Angel - Sehemu ya Ishirini na Mbili (22)
“Nini bosi?”
Huyo Juma alimuuliza Rebeca baada ya kufika ndani hapo.
“Yule binti wa hapa mgeni si unamjua?”
Akauliza Rebeca.
“Yaah! Nampata.”
Akajibu Juma.
“Amenipiga teke la kitovu yaani kaniumiza kweli.”
“Yuko wapi?”
“Amepita dirishani baada ya mimi kukuita.”
“Dirisha lipi hili au?”
Juma aliuliza na asitegee kama jibu ni ndiyo.
“Ndiyo.”
Rebeca akajibu.
“Wee!”
Juma hakutaka kuamini ikabidi asogee alione vizuri kwa maana anajua madirisha ya nyumba hiyo yapo juu sana.
“Kapita hapo we bosi?”
“Ndiyo Juma.”
Akajibu Rebeca.
“Huyu si profeshno kabisa?”
Akajiuliza Juma maana haikuwa kawaida licha ya mwanamke hata mwanaume kupita sehemu kama ile.
“Kwahiyo nimfuatilie?”
Akauliza Juma.
“Hapana kwa kuwa keshakimbia na ni usiku basi achana nae tutangalia utaratibu wa kumfuatilia kesho.
Naomba unipeleke chumbani kwangu.”
“Sasa mbona hauna nguo?”
Akauliza Juma kwa mshangao.
“Kulikuwa na dharura huku.”
Akajibu jibu la uwongo Rebeca.
Basi Juma akafanya vile alivyoagizwa na kumfikisha Rebeca chumbani kwake kisha yeye akarejea lindoni kwake.
Asubuhi na mapema...
Rebeca alikuwa ni mtu wa kwanza kuamka.
Aliamka kitandani huku bado akiyasikia maumivu ya kitovu pale alipopigwa teke na Angel.
“Halafu huyu mtoto kaenda wapi sasa?”
Alianza kujiuliza Rebeca.
Akajikongoja mpaka kwenye mlango wa chumba cha mfanyakazi wake wa ndani Agnes na kugonga mlango.
“Bosi.”
Akaitikia Agnes kwa kusema bosi.
“Hebu amka mara moja.”
Akasema Rebeca.
“Sawa bosi.”
Akajibu Agnes huku akikurupuka kabisa.
“Unasikia we Agy?”
“Abee!”
“Hebu naomba unichemshie maji mara moja.”
“Maji tu?”
“Ndiyo.”
“Sawa.”
Akajibu Agnes wakati huo akimalizia kuvaa tisheti.
Basi baada ya Rebeca kukamilisha maagizo hayo kwa Agnes yeye akaondoka na kutoka nje.
Alizunguka mpaka nyuma ya nyumba usawa wa kilichokuwa chumba cha Angel.
Akasogelea kabisa mpaka dirishani...
Gafla macho yake yakaganda chini kwa mda wa sekunde tano kavu huku akiwa kayatumbua haswaa!
Mwishowe hofu kubwa sana ilianza kumtawala moyoni sambamba na mikono kuanza kumtetemeka.
Nguvu zikaanza kumwishia, miguu nayo ikaanza kumsaliti kwa kukosa nguvu za kuuhimili mwili wake.
Taratibu Rebeca alikaa chini huku akiwa kashikilia kichwa asitake kuamini kwa kile kinachokwenda kumtokea katika maisha yake.
Kitu kilichopelekea Rebeca kukumbwa na hali ile ni baada ya kuona risasi ya bastola ikiwa chini pale bila bastola yenyewe.
Mmmh!
Pale pale akakumbuka kuwa kuna muda Angel alirusha bastola ya John nje kabla hajaondoka, sasa swali likamjia kuwa je?
John alipotoka kule chumbani alikumbuka kwenda kuichukua bastola hiyo?
Rebeca hakupata jibu.
Hapo ndipo akili ikamwambia kuwa John muda ule alikuwa na haraka sana si rahisi kama aliikumbuka bastola hiyo.
Sasa swali likaja...
Je kama John alisahau bastola hiyo na hakuichukua sasa imekwenda wapi?
Rebeca akajua moja kwa moja Angel aliichukua bastola hiyo na huenda akaenda nayo polisi kwenda kushitaki kwa tukio alilotaka
kufanyiwa!
Aisee!
Rebeca alipolipata wazo hilo alichanganyikiwa kiasi ambacho haijawahi kumtokea tangu azaliwe.
Hata kichwa kikaanza kumuuma.
Hakujua kama huo msala huo angeuzima vipi iwapo kweli ingekuwa hivyo.
“Angel acha usifanye hivyo utaniangamiza shangazi yako.”
Alijisemea hivyo Rebeca huku akianza kurudi chumbani kwake haraka sana.
Lengo lake lilikuwa ni kumpigia John na kumueleza kuhusu jambo hilo.
Alifika mpaka chumbani kwake na kuchukua simu yake.
Haraka sana bila kupoteza muda alianza kuitafuta namba ya John.
Akaiona!
Bila kupoteza muda alipiga simu.
Simu ilianza kuita...
Cha ajabu sasa simu iliita muda mrefu sana bila kupokelewa.
“John pokea simu jamani.”
Rebeca alianza kuhaha huku akizunguka zunguka huku na kule ndani ya chumba chake kama mwehu.
“Hallo!”
Mwishooni karibia ya simu kukata ndiyo anakuja kupokea.
“Ee.. Baba za asubuhi?”
“Njema.. Mbona mapema mapema nini tena?”
Akauliza.
“Kuna tatizo...”
Akasema Rebeca huku akihema kwa nguvu.
“Tatizo? Tatizo gani tena?”
Akauliza John kwa taharuki.
“Hivi bastola yako jana ulikwenda kuichukua?”
“Aaaam ndiyo kwani vipi?”
Akajibu John huku akiwa makini kumsikiliza.
(Akashusha pumzi zito) “Lo! Nilianza kuchanganyikiwa hapa mimi.”
“Kwanini?”
“Aa unajua muda ule umetoka nami nimezingua na kale kaschana kakanikimbia halafu alipita dirishani.
Sasa leo wakati nafanya ukaguzi wa mazingira kule nyuma ya nyumba nimekutana na risasi tupu eneo la dirishani.
Vile nimechanganyikiwa mie hatari kabisa.”
“Hahaha...
Ulijua amekwenda nayo ili baadae aje kukushuti?”
Akauliza kiutani John.
“Halafu hata sijafikiria hilo, mi nilijua atakwenda nayo polisi...
Yaani hapo sasa ndiyo ingekuwa majanga.”
“Ahyaa! Umewaza mbali.”
“Sana!”
“Usihofu ninayo.. Ila hiyo risasi itunze...
Ilidondoka kutoka kwenye bastola pindi alipoirusha.”
“Kuhusu hilo usipate shida utaikuta...
Vipi sasa safari ya South imeingia mdudu?”
“Hapana tunaenda hivi ndiyo tupo airpoti hapa KIA.”
“Ooh! Sawa safari njema John.”
Unaweza pia kusoma: