Muonekano wa Giza:

Msaada

Angel - Sehemu ya Pili (02)

Maskini Angel mama yake alikuwa amekufa kitambo sana, alifariki usiku wa kuamkia siku hiyo!
“Haaa!! Mama umekufa? Hebu acha utani bwanaa.”
Angel alisema kwa sauti huku akimtikisa kwa nguvu.
Lakini wahenga walisema maji yakishamwagika... Hayazoleki na ndivyo ilivyokuwa Mama yake Angel hakuwa hai tena hivyo ilikuwa ni lazima Angel akubaliane na hali halisi...
Hakika ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa binti Angel alishindwa kujua aanzie wapi aende wapi?
Hatimae alianza kuzunguka zunguka ndani ya nyumba huku akipiga makelele kama mwehu.

Mayowe yale yaliweza kuwashitua majirani ambapo nao baada ya kusikia mayowe hayo walimiminika nyumbani kwa bwana Taison kuona nini kinatokea!
Hatimae wanafika!
Angel anaarifu kuwa mama yake alifariki usiku!
Kila mmoja anashika kinywa chake, watu wengi sana walihuzunika sana!
Bi Anneth hakutakiwa kufa kabisa kwa sababu alikuwa ni mama mpole sana na alikuwa mkarimu mno kwa majirani na ndiyo maana walimpenda sana kwahiyo kifo chake kilizua simanzi kubwa sana hapo mtaani.
Sasa kitu cha ajabu kilichokuja kuushangaza umati huo wa watu uliofika nyumbani hapo ni kwamba bwana Taison hakuwepo mpaka wakati huo na hata walipojaribu kumpigia simu nayo pia haikupatikana!
Majirani ilibidi wamuulize Angel kwa kuhisi wenda anafahamu ni wapi baba yake alipo...

JILANI: “Angel kwani baba yako yuko wapi?”
ANGEL: “Sijui.”
JILANI: “Haujui? Kwani hajaaga?”
ANGEL: “Aliondoka tangu jana asubuhi, pia aliaga na kuahidi kuwa angerudi, lakini hakurudi.”

Ukweli ulibaki pale pale kuwa Bwana Taison tangu alivyoondoka jana hakurejea tena.
Je kwanini hakurejea?
Sasa hebu turudi nyuma kidogo...
Katika kipindi chote ambacho mama Angel alikuwa akisumbuliwa na Saratani, mumewe Taison alihangaika sana.
Alimtembeza katika mahospital makubwa karibu yote nchini lakini wapi Anneti hakuonesha dalili zozote za kupona.
Mara ya mwisho kumhangaikia mama huyo ilikuwa ni katika Hospital ya OCEAN ROAD iliyopo Dar es salaam.
Anneth alipatiwa barua ya kwenda OCEAN ROAD na Hospital ya rufaa ya mkoa wa Mbeya kuwa waende huko kwani hali ya mama huyo ilizidi kuwa mbaya kila uchwao.
Taison hakukata tamaa, aliandaa pesa ya kutosha kisha wakafunga safari mpaka Dar es salaam.
Huko walipokelewa vyema.
Baada ya muda kidogo walifanikiwa kuonana na madaktari, ambapo kabla ya mazungumzo meengi Taison alitoa barua aliyokuwa ametoka nayo huko Mbeya.
Daktari anapokea na kuanza kuisoma, baada ya muda mfupi akasema.

DAKTARI: “Hili ni tatizo kubwa inatakiwa lichunguzwe na daktari mmoja nguli kutoka Berlin.”
TAISON: “Berlin?”
DAKTARI: “Yah!”
TAISON: “Sasa ndugu yangu nitawezaje kufika huko?”
DAKTARI: “Sikuwa na maana uende huko! Yupo hapa, utapelekwa!”
Daktari huyo alijibu...

Taison alizidi kuchanganyikiwa vibaya sana kwani kila Hospitali aliyokwenda alikutana na maneno ya aina hiyo kuwa mkewe alikuwa na hali mbaya sana!
“Oooh! Mungu baba ingilia kati.”
Zilikuwa ni dua za mwanaume huyo alizokuwa akizipiga muda wote...
Haikupita muda mrefu, Anneth alichukuliwa na jopo la madaktari kadhaa huku Taison akiambiwa amsubili katika ukumbi wa mapumziko.
Angeletewa majibu baada ya vipimo.
Hakubisha, alikubaliana nao, kisha akamshika mkewe mkono na kumtizama kwa sekunde kadhaa kisha akamwachia madaktari wakaondoka nae.
Taison alisubili kwa muda mrefu sana bila madaktari kurudi hata akaanza kupatwa na wasawasi lakini kumbe...

DAKTARI: “Aisee! Pole kwa kusubili kwa muda mrefu.”
TAISON: “Aah! Hakuna shaka doctor kazi nzuri inahitaji muda!”
DAKTARI: “Ni kweli… Sasa unasikia Mr nani?”
TAISON: “Taison.”
DAKTARI: “Oky! Ndugu ulikuwa wapi kipindi choote hiki kumuwahisha mgongwa wako kwenye matibabu?”
TAISON: “Yaani ndugu yangu huwezi amini nimetembea mpaka bugando, nina makaratasi yote ya Hospital zaidi ya 30! Ambazo nimezunguka!”
DAKTARI: “Aisee! Sasa mbona tatizo limekuwa kubwa kupita usalama?”
TAISON: “Una maana gani Doctor?”
DAKTARI: “Haponi huyu.. Usihangaike nae tena ndugu!”
TAISON: “What?! Doctor hebu nitolee ujinga wako hapa sawa?”
DAKTARI: “Sikiliza kaka… Hii ni kwa faida yako mwenyewe! Sawa?
Sijataka Hospital ikuchukulie pesa yako isiyo na faida ingali hali ya mgongwa imeshaeleweka...
Sijui unanielewa?”
Aliongea daktari huyo huku kijasho chembamba kikimtililika kutokea kwenye nywele mpaka mashavuni na nyuma ya kichwa...
Yaani kisogoni na kuchuluzikia shingoni.
TAISON: “Sijakuelewa ndugu Daktari.”
DAKTARI: “Oky! Naomba unisikilize kwa makini...
Mkeo kwa hali aliyonayo sasa hivi hawezi kupona tena kwani Saratani amekwisha jenga na wadudu wamekwishasamba mpaka kwenye kibofu cha mkojo na maeneo mengine hivyo basi muda wowote atapoteza maisha...
Pole kwa hilo Mr Taison.”
Aliongea kwa msisitizo Daktari huyo kuonesha kile alichokuwa akikizungumza hakikuwa na hata chembe ya utani...

Hapo sasa ndipo bwana Taison alipoona kama Dunia imemgeuzia matako.
Mengi alianza kuyafikiria kichwani kwake.
“Hivi ni kweli Anneth unakwenda kuniacha? Dooh!!”
Alihuzunika mno Taison hata akayachukia maisha yake na kuyashutumu kwa adhabu aliyopatwa nayo kupitia maisha jayo…
Basi Mwanaume huyo hakuwa na jinsi tena zaidi ya kumtoa mkewe Hospitalini na kumrudisha nyumbani kwao mbeya...

Siku tatu zilikatika tangu warudi kutoka Dar es salaam.
Anneth yeye hakuambiwa chochote na madaktari hao zaidi ya kumzuga zuga kuwa tayari walishawasiliana na mumewe na kuna utaratibu walikuwa wamempatia jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote.
Sasa katika siku zile tatu Taison alionekana kutokuwa sawa kabisa.
Yaani alikuwa ni mtu aliepoa kila wakati, yaani alionekana ni mtu aliekuwa na simanzi kubwa sana moyoni.
Anneth mke wake alimshtukia akamuuliza jioni moja baada ya chakula cha usiku...

ANNETH: “Mume wangu, siku hizi unaonekana wazi kabisa kukosa furaha tatizo nini?”
TAISON: “Hapana mke wangu! Nipo sawa… Isipokuwa kesho nina kasafari kidogo!”
ANNETH: “Wapi tena mume wangu! Huniambii muda wote sasa hivi ndiyo waniambia baada ya kukuuliza jambo!”
TAISON: “Noo! siyo hivyo…. Nilipanga kukuambia sasa hivi...
Hata hivyo ni fupi ya kwenda na kurudi...”
ANNETH: “Hakuna shida…. Halafu pia Madaktari…”
TAISON: “Nitakuja kukueleza nikirudi.”
Taison alimkatisha mkewe kwani alijua anataka kuuliza nini...

Kwa sababu Anneth alikuwa ni mgonjwa mgonjwa, mada haikuwa ndefu, walipanda kitandani wakalala...
Hatimae siku ya pili yake, asubuhi na mapema, bwana Taison alijiandaa asubuhi asubuhi na kuondoka bila shaka ilikuwa ndiyo ile safai aliyokuwa amemuahidi mkewe!
Lakini tangu alivyondoka asubuhi hiyo, mpaka mkewe anakutwa na mauti hakurudi tena!

Mpaka mazishi ya Bi. Anneth yanafanyika na kumalizika mumewe hakurejea tena!
Hakika hii ilikuwa ni zaidi ya kituko!
Angel ndiye aliepata tabu muda wote kwani watu wengi hususan ndugu walimuhoji sana kutaka kujua kama ulitokea ugomvi kabla ya baba yake kuondoka?
Hilo kwake lilikuwa ni jibu la wazi kabisa kuwa hakuna ugomvi wowote ulikuwa umetokea kabla ya baba yake kuondoka hapo nyumbani siku tatu zilizopita.

Sehemu 1 Sehemu 3
0
0