Angel - Sehemu ya Sita (06)
Hilo tu? Halikutosha! Haja zote zilimtaiti kwa mara moja!
Yaani binti wa watu alizongwa na uoga usipime!!
“Angel… Angel… Angel, Ngo! Ngo! Ngo!”
Hatimae mgongaji aliamua kuita, na huyo hakuwa mwingine alikuwa ni bibi yake Angel.
“Bee bibi.”
Angel aliitikia kivivu huku akinyanyuka kabisa kitandani.
“Uamke kuna kazi ya kufanya huko nje.”
Bibi alisema.
Angel alinyanyuka na kuvaa nguo zake kisha akatoka na kupitia sebleni ambapo alichota maji kwenye
kikombe na kutoka nayo nje.
Moja kwa moja alisogea pembeni kidogo ya uwanja wa nyumba ya babu yake huko alianza kunawa uso huku akisikilizia
kama atasikia tena vile vishindo au?
Bado vile vishindo viliendelea kusikika na safari hii vilisikika nyuma ya nyumba.
“Huyu ni babu au?”
Alijiuliza Angel huku akirudisha kikombe ndani.
Lengo lake alitaka akaweke kikombe ndani halafu aende akachungulie huko nyumba ya nyumba.
Ila sasa kwa bahati mbaya wakati anaweka kikombe pale sebleni, Bibi yake alifika hapo akitokea jikoni.
“Chukua ufagio fagia uwanja huo mi naandaa chai huko jikoni.”
Bibi alisema akimwambia mjukuu wake...
“Sawa bibi, lakini nina swali.”
Alisema Angel.
“Lipi hilo?”
Alihoji bibi.
“Hivi huko nyuma kuna vurugu za nini?”
“Hahahaha.”
Bibi alikenua mapengo yake kwa kucheka kidogo kisha akasema.
“Huyo ni babu yako anagombana na vyuma huko nyuma”
“Anagombana na vyuma?”
Angel alitaharuki, ni wazi hakumuelewa bibi yake.
“Yupo zoezini.”
Bibi alinyoosha maelezo.
Angel kusikia hivyo alishikwa na kimuhe muhe, alitamani sana kwenda kuona kile babu yake anafanya.
Macho yalijionesha wazi kabisa mbele ya bibi yake kuwa alikuwa anahitaji nini...
“Unataka kwenda kuona anavyofanya zoezi la asubuhi?”
Bibi aligonga kwenye point aliyokuwa akiifikiria mjukuu wake.
“Ndiyo bibi!”
Alijibu haraka Angel.
“Haya nenda mara moja, lakini kumbuka una kazi huku.”
Bibi alisema.
Kusikia hivyo Angel alitimka fasta sana mpaka huko nyuma ya nyumba.
Huko alimkuta babu yake akiwa ndani ya pensi na singlend, mzee anakula mazoezi ya kufa mtu!
“Babuuu….. Hahahaha!!”
Angel alijawa na kicheko pindi alipomwona babu yake akitoa jasho ingali ni asubuhi...
“Angel mjukuu wangu umeamka?”
Babu alimuuliza mjukuu wake huku akitua chini mzigo wa chuma la kilo 30 alilokuwa kalibeba.
“Ndiyo babu nimeamka! Daah, halafu babu umenishtua sana!”
“Na nini tena mjukuu?”
Babu alimuuliza mjukuu wake huku akimtizama usoni.
“Si ile naamka tu usingizini nakumbana na sauti za vishindo nje ya nyumba?”
“Kwahiyo ulijua umevamiwa?”
Babu aliuliza!
“Kwanini nisifikiri hivyo sasa?”
Angel alisema!
“Ahahahaha… Nani huyo kwanza haogopi?”
Babu alijibu kwa kujigamba!
“Hata majambazi.”
Angel alisema kwa bashasha.
“Mjukuu wangu mi nimepitia jeshi bwana!”
“Jeshi?!”
“Ndiyo!”
“Tangu nimezaliwa na kuliona jua mpaka leo hii nipo hivi sijawahi kusikia kama babu alikuwa mjeda.”
Aliongea Angel huku akimtizama babu yake kwa taharuki.
“Ooh! Ahahaha… Jeshi la mgambo mjukuu wangu!”
Babu alisema!
“Aaah! Babu bwana kumbe mgambo?”
Angel aliuliza!
“Eeh yaani huu mtaa wananiogopa kama simba!”
Babu alijigamba!
“Kwa lipi?!”
Angel aliuliza kimzaha.
“Atakaeleta fujo tu, nikienda kumkamata kabla ya kumfikisha kwenye vyombo vya sheria lazima kwanza nimpe adhabu ya maana!”
“Kama?”
“Tukielewana nampigisha Push Up kumi na viboko Kumi pia!”
“Na akibisha je?”
Angel alihoji huku kashika kiuno!
“Atanitambua!”
Babu alijibu kisha akaendelea na zoezi lake kama kawaida.
Angel aliendelea kumtizama babu yake anavyotoa jasho pale.
Baadae akaondoka zake kwani alikumbuka kuwa bibi yake alikuwa amempatia kazi ya kufanya asubuhi ile.
Babu yeye aliendelea na tizi kama kawaida yake mpaka pale alipokamilisha zoezi kwa kuridhika ndipo akana nayo.
“Mazoezi hujenga mwili sana na kufanya mtu aishi bila kupatwa na presha au shida yoyote ile kama vile kusumbuliwa na maradhi ya
kisukali na kadharika.”
Alikuwa akiyawaza hayo binti Angel wakati huo akiendelea kufanya usafi wa nje ya nyumba kwa kufagia matakataka yaliyoletwa na upepo wa usiku.
Bibi yake alikuwa ameelekea sokoni kama kawaida yake huku nyuma akiwa kaacha maagizo kwa mjukuu wake Angel kuwa angemwandalia
babu yake chakula cha machana, Kwani yeye huenda asingerudi.
Basi Angel baada ya kukamilisha maswala ya usafi wa nje alihamia ndani ambako alifagia kwa ustadi zaidi mpaka nyumba ikapendeza kabisa.
Alipomaliza huko alihamia kwenye vyombo, alikusanya vyombo vyote na kuvipeleka nje.
Aliviosha saafi mpaka vikatakata baada ya hapo akahamia jikoni.
Siku hiyo babu yake hakwenda popote zaidi ya kwenda kukaa nyuma ya nyumba yao huku akisikiliza redio asubuhi asubuhi.
“Hivi kumbe babu upo?”
Alitaharuki Angel na kuuliza baada ya kumkuta babu yake huko nyuma ya nyumba wakati alipokwenda kuchukua kuni.
“Nipo mjukuu wangu.”
Alijibu babu yake Angel.
“Chai umekunywa?”
Aliuliza tena Angel.
“Ndiyo!”
“Sawa babu.”
Angel alisema kisha akabeba kuni na kuondoka huku akimuacha babu yake akiwa bado anasikiliza redio huko nyuma ya nyumba.
Angel aliendelea kutekeleza majuktmu yake ya jikoni mpaka pale inatimia saa tano kasorobo kila kitu kilikuwa tayari.
Alikipeleka mezani kisha akaemda kuwita babu yake ili waje kula...
“Eti babu!”
Ilikuwa ni mezani wakila, Angel alionekana kuwa na jambo la kuzungumza...
“Naam mjukuu wangu.”
Babu aliitikia wito...
“Mimi nataka niwe nafanya mazoezi kama wewe!”
“Ahahahaha... Sikiliza wewe ni mtoto wa kike hauwezi.”
“Babu naweza eti.”
Angel alizidi kumshawishi babu yake amfundishe kufanya mazoezi.
“Wewe uwe unakimbia tu ila vyuma sitokuruhusu.”
Bado babu aliendelea kuweka vizingiti...
“Hata hivyo sawa.”
Angel alikubaliana na babu yake ingawa hakurizika.
Angel alitamani sana siku moja awe mwanamke wa shoka kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake.
Lakini licha ya siku hiyo kushindwa bado alijipa matumaini kuwa ipo siku angefanikiwa.
Siku zikazidi kusogea mbele.
Baadae wiki moja ikakatika tangu Angel akwame Morogoro kwa babu yake.
Rebeca alianza kuwatinga wazazi wake kumtaka binti huyo akidai ya kwamba alitakiwa kwenda kuanza masomo mapema
sana kwani tayari alikwisha mfanyia mpango wa shule.
“Atakuja wiki kesho.”
Alijibu babu yake Angel kwa njia ya simu siku moja baada ya Rebeca kupiga.
“Baba wiki ijayo ni mbali fanyeni mpango aje mapema huku si zaidi ya siku mbili.”
Unaweza pia kusoma: