Muonekano wa Giza:

Msaada

Angel - Sehemu ya Kumi na Tano (15)

Angel aliwaka kama mbongo.
Pale pale akambetua Agy kwa nguvu kisha akambeba juu juu kama karatasi lengo lake aende akamtupe kwenye jiko la mkaa lenye moto.
Lakini kabla hajatekeleza kitendo hicho, mlango wa jikoni ulifunguliwa kwa nguvu, Rebeca akajaa!
“Yaani mshushe chini mwenzio kabla sijakuharibu sura sasa hivi.”
Rebeca alifoka mithili ya kobla amwonapo binadamu katika himaya yake!
Angel nae baada ya kufanya kile alichoagizwa yeye akabaki akimtizama shangazi yake usoni kama sanamu.
“Angel nimesema mshushe mwezio hauskii?”
Rebecca aliwaka kwa sauti.
“Sikuwahi kufikiria kama shangazi unaweza kuwa na mambo ya ajabu kiasi hiki.”
Kutokana na hasira kali alizokuwa nazo Angel alijikuta akibwatuka maneno mabovu yaliyokwenda moja kwa moja kutibua sumu kali ya Rebecca mahali ilipolala.
“Umesema..?”
Rebecca alihoji kwa sauti kavu huku akimsogelea Angel kwa ukaribu zaidi.
“Sikuwahi kufikiria kama shangazi unaweza kuwa na mambo ya ajabu kiasi hiki.”
Angel alirudia!
“We mbwa unajiamini nini ee?
Mimi ndiyo wa kuniambia ujinga, mimi?
Ndicho ulichofunzwa na babu yako siyo?”

Rebecca aliwaka kama mbogo.
Angel akabaki akimtizama tu...
“Mshusheee!”
Akamshusha, kisha Agnes akaondoka zake na kuwaacha wawili huko jikoni...
“Nimepata taarifa zako kuwa wewe ni malaya sugu kabisa, kwanza kukusomesha wewe unaweza kuwa ni upotezaji wa pesa usio na faida!”
Rebecca aliongea maneno yaliyokwenda kumgusa vilivyo Angel.
Kwanza hakuwahi kutegemea hata siku moja kama Rebecca angekuja kumwambia maneno ya kuumiza kiasi hicho.

“Shangazi mimi ni malaya? Mimi?”
Angel aliongea kwa uchungu mno.
“Ndiyo! Wewe ni malaya tena usie na haya!”
Dooh!
Maskini Angel alianza kulia kabisa ni kwa kiasi gani inaumiza hii mtu humjui hata mwanaume leo hii unaambiwa wewe ni malaya tena usie na haya?
Kwanza Angel alipandwa na hasira za gafla!
Mpaka akajikuta akilopoka kwa kusema...
“Shangazi mimi siyo malaya tambua tu hivyo na simjui mwanaume tangu nizaliwe kwahiyo wewe kama haupo tayari kuitimiza ahadi yako naomba nirudi Morogoro kwa bibi na babu.”
Akasema Angel huku akiendela kudondokwa na machozi.
“Morogoro hautorudi kaa ukijua hilo kabisa!”
Alipokwisha kusema hayo Rebecca aliondoka kabisa na jikoni akamwacha Angel akiwa kaduwaa peke yake kama msukule.

“Haya ndiyo maisha ninayokwenda kuishi mimi Angel lo!”
Angel alianza kufikiria mengi sana hata akaanza kuyakumbuka maneno ya marehemu mama yake siku moja baada ya chakula cha usiku enzi za uhai wake.
Alikumbuka aliwahi kumwambia kuwa...
“Dunia ya sasa haina usawa, dhuruma ndiyo imekuwa habari ya mjini.
Unakuta mtu anamdhurumu ndugu yake wa damu kabisa kwa kumfanyia vitendo vya kikatili kama vile kumbaka, kumdhurumu mali zake na hata haki zake za msingi.
Kwahiyo dunia ya sasa hivi haina cha ndugu wala nani, ndugu wa kuaminika sasa hivi ni mzazi wako pekee!
Angel mwanangu nakusihi sana, sasa hivi unakua mtu wa kwanza kuepukana nae ni “Mwanaume”, wanaume ni watu wabaya sana katika hii dunia lakini pia ni watu wazuri sana katika hii dunia...
Uzuri wao ni kwamba wakikutana na mwanamke mwenye kuwa na msimamo basi wanapenda kweli na hufanya nao malengo...
Na ubaya wao ni kwamba, wakikutana na mwanamke ambae hana msimamo, hajatulia na hajitambui basi wao huchukulia hiyo ni kama fursa kwao kufanya nae starehe za masaa kila wakijiskia.
Wapo tayari hata kumhonga pesa kwani wanatambua kuwa pesa hutafutwa na thamani ya mtu haitafutwi.
Mwanamke akishashushwa mbele ya jamii kuwa huyo ni “malaya” basi tena thamani yake imeshashushwa na keshadharaulika jumla!
Kwahiyo ndiyo hivyo, nakusihi sana mwanangu usije ukajishusha heshima yako kwa kumsikiliza mtu yoyote katuuuu...”

Baada kumbukumbu hiyo Angel akashusha pumzi ndefu Kisha akageuka huku na kule kuona kama kulikuwapo na mtu mwingine pale jikoni lakini akabaini kuwa alikuwepo yeye pekee.
“Sitoweza kumsikiliza mtu yeyote kamwe, Mungu nisaidie katika hili niepushe na mabaya yote dhidi yangu amen.”
Yalikuwa ni mawazo ya mschana Angel.
Akatoka kule jikoni, hata kula alikuwa hajala vizuri kwani kama unakumbuka kulitokea varangati basi hali ile ilipelekea hata njaa kufa.
Chakuka akakiacha kama kilivyo.
Basi taratibu siku ikawa inaisha kihivyo ndani ya nyumba hakukuwa na mazungumzo tena kati ya Angel, Agnes na Rebecca.
Kiufupi ni kama walimnunia vile.
Angel hakujali nae alikaa kivyake alijua kuna muda hasira zao zitaisha na kila kitu kitakwenda sawa kama kawaida...

Siku hiyo ikaisha na hatimae siku ya pili ikawadia.
Bado bifu liliendelea Angel hakujua ni kwanini Rebecca aliamua kuwa katika hali ile?
Hata kama ni chuki je, ni chuki za aina gani hizo?
Hakujali akaendelea kufanya kazi zilizombidi kama vile kufagia uwanja n.k
Asubuhi hiyo Rebecca kama kawaida yake alijiandaa na kuelekea kazini huku maagizo yote akiwa amemwachia Agnes pasipo kumshirikisha Angel kama siku iliyopita.
Pia Angel hakujali kwanza aliona ni kama amempunguzia mzigo fulani kwani hata yeye hakutaka kuambataba na Agy mahali popote pale.
Kwanza alienda zake chumbani, kuna kitu alikuwa amekumbuka kwenye begi lake sasa alikwenda kukiangalia kama kipo?
Kwani ni siku nyingi kidogo tangu akiweke humo begini sasa leo kakikumbuka basi akaona si mbaya aende kukiangalia.
Mara mlango ukagongwa!
“Ngo! Ngo! Ngo! Ngo!…. We Angel unalala saa hizi kwani umesahau kama tunakwenda sokoni?”
Alikuwa ni Agnes...
“Sikujua kama naenda kwani sikuambiwa.”
Angel akajibu.
“Usiende ukiwa kama nani?”
Agnes akajibu kishari shari.
“Aya nakuja.”
Angel akaamua kuwa mpole tu.
Haraka haraka akavaa nguo nzuri nzuri pamoja na viatu pia kisha akatoka akiwa tayari kwa safari ya sokoni akiwa na Agnes.

“Hivi Agy.”
Angel aliita wakati huo wakiwa njiani...
“Nini?”
Agnes akaitikia kwa dharau.
“Kwani kosa langu ni nini kwako?
Kwanini unapenda kunikera?
Kwanini unanidharau?”

“Kwahiyo watakaje labda?
Unataka nikunyenyekee kama bosi wangu ama?”

“Sina maana hiyo Agy.”
“Ila una maana gani?”
“Maana yangu ni kwamba ninahitaji mimi na wewe tuwe kitu kimoja, tupendane, tuheshimiane ili tuheshimike pia.”
“Hahaha… Ulichokizungumza ni sawa sawa na pumba iliyochanganywa na mashudu kwahiyo hata hujaelewaeka umezugumza nini?”
Agnes aliongea kwa nyodo na dharau kibao huku akibetua na mdomo juu...
“Ok sawa asante kwa jibu lako zuri nimelipenda.”
Angel alijibu kisha wakaendelea na safari yao.
Kiukweli jibu hilo lilimuuma sana Angel aliumia mno ila hakuwa na namna kwani alimuanza yeye hivyo ikambidi atulie tu.

Sehemu 14 Sehemu 16
0
0