Muonekano wa Giza:

Msaada

L and L (Msimu wa Kwanza) - Sehemu ya Sita (06)

“As long as a I’m with you hautokuwa na mawazo I will give you anything you want nitakupeleka popote duniani.
Chochote utakachokisema nitakitenda.”

Alisema Leonard akiwa amemkumbatia Lissa.
“Hahah mimi niko kazini Leo,sio muda hutanipata tena.”
Lissa aliwaza.
“Thank you baby I’m so glad to have you.”
Leonard akambusu Lissa kwenye paji la uso.
Jioni hiyo walibakia hapo walikunywa, walipika pamoja na mambo mengi ya mahaba huku Leonard akiwa amevalia mavazi ya Lissa.
Walifanya kazi mbalimbali pamoja kama usafi, kupanga nyumba, kufua, kuosha vyombo na mwishowe wakaanza kunywa bia mpaka walipolewa.
“Jamani bia tamu.”
Alisema Leonard kwa sauti ya kilevi.
Walilala hapo hapo sebuleni mpaka asubuhi ambapo Leonard aliondoka na Lissa mpaka chuoni UDSM akamuacha pale na yeye akaondoka.
Alipopotea tu Lissa nae akapanda gari kwenda kazini.

Zilikuwa takribani wiki tatu za mapenzi moto moto baina ya Lissa na Leonard.
Walienda kufanya manunuzi mbalimbali na sehemu za burudani kuburudika.
Walitembea visiwa vya Zanzibar kufurahia mapenzi yao.
Leonard alimpeleka Lissa kwenye kampuni yake ya fenicha zinazotengenezwa nje ya nchi na kumtambulisha kama mkewe mtarajiwa.
Baadhi ya wafanyakazi walimshangaa kwani hakuwaga na habari na wanawake.
“Lissa mi ninapenda sana furniture, huwa nabadili kila baada ya miezi mitatu ndiyo maana umezikuta kule ndani mzigo mpya.
Ukija nitabadili hadi za kule kwako.
Hii ndiyo biashara yangu kubwa ukiachana na maduka niliyonayo.”

Leonard alimpa maelezo marefu Lissa.
Walisafiri sehemu mbalimbali kibiashara na Lissa alifurahia.

Mkuu wake wa kazi alikuwa akipiga simu kumuuliza kuhusu ripoti.
Ilionekana kama Lissa amejisahaulisha kuhusu kazi.
Baada ya wiki tatu kuisha Lissa aliamua kuandika ripoti ya kuthibisha kuwa Leonard ni mtu mwema anaefanya biashara zake kihalali pia alipanga kufikisha tamati mahusiano yake na Leonard.
Ni siku ambayo Lissa alikamilisha kuandika ripoti na alikuwa na furaha sana.
Hatimaye ameweza kufanya kazi yake kwa weledi na kwa mafanikio kuliko askari wenzake wote.
Aliamua kwenda kwa Leonard akafurahie kabla hajakabidhi ripoti ile na kuhitimisha mahusiano yao.
Ingawa alitoa taarifa kuwa yupo njiani kwenda lakini hakukuta mtu.
Alizunguka nyumba nzima bila mafanikio akatoka nje na kuangaza huku na huko.

“Leo is playing me, si nimemuambia nakuja.”
Alitembea kwa hasira kuingia ndani kuchukua pochi yake ili aondoke.
“Surprise.”
Alikuwa ni Leonard na hapo alipokuwa alikuwa amevaa kaptula tu huku kifua chake kikiwa wazi.
Pale Lissa alipokuwa akimtazama aliona mchoro ambao hakuwahi kuuona kifuani kwa leonard.
Ni maneno machache ambayo yalikuwa ni jina lake “Lissa”.
Hapo mezani palikuwa na keki kubwa iliyoandikwa “Our love is forever Lissa”, shampeni pamoja na vitafunwa vidogo vidogo.
Pia kulikuwa na boksi la zawadi ambalo Lissa hakujua lina nini ndani.
Lissa alikosa cha kuongea alimsogelea Leonard na kumkumbatia.

“I love you Leo.”
Akasema Lissa kwa hisia.
Ni kweli aliona kila sababu ya kumpenda Leonard.
Na alipowaza kumpenda Leonard aliona kuwa Leonard ni aina ya mwanaume aliyepanga na aliyetaka kuwa nae maishani mwake.
“He is innocent rich, loving, handsome and all kwanini nisiwe nae tu.”
“Ananipenda sana na mimi nahisi kumpenda pamoja na kwamba misheni imeisha mi nimekwisha kuamua kama naendelea nae.
I love him, mapenzi yake yanazidi kukua kila dakika ninayovuta pumzi.
I’m thanking god that I was able to get the love of my life.”

Aliwaza Lissa huku akiwa ametulia kifuani mwa Leonard akipapasa mchoro ama tatoo yenye jina lake hapo kifuani mwa Leonard.
Baada ya dakika kadhaa Lissa alijiondoa kifuani mwa Leonard na hafla fupi ya watu wawili ilianza.
Walifungua shampeni wakakata keki na wakala pamoja na vitafunwa.
“Inabidi tule chakula kizuri sana kama makange hivi.”
Alisema Leonard.
“Ngoja nikaandae.”
Akasema Lissa huku akinyanyuka.
Leonard alimtazama Lissa mpaka alipotelea jikoni huku akijisifu kwa kuchagua kifaa.
Wakati Lissa akiendelea kuandaa chakula huko jikoni Leonard alibakia sebuleni akiangalia televisheni iliyokuwa ikionekana miziki mbalimbali ya wasanii wa nyumbani.
Ndipo simu ya Lissa ikaita.
Leonard alichukua uamuzi wa kuichukua na kumpelekea simu kule jikoni kwani simu ilitoka kwa "mkuu" ambaye Leonard alimtambua kama kiongozi wa kundi lao huko chuoni.
Na pale alipokuwa akitoa simu, waleti ndogo ilianguka.
Leonard aliiokota haraka ili amuwahishie simu Lissa na hapo aliona kitu kilichomshitua hata akasahau habari ya simu tena.
Waleti aliyoiokota ilikuwa ni maalumu kwa kuhifadhia vitambulisho na hata pale alipokuwa akitazama aliona kitambulisho cha kazi cha Lissa.

“Ee bwana wee!! Lissa ni mpelelezi?!”
Alijiuliza mwenyewe kana kwamba anaweza kujithibitishia.
Simu ilianza kuita tena.
“Mkuu” alikuwa anapiga simu.
“Baby niletee simu yangu.”
Lissa aliongea kwa makelele huko jikoni.
Leonard huku sura yake iliyojaa mahaba ikabadilika, alipokea simu ile.
“Halo Lissa hongera jeshi la polisi linajivunia utendaji kazi wako tunaomba ukabidhi ripoti as soon as possible tuendelee na mambo mengine.”
Leonard alikata simu bila kujibu chochote.
“Leo mbona huniletei simu wakati inaita.”
Lissa aliongea huku akiwa ameinama hapo sebuleni katika unjia unaoelekea jikoni.
“Ooh simu yako hii hapa nimeshaongea naye tayari, alikuwa ni mkuu wako wa kazi.”
Akasema Leonard huku uso wake ukionesha kutokuwa na mzaha wowote.
Lissa alishituka sana hakutegemea Leonard kufahamu siri ile kwa wakati ule.

“Anakuambia ukakabidhi ripoti.”
Akasema tena Leonard na kisha akacheka kwa uchungu.
“I hope mtu uliyekuwa unampeleleza sio mimi.”
Kimya.
“Ni mimi?”
Kimya.
“Nijibu Lissa.”
Alisema kwa ukali Leonard.
Ni kama vile Lissa alitaka kuongea lakini alisita na kukwama kati ya kuchagua kuongea ama kutoongea.
“Umegundua nini kwangu eeh?”
Leonard aliuliza huku akitegemea kutojibiwa.
“Nilijua tu we sio mtu wa klabu wala ulevi ulikuja ili unichunguze.
You changed your life style ili unipate.
Sikujua hayo yote and I fall for you blindly.
Tell me ulichogundua we mwanamke.”

Aliongea kwa ukali Leonard na Lissa alibakia amegwaya.
Leonard alikuwa akizunguka huku na huko huku akiwa amechanganyikiwa.

Aliokota chupa ya mvinyo na kuibamiza ukutani nayo ikapasuka vipande vipande.
Lissa alibakia akitetemeka asijue ni kitu gani ambacho Leonard angemfanya kutokana na hasira alizonazo.
Bila ya kuchelewa Lissa alikimbilia ilipo pochi yake na kutoa bastola yake aina ya berreta M9 wakati Leonard akiwa amegeukia ukutani akijitahidi kushindana na machozi yaliyolkuwa yakimtoka na alipogeuka alikuta bastola ikimuangalia.
“Easy Lissa.”
“We sio mhalifu usinifosi nifanye kitu kibaya.”
Lissa alitema cheche.
Machozi yalikuwa dhahiri usoni kwa Leonard.
“But why Lissa, mbona sielewi?
Anyway I don’t care kama umenidanganya kama wewe ni nani just tell me unanipenda na haupo kwangu kikazi.”

Sehemu 5 Sehemu 7
0
0