu na kunitelekeza kwa baba yangu akaenda kuolewa na mwanaume mwingine mwenye hela uko.
Baba akaoa mke mwingine mwanamke alienitesa mpaka nikatoroka nyumbani hata sijui baba alipo sasa kama yupo hai.
I sweared not to trust any woman but Lissa…
Lissa alinifanya nikasaliti haya yote kumbe hakunipenda alikuwa kazini.
Nimemwambia siri yangu so nimekaa hapa namsubiri anikamate niishie gerezani kama bwege.
Daah women can destroy something they didn’t build.”

Akaongea kwa hasira sana Leonard.
Aliingiza mkono kwenye showcase na kutoka na bastola ndogo aina ya AMT hardballer.

“I’m going to kill myself siwezi ruhusu Lissa aje anikamate hapa.”
Alijiwazia kwa huzuni huku akiitazama picha ya Lissa iliyokua katika kuta aliyokuwa akiitazama pale sebuleni, kwa uchungu.
Bila kutarajia mikono milaini ilipita chini ya kwapa zake na kumbana kifuani.
“Leo… I love you.”
Lissa aliongea kwa sauti ya kilio iliyoonesha kuwa amekuwa akilia kwa muda mrefu.
“Kwa nini uwe mhalifu? Ukifungwa nitaishi na nani? Baby why?”
Lissa aliendelea kulia huku amemkumbatia Leonard kutoka nyuma.
Leonard alijinasua kutoka kwenye kumbato la Lissa akageuka na kumkumbatia tena.
“I’m sorry baby I never know if I would meet you ningeishi maisha yangu yote kama raia mwema nikikungoja.
Ukinipa nafasi I promise I’m going to quit everything and live everyday for you.
Nipende hata kama ni mhalifu.”

Lissa alilia.

“Nakupenda Leo kwanzia sasa na mimini mhalifu kama wewe I’m going to lie to the country and government.
I’m going to cover your sin and live with you forever.”

Aliongea Lissa kwa hisia baada ya kuacha kulia na kumkumbatia Leonard kwa nguvu.

Nusu saa iliyopita iliwakuta kitandani wakifurahia penzi wakiwa wahalifu rasmi wawili.
“Naenda kupeleka ripoti ile ya kwanza ila uache hizo mishe zako zote promise me.”
“I promise you nimeacha kwanzia sasa.”
Lissa alimtazama Leonard na machozi yalimtoka.

Sehemu 6 Sehemu 8
0
0