Angel - Sehemu ya Kumi na Tatu (13)
Agnes akaita kwa sauti kidogo mpaka Angel akashituka!
“Naomba kikapu mi nitangulie nyumbani.”
Akaongea Angel...
Agnes akaishia kumtizama huku nyuso zake zikionekana wazi alitaka kumcheka!
Mara wakiwa pale akatokea mwanaume mmoja hivi akitokea ndani ya mgahawa huo.
“Agyy!!”
Akaita mwanaume huyo kwa sauti yake kubwa yenye kibesi.
“Waooo! Mpenzi umejuaje kama nilikuwa nakungoja kwa hamu sana hapa?”
Akaongea kwa kudeka Agnes.
Angel akabaki ameduwaa.
Hakika ilikuwa ni zaidi ya maajabu.
Mwanaume mwenye zaidi ya miaka arobaini kutembea na mschana mdogo kama Agnes ambae umri wake si zaidi ya miaka kumi na sita.
“Ninajua na ndiyo maana sijakawia tangu nimepata simu yako kuwa unaningoja hapa nje.”
Akajibu mwanaume yule.
“Sawa ni vizuri sana baby.”
Akaendelea kudeka Agnes.
“Na huyu hapa je?”
Akauliza mwanaume huku akimtizama Angel.
“Huyu ni rafiki yangu nimekuja nae.”
Akajibu Agy.
“Aha! Shem za kwako?”
Mwanaume huyo akamsalimia Angel huku akimpatia mkono.
“Salama shikamoo.”
Akajibu huku akinesa kabisa baada ya kuupokea mkono ule.
“Safi tu.”
Akajibu mwanaume huyo kwa kuitikia “Safi tu” baadala ya “Marahaba” kama alivyosalimiwa!
Makubwa!
“Sasa?”
Akauliza mwanaume huyo akimuuliza Agnes.
“Twende.”
Akajibu...
“Na huyu je?”
“Huyu nishamwelekeza kila kitu kwahiyo hakuna tatizo.”
Akajibu Agnes.
“Twendezetu… Shem twende.”
Akamshika mkono Agnes wakawa wanaelekea ndani.
Angel hakuwa na chaguo tena, ilibidi afanye vile alivyokuwa ameambiwa na Agnes kwani kikapu hakumpa.
Labda angeweza kurudi nyumbani lakini kwa wakati huo haikuwezekana kwani kapu lililokuwa na mazaga zaga waliyotumwa
kuyanunua sokoni lilikuwa na Agnes sasa angefanyaje?
Hakuwa na namna.
Wakafika mpaka kwenye ukumbi mkubwa ulio ndani ya mgahawa huo.
Aise kulikuwa kumechangamka balaa!
Mziki wa taratibu ujulikanao kwa jina la (Love is weekend) ulikuwa ukidunda taratiiibu ndani ya ukumbi
huku watu wenye pesa zao wakila burudani.
Bonge la burudani bila shida!
Angel baada ya kufika mule ndani alianza kuyasabahi mazingira yale kwa makini pamoja na kuwatizama wale wote waliokuwa mule ndani.
Katika uchunguzi wake aliweza kugundua kuwa ule haukuwa mgahawa kama alivyodai Agnes bali ilikuwa ni bar ya
watu matajiri sana ndiyo waliokuwa wakipata vinywaji mule na ndiyo maana kulikuwa tulivu sana.
“Hii ni bar!”
Alijisemea Angel huku akitafuta namna ya kutoka.
Hakuchelewesha pale pale aligeuka nyuma na kutoka nje kisha akatokomea kabisa huko.
Bahati nzuri hakuna mtu aliemfuata kwa sababu wengi walikuwa bize na grass zao.
Agnes nae tangu aingie na mtu wake hakuonekana tena.
Wazo alilokuwa amelipata Angel kichwani kwake ni kurudi nyumbani na iwapo Rebeca angerudi na kukuta kile walichoagiza
hakijatekelezwa basi angekuwa na kisingizio.
Aliona ni afadhari kurudi nyumbani kuliko kubaki maeneo hatarishi kama yale.
Sasa bwana kikaja kumkost kitu kimoja.
Angel alipotea njia ya kurudi kule anakoishi shangazi yake Rebeca.
Hii ilitokana na ugeni alikuwa hajayakariri mazigira vizuri kwahiyo huo ukawa ni mwanzo wa yeye kupotea.
Angel sasa alianza kuzunguka zunguka ovyo bila ramani yoyote...
Yaani alizunguka sanaa!
Mpaka inatimu saa sita kamili mchana tangu asubuhi bado Angel alikuwa akizunguka zunguka ovyo ndani ya Temeke bila
mafanikio ya kufika kule alikotakiwa kufika.
Katika kuzunguka zunguka alifika sehemu moja ambapo kulikuwa na bomba la maji.
Pale bombani alikwepo bibi mmoja akikinga maji kwenye bomba lile.
Angel akili ikamtuma kuwa yule bibi angekuwa ni msaada kwake, alichokifanya ni kupita pale bombani.
Lengo lake lilikuwa ni kujaribu kumuuliza kama anapafahamu mahali alipokuwa akiishi mama mmoja aitwae Rebeca.
“Bibi shikamoo.”
Angel alimsalimia bibi huyo kwa heshima zote pindi alipokuwa amefika hapo bombani.
“Marhaba mjukuu wangu.”
Bibi huyo akajibu...
“Bibi samahani...
Eti utakuwa unapafahamu mahali anapoishi mwalimu mmoja wa kike anaefundisha secondari aitwae Rebeca?”
Bila kupepesa Angel alienda kwenye point moja kwa moja.
“Hata simjui mjukuu wangu kwani una shida gani nae?”
Akajibu na kisha kumuuliza swali tena.
“Nilikuwa na shida nae nyumbani kwake bibi.”
Akajibu Angel huku akiwa kapoa mno.
“Hapa cha kukusaidia mjukuu wangu jaribu kuonana na wanafunzi wake watakusaidia.”
Bibi akasema.
“Lo! Bibi kanikumbusha kitu muhimu sana jamani.”
Angel alijisemea moyoni huku akifurahia sana.
Kama Angel angelipata wazo hilo mapema basi angekuwa amekwishafika muda sana nyumbani kwa shangazi yake
kwani kama ni wanafunzi alikutana nao wengi sana barabarani ila tatizo hakukumbuka hilo.
“Bibi asante sana nashukuru nitawauliza na nitafika.”
Angel akamwaga bibi yule huku akitaka kuanza kuondoka.
“Haya.. Lakini naomba unitwishwe kwanza.”
Bibi akasema...
“Anhaa... Sawa bibi yangu.”
Angel akasogelea mahali pale na kumtwisha yule bibi kisha wakatawanyika kila mtu akaelekea kule anakopaswa kwenda.
Angel alitembea sana huku akiomba sana kukutana na wanafunzi ili aweze kuwauliza mahali anapoishi mwalimu wao Rebeca
ambae ni shangazi yake.
Naam katika harakati zake alibahatika kukutana na wanafunzi watatu wa kike wakiwa na mabegi yao wakirejea majumbani
kwao mdogo mdogo baada ya masomo...
“Hi.”
Aliwachangamkia...
“Hi kwako! Vipi?”
Nao pia walichangamkia kama alivyowachangamkia...
“Njema za shule dada zangu?”
Angel aliwapa heshima yao kwani kweli wale walikuwa ni kinadada kwake maana wao walikuwa Form two yeye darasa la tano labda
kwenda la sita, kwahiyo walikuwa wamemzidi kidogo.
“Za shule kwetu ni njema, sijui wewe mwenzetu?”
“Za kwangu ni nzuri...
Samahanini nina shida kidogo.”
Akaongea Angel.
“Karibu, ni shida gani hiyo mdogo wetu?”
“Nina shida na mwalimu Rebeca naomba kujua nyumbani anapoishi.”
Angel akasema.
Kusikia vile wale wanafunzi walitizamana kwanza.
Unaweza pia kusoma: