Angel - Sehemu ya Ishirini na Tano (25)
Akasema mwanaume huyo.
“Mungu wangu Rebeca katuma watu wanifatilie.”
Alijisemea Angel huku moyo ukianza kumwendea mbio mbio...
“Nilimfuatilia tangu sehemu moja hivi mpaka anashuka hapa stendi ya ubungo wahi wahi wenda akapanda basi huyu.”
Akahitimisha...!
Angel akaona sasa anakwena kukamatwa kwani huyo aliekuwa anazungumziwa ni yeye kabisa.
Daah!
Ilibidi atoke haraka sana kabla mambo hayajaharibika.
Alitoka pale kwa hatua za haraka mpaka getini.
Sasa ile kufika getini akakutana uso kwa uso na Rebeca nae akiingia humo kwa mwendo wa haraka haraka huku akiwa na maaskari wawili wa kike.
Ayaaaa!!
Angel alichanganyikiwa mno!
Akajua kiama hiki hapa...
Asee!
Lakini kumbe kwa bahati nzuri ni kwamba Rebeca alikuwa hajamwona hivyo walipishana point ndogo sana!
Hakumwona kwa sababu yeye akili zake zote zilikuwa kule alikopigiwa simu, alijua atamkuta huko na kumtia mbaroni.
Baada ya Rebeca na wale maaskari kupita, Angel alishusha pumzi kubwa na kisha kutoka nje ya stendi hiyo haraka sana.
Baada ya kutoka hatua kadhaa alisimama na kuangaza macho yake huku na kule akitafuta mwelekeo.
“Ngoja nielekee hivi.”
Alijisemea na kisha kuipa akili uongozi, imwongoze.
Basi kwa mwendo wa haraka na uliojaa mashaka akaanza kukatiza mitaa huku asijue anakoenda.
Alikata mitaa kama mitatu hivi akakutana na kijiwe cha boda boda, akili ikamtuma asogee mahali pale.
“Kaka za saa hizi.”
Alisalimia Angel.br>
Alimsalimia mpiga boda boda mmoja ambae alikuwa amelala juu ya boda boda yake huku akichati.
“Ahaa.. Safi dada karibu.”
Mwendesha boda boda huyo aliipokea salamu hiyo kwa uchangamfu mkubwa huku akiinuka kabisa.
“Asante.. Nataka kufika barabara ya kwenda Tanga.”
“Ahaa, hapo nitoe buku dada angu nakukimbiza.”
Elfu moja kwa Angel haikuwa changamoto, alimwamuru awashe pikipiki waondoke.
Pikipiki ikawashwa Angel akapanda kisha wakaondoka...
Dakika kumi wakafika, Angel alimlipa boda boda huyo ujira wake kisha wakaachana ye akaondoka.
Sasa Angel akabaki barabarani hapo huku akiendelea kuwa makini mno na kila aliemwona.
Rebeca alikuwa amechukua barua kituoni huku akiwa amepeleka na mashtaka dhidi ya mschana huyo aitwae Angel.
Alidai kuwa mschana huyo alitoweka usiku wa kuamkia siku hiyo huku akiwa ameiba kiasi cha pesa isiyopungua laki sita.
Rebeca anadai kuwa pesa hiyo alikwenda kuihifadhi nyumbani siku hiyo baada ya kwenda kuitoa benki na ilitakiwa kwenda kwenye
mfuko wa shule kwaajili ya kusaidia watoto yatima.
Rebeca aliripoti kuwa pesa hiyo ilitolewa na kampuni moja inayojihusisha na masuala ya kibiashara, anadai kuwa yeye na
wasimamizi wa kampuni hiyo ni marafiki mno kwahiyo waliamua kumpa msaada wa kibinadamu ili aweze kuwasaidia watoto yatima
walio katika shule aifundishayo.
Alipoulizwa kuhusu kampuni hiyo na wahusika, alijibu kuwa kampuni hiyo ya kibiashara ilikuwa na makao yake huko Cape town,
South africa na alidai kuwa ni wafanya biashara wa madini.
(Maana ake hapo alishatengeneza ushahidi wa kutosha na kama bado angeendelea kuhojiwa zaidi basi angempigia John yeye ajifanye kama
ni mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo, jambo ambalo lilikuwa ni uwongo mtupu.)
Kufuatia madai hayo na kiasi cha pesa kilichotajwa, pamoja na mahali zilipotakiwa kwenda Polisi wakawaka.
Simu zikapigwa kila sehemu, polisi wote waliokuwa sehemu mbali mbali za mji walipewa taarifa juu ya mschana huyo
anaetafutwa kwa kutoroka na hela za uma.
Wakati huo huo ndipo Rebeca alipowasiliana na mwanaume mmoja hivi aliekuwa anafahamiana nae na anamfahamu kuwa ni
moja kati ya wapelelezi wazuri sana.
Aliwasiliana nae na kumwambia kuwa alikuwa akimtafuta mschana aliekuwa amevaa tishet jeupee lenye lebo ya AS,
modo nyeusi ya mpira na raba za kufunga na kamba miguuni, pia alikuwa na begi jeusi mgongoni.
Yaani alimwelekeza vizuuri jinsi Angel alivyokuwa kuwa na akamwahidi kitita kinono sana iwapo angefanikiwa kumuona na
kumpatia taarifa.
Mwanaume anaingia kazini, anafanikiwa kumwona na anamfwatilia mpaka Ubungo stendi huku akiwasiliana na Rebeca kwa njia ya simu...
Lakini bahati nzuri au mbaya...
Angel anamwona mtu huyo na kumtilia shaka akiwa pale ubungo.
Ni kweli baada ya kumchunguza anabaini ni mtu anaewasiliana na Rebeca, anafanikiwa kumkwepa na kumkimbia ingawa
ananusurika kuonwa na Rebeca baada ya kupishana nusu hatua wakati anatoka.
Rebeca akafika na timu yake mpaka mahali alipokuwa mwanaume huyo...
“Yupo wapi?”
Akauliza...
“Aah! Kanipotea wakati naongea na simu.”
Akajibu mwanaume huyo na kufanya Rebeca akunje uso...
“Lakini hajaenda popote yupo hapa hapa karibu.”
Akaongezea.
“Tumtafteni... Tumtafteni.”
Rebeca akaamuru.
Msako mkali ukazuka walimtafuta sana ndani ya ubungo na wasimuone.
“Vipi mama mbona unaonekana kuchanganyikiwa?”
Raia mmoja alipata kumuuliza Rebeca.
“Kuna mschana katoroka sasa nimepata taarifa yupo hapa ubungo.” (akataja na mavazi aliyovaa na kila kitu.)
“Kheee! Huyo dada mbona keshatoka kitambo sana?”
Dooh!
Rebeca akaishia kushika nyonga...
“Hahalafu unajua nini? Mmepishana nae palee.”
“Wapi?”
“Palee... We unaingia ye anatoka yaani mmepishana nusu hatua.”
“Shiiit.”
Haraka sana Rebeca akatoa simu yake na kupiga sehemu.
“Amekwisha toka huyu hayupo humu.”
Aliongea Rebeca baada ya simu kupokelewa upande wa pili.
“Tena?”
Ilisikika sauti ya kiume upande wa pili, bila shaka ndiyo yule mpelelezi.
“Ndiyo, nimepata taarifa hapa kumbe katoka muda ule ule.”
“Akaaa! Sasa we upo maeneo gani?”
“Hapa zinapopaki bajaji.”
“Nakuja sasa hivi.”
“Sawa nakusubili.”
Sekunde kadhaa yule mwanaume alifika mahali alipokuwa Rebeca.
“Ameshatoka kashtuka huyu.”
Alisema Rebeca.
“Daah! Asa atakuwa kaelekea wapi tena?”
“Huyu lengo lake anataka kwenda Morogoro sasa cha kufanya we si una gari?”
“Ndiyo.”
“Wahi barabarani atakuwa mbele huko hana pa kwenda huyu.”
“Eti?”
“Ndiyo nenda na uwe makini pembezoni mwa barabara nina uhakika yupo mbele huko.”
“Wacha niwahi.”
Unaweza pia kusoma: