Muonekano wa Giza:

Msaada

Angel - Sehemu ya Ishirini na Tatu (23)

“Asante nashukuru.”
Simu ikakata.
Rebeca akaacha msonyo wa nguvu kisha akasema.
“Umenikimbia? Sasa nitakutafuta nitakukamata na nitakuweka ndani kwa kudai umeniibia mjinga wewe.”
Alikuwa ni Rebeca ndiyo alikuwa akijisemea maneno huku apiga hesabu za kuelekea bafuni.

Upande wa pili...
Angel baada ya kutoroka usiku ule alitembea umbali mrefu sana mpaka inatimia saa sita kasoro usiku alikuwa sehemu ambayo hata hakujua ni wapi?
Lakini ilikuwa ni sehemu ambayo ilikuwa na makazi kama kawaida, kutokana na dhahama alizokumbana nazo usiku huo ikichangia na mwendo aliotembea mpaka kufikia hapo alikuwa amechoka mno.
Alitamani angepata sehemu walau alaze ubavu wake.
Katika pita pita zake aliweza kukutana na jumba bovu sehemu moja hivi.
Jumba hili lilikuwa maeneo ya kati kati ya mtaa na lilionekana kutokuwa na kiumbe yeyote ndani.
Akili ikamtuma aingie humo ndani apumzike walau kukuche.
Bila kusita akaingia!
Mwanga wa mataa ya umeme yaliyokuwa yakiwaka nyumba za jirani yaliweza kupenya ndani ya jumba hilo kupitia madirishani na hata baadhi ya nyufa zilizokuwa zimepasuka ukutani mwa jumba hilo.
Mwanga huo uliweza kumsaidia kuona ndani aendako.
Humo ndani bwana kulikuwa na mabox yaliyotandikwa tandikwa ovyo ovyo tu bila mpangilio wowote!
Bila hata kufikiria chochote Angel alijitupa kwenye mabox hayo na usingizi mzito ukamchukua...
Fofofo!!

Kumbe!
Lile jumba lilikuwa ni geto la wahuni na vibaka wa mji na wakati ule Angel anafika pale wao walikuwa wameondoka kwenda kutafta riziki huko mitaani...
Unaona mambo hayo?
Baadae si wakarudi bwana!
Kufika mlangoni mhuni mmoja akapata kunusa harufu ya mafuta ambayo kwake ilikuwa ni ngeni kabisa...
“Shiiiiii.”
Akawasimamisha wenzake.
“Vipi?”
Mmoja akauliza kwa sauti ya chini sana.
“Aise! Hebu tufanye uchunguzi kwanza maana nahisi kama geto limeingiliwa vile.”
“Eeh!”
“Umesema?”
“Vipi kuna upepo wa polisi nini?”
Kila mmoja aliuliza swali lake wakati huo wakisogeleana zaidi ili wapate kujua mwenzao kahisi nini.
“Asee hebu mulika huko ndani kwanza.”
Akanong'ona.
Tochi ya mwanga mkali ikapigwa ndani...
Alaaa!
Kwanza walishituka!
“Mtu...mtu...mtu.”
Mhuni moja alisema huku akijiandaa kukimbia kabisa.

“Hebu tulia.. Lete tochi hiyo kwanza.”
Mmoja kati ya wale vibaka alisema huku akivuta upanga wake aliokuwa ameuchomeka kwenye surali.
Akapewa tochi kama alivyotaka.
Taratibu akaanza kupiga hatua za tahadhari kumsogelea Angel wakati huo akimulika mulika kila kona ya nyumba kuhakikisha usalama kwanza.
Akamfikia.
“Aaaaah! Washkaji ee? Nyapu imekosea geto mkuje tumpige mtungo wa maana huyu.”
Yule mhuni alibwatuka hivyo baada ya kubaini kuwa yule aliekuwa pale ni mschana na mbaya zaidi alikuwa katika usingizi mzito, na begi lake likiwa pembeni.

Licha ya mhuni yule kuongea kwa sauti wakati akiwaita wenzake bado Angel hakuweza kuzinduka usingizini hii ni kwa sababu ya usingizi mzito uliokuwa umemchukua!
Wale wengine kusikia kuna mschana alikuwa ndani ya geto lao wakajua leo ndiyo leo.
Yale manyege ya miaka yote wanakwenda kuyatua kwa huyo manzi aliekosea geto.
Wote kwa pamoja wakamsogelea…!
“Oya! Oya.. Sasa tuheshimiane nitaanza mimi mkubwa wenu sawa?”
“Hebu acha kuleta noma mzee uanze wewe kivipi asee?”
“Yaani mkileta uzwazwa hapa mi nazama barabara ya vumbi.”
“Afu na we dogo acha kuleta mizinguo, huko ndiko ninakokupigia mahesabu mimi na ndiyo maana unaona niko kimya!”
Walianza kurumbana kuhusu nani aanze...
Na hapo ndipo walipokuja kukosea sasa.

Makelele ya kurumbana kule yakapelekea Angel atokwe na usingizi...
Sasa kufumbua macho anakuta kesha zingirwa na vibaka!
“Ooh! Mungu wangu Angel mimi nimepotea kweli yaani kumbe hii ni nyumba ya watu?
Maskini mimi.”

Angel alianza kujilaumu kwa kuingia mle ndani sasa ndiyo anatambua kama lile ni geto la wahuni.
Akainuka na kukaa kitako...
“Oya oya dada mambo vipi? Naitwa bakari unaj……”
Mwenzake akamkatiza kabla hajamaliza kuongea...
“Toka uko.. Unataka kuongea nini we fara?”
Alimsukumia mwenzake pembeni kisha yeye akamsogelea Angel na kumshika matiti mazima mazima.
Alipotaka kumsukumia Angel chini ili alale chali mwingine akamuwahi.
“Hebu acha uk**ma hapa...
Unamshika huyo demu ukiwa kama nani?”

Hapo sasa vurugu zikazuka.
Wababe wawili walikamatana ndani ya jumba hilo katika harakati za kumgombania Angel unaambiwa zilianza kupigwa ngumi za uhakika, wahuni wengine waliosalia wakabaki watizamaji.
Angel bwana ni mschana mjanja sana...
Pale pale akapata wazo!
“Hii ndiyo nafasi yangu ya pekee!
Nikibugi hapa imekula kwangu hawa vibaka watanibaka tena siyo kidogo.”

Alijisemea Angel huku akiendelea kukamilisha mpango wake kabambe kichwani wa kufanya tukio la kustaajabisha litakalowaacha vinywa wazi vibaka hao.

Wakati ugomvi ukiwa umepamba moto kati ya wale vijana wawili.
Pale pale Angel alifanya kituko cha ajabu kabisa!
Unajua alifanyaje?
Kwanza aliyatembeza macho yake katika kila uso wa vibaka watazamaji...
Akaona ni kama hawajamtilia maanani vile wao walikuwa wakiangalia ngumi na si kingine.
Pale pale Angel akakwapua begi lake na kupita nalo dirishani kama upepo kwanza hakuna hata aliemwona!
Kuna mhuni mmoja tu ndiyo alihisi kuondoka kwa mschana huyo ingawa hakuona vizuri.
Sasa ikabidi ahakiki kwa kutizama mahali alipokuwa amekaa!
Macho yake yanaambulia kuona mabox pekee sehemu alipokuwa amekaa mschana huyo ingawa hakwepo tena!
“MZIMUUUUUUUUUU...”
Alipiga kelele kwa nguvu mpaka na wale waliokuwa wanapigana wakaachana!
“Mzimu?”
Walianza kuulizana wao kwa wao bado hawakujua mwenzao alimaanisha nini?
“We chale mzimu upo wapi?”
Mmoja akaulizwa.
“Nyie bado mnamwona yule demu hapa?”
Swali hilo likawafanya wote waelekeze mboni zao mahali alipokuwepo Angel...
Hawakumuona!
Daah!
Kwani humo ndani alibaki mtu?
Unaambiwa vijana walipoteana balaa!
Neno “Mzimu” lilimkaa kila mmoja akilini kwake kwahiyo kila mmoja akaamini kuwa kweli msichana yule alikuwa ni mzimu.
Jambo lililopelekea vijana wakimbie nusu ya kufa.

Sehemu 22 Sehemu 24
0
0